KUPANDA MBINGUNI

KUPANDA MBINGUNI

 

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumuongoza, Hufungulia kifua chake Uislamu; na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumhukumu kupotea, Hufanya kifua chake kizito kinaona tabu kubwa (kufuata huo Uislamu); kama kwamba anapanda mbinguni (kusikokuwa na pumzi). Namna hivi Mwenyezi Mungu Anajaalia uchafu juu ya wale wasioamini.   Aya ya 125 Suratul An-am.

UKWELI WA KISAYANSI:

        Ujuzi juu ya mpangilio wa anga ulikuwa haupo hadi Pascal alipothibitisha mwaka 1648 kuwa shinikizo la hewa hupungua kila unapokwenda juu ya usawa wa bahari. Ikabainika baadae kuwa hewa iko kwa wingi zaidi katika tabaka za chini ya angahewa  Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Basi yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumuongoza, Hufungulia kifua chake Uislamu; na yule ambaye Mwenyezi Mungu Anataka kumhukumu kupotea, Hufanya kifua chake kizito kinaona tabu kubwa (kufuata huo Uislamu); kama kwamba anapanda mbinguni (kusikokuwa na pumzi). Namna hivi Mwenyezi Mungu Anajaalia uchafu juu ya wale wasioamini.   Aya ya 125 Suratul An-am.

UKWELI WA KISAYANSI:

        Ujuzi juu ya mpangilio wa anga ulikuwa haupo hadi Pascal alipothibitisha mwaka 1648 kuwa shinikizo la hewa hupungua kila unapokwenda juu ya usawa wa bahari. Ikabainika baadae kuwa hewa iko kwa wingi zaidi katika tabaka za chini ya angahewa, hukusanyika asilimia hamsini (50%)  ya gesi za anga baina ya usawa wa ardhi na urefu wa futi elfu ishirini (20,000) juu ya usawa wa bahari, na asilimia tisini (90%) baina ya usawa wa ardhi na urefu wa futi elfu hamsini (50,000) kwenye usawa wa ardhi. Kwa hiyo wingi wake hupungua kila unapopanda juu kwa ujumla. Na hewa hugotagota kwa kiasi kikubwa katika tabaka za juu kabla ya kupotea kabisa katika anga. Na kuwepo kwa binadamu katika muinuko usiopindukia futi elfu kumi (10,000) juu ya usawa wa bahari, hakumsababishii tatizo lolote. Chombo cha kuvutia pumzi kinaweza kuzoea kwenye urefu kati ya futi elfu kumi  na ishirini na tano (10,000 – 25,000). Binadamu kila anapopaa juu mbinguni, basi hupungua shinikizo la anga na hupungua kiasi cha oksijeni, jambo ambalo husababisha kubanwa kwa kifua na tabu kubwa ya kuvuta pumzi huzidi kutokana na haja kubwa ya tishu (mkusanyiko wa seli mwilini) ya oksijeni. Iwapo isipokuwepo na seli za mwili kuzidi kuhitaji ili zifanye kazi zake wakati inapozidi kupanda juu, hupatwa na hali mbaya mno ambapo uvutaji pumzi huchafuka (Oxygen Starvation). Kwa sababu ya upungufu mkubwa wa oksijeni, binadamu wakati huo hupatwa na kufeli kwa chombo cha kuvutia pumzi (Respiratory System) na huangamia.

UPANDE WA MIUJIZA: 

         Ni wazi kuwa binadamu wakati wa wahyi,  hakujua suala la mpangilio wa gesi  ya angahewa katika tabaka zake tofauti, na kwa hiyo hali ya kupungua kwa shinikizo katika tabaka za juu na kupungua kiasi wingi wa gesi ya oksijeni ya lazima kwa uhai kila binaadamu anapozidi kupanda angani, na kwa hiyo hajui athari za hayo kwa uvutaji wa pumzi na kubakia uhai, kwani humalizikia kufeli kwa chombo cha kuvutia pumzi. Bali kinyume cha hivyo, watu walikuwa wakidhani kuwa kila binadamu anapozidi kwenda juu kifua chake hutanuka zaidi na kuzidi kufurahia hewa safi.

         Aya tukufu inaashiria kwa uwazi kabisa mambo mawili yaliyogunduliwa  na sayansi mpya. Kwanza ni kubanwa kwa kifua na uzito wa kuvuta pumzi kila binadamu anapozidi kupanda juu katika tabaka za anga. Iliyobainika ni kuwa hutokea kwa sababu ya kupungua kwa oksijeni na kushuka kwa shinikizo la hewa angani. Pili ni hali mbaya inayotangulia mauti, ni kubanwa kwa pumzi wakati anapojaribu kupanda tabaka za anga futi elfu thelathini, kwa sababu ya kushuka sana kwa shinikizo la anga na upungufu mkubwa wa oksijeni ya lazima kwa uhai hadi kumalizika kwa oksijeni ndani ya mapafu na binadamu kufikwa na mauti na kuangamia.

         Mbali na neno (anapanda mbinguni) ambapo kwa maana yake ya Kiarabu inaongeza uzito wakati wa kupanda. Na huu ni wasfu wa kina wa mashaka na machungu yanayoambatana na tukio. Hivyo inawezekana habari za ukweli huu kuwa chengine isipokuwa ni wahyi toka kwa Mwingi wa kujua na Mwingi wa habari.