Ujumbe mmoja

Kitabu hiki kinazungumzia: Umuhimu wa tawhidi ya kweli na kwamba Mitume wote wa Allah walitumwa kuja kuwafundisha watu tawhidi ya kweli nayo ni kumuabudu Allah peke yake na kujiepusha na shirki.


Ujumbe Mmoja

[Swahili- Kiswahili سواحيلي -]

 


        
Mtunzi:
Dr. Naaji Bin Ibrahim Arfaj




Mfasiri:
 Yasini Twaha Hassani.


Kimerejewa na:
Yunus Kanuni Ngenda.
Saada Harun Yunus
Abubakari Shabani Rukonkwa.

 


رسالة واحدة فقط

المؤلف:
دكتور/ ناج بن ابراهيم أرفج
المترجم:
ياسين طه حسن

المراجع:
يونس كنون نغندا
سعادة بنت هارون يونس
أبوبكر شعبان ركونكوا.

 

 

 

بسم الله الرحمن الرحيم

Ujumbe Mmoja


    YALIYOMO KATIKA KITABU

Maswali kabla ya kusoma……………………………………....3
Kiini cha mada………………………………….........................3
Tauhidi katika kitabu kitakatifu (Agano la kale)……………….8
Tauhidi katika kitabu kitakatifu (Agano jipya)………………...9
Tauhidi katika Qur-an Tukufu………………………………...10
Hitimisho……………………………………………………...11

 

 

 

 

 

MASWALI KABLA YA KUSOMA.
1: Kuna malengo gani kwenye ujumbe huu mmoja?
2: Kinasemaje kitabu kitakatifu kuhusu hilo?
3: Qur-an inasemaje kuhusu hilo?
4: Ipi rai yako baada ya hapo?

KIINI CHA MADA:
Baada ya kuumbwa Adam (s.a.w), ujumbe mmoja wamepewa watu karne na karne, kuna umuhimu wa kuwakumbusha watu ujumbe huu na kuwaweka katika njia iliyo nyooka, amewatuma Mwenyezi Mungu mmoja wa kweli Manabii na Mitume kama vile Adam, Nuuh, Ibrahim, Mussa, Issa na Muhammad (s.a.w), ili wafikishe ujumbe mmoja nao ni: (Mungu wa kweli ni mmoja tu muabuduni).
Mungu mmoja wa kweli ndiye (Muumbaji) na ndiye muabudiwa.

Afikishe ujumbe huu    Amemtuma Mtume
Mungu ni mmoja muabuduni Mwenyezi Mungu    Nuuh (s.a.w)
Mungu ni mmoja muabuduni Mwenyezi Mungu    Ibrahim (s.a.w)
Mungu ni mmoja muabuduni Mwenyezi Mungu    Mussa (s.a.w)
Mungu ni mmoja muabuduni Mwenyezi Mungu    Issa (s.a.w)
Mungu ni mmoja muabuduni Mwenyezi Mungu    Muhammad (s.a.w)

Kwa hakika Mwenyezi Mungu ametuma Mitume wastahamilivu na wengineo tunaowajua na tusiowajua miongoni mwa Manabii wake na Mitume wake, ili watekeleze mambo mengi yakiwemo:
1: Kupokea wahyi wa Mwenyezi Mungu na kuwafikishia watu wao na wafuasi wao.
2: Kuwafundisha watu tauhidi na kutakasa ibada zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
3: Wawe ndio kiigizo chema kwa kauli na matendo ili watu wawaige katika njia ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu.
4: Kuwaelekeza wafuasi wao namna ya kumuogopa Mwenyezi Mungu na kumtii na kufuata amri zake.
5: Kuwafundisha wafuasi wao mambo ya dini na tabia njema.
6: Kuwaongoza wafanyao maasi na washirikina wanaoabudu masanamu na wengineo.
7: Kuwaambia watu ya kwamba watafufuliwa baada ya kufa kwao na watahesabiwa siku ya kiyama kutokana na matendo yao, atakayekuwa amemuamini Mwenyezi Mungu peke yake na akafanya matendo mema malipo yake ni pepo, na yeyote atakae mshirikisha Mwenyezi Mungu na akamuasi mafikio yake ni motoni.
 Kwa hakika Manabii hao na Mitume hao amewaumba na amewatuma Mungu mmoja tu.
Kwa hakika ulimwengu na viumbe vilivyomo vinakubali kuwepo Mungu muumbaji na vinashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja tu, Mwenyezi Mungu ndiye aliyeumba ulimwengu na vilivyomo miongoni mwa binadamu na wanyama na wadudu. Naye ndiye aliyeumba kifo na uhai wenye kumalizika na maisha ya milele.
Kwa hakika vitabu vitakatifu upande wa Mayahudi na Manaswara vyote vinashuhudia uwepo wa Mwenyezi Mungu na kumpwekesha.
Kwa hakika yule anaetafuta haki atakapo soma maana ya Mungu kwa kina na ukweli kabisa katika vitabu vitakatifu na Qur-an Tukufu ataweza kupambanua sifa maalum zinazo muhusu Mwenyezi Mungu bila ya kushirikiana na miungu ya uongo. Na hizi ni baadhi ya sifa:
1: Mwenyezi Mungu wa kweli ndiye muumbaji na siyo kiumbe.
2: Mwenyezi Mungu wa kweli ni mmoja hana mshirika, na siyo zaidi ya mmoja hakuzaa wala hakuzaliwa.
3: Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakasika kutokana na taswira ya viumbe, hadirikiwi (haonekani) na macho hapa duniyani.
4: Mwenyezi Mungu ni wa enzi, hafi wala hajitokezi au kujifananisha na maumbile ya viumbe vyake.
5: Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kutegemewa na viumbe mwenye kujiendesha, mwenye kujitosheleza na viumbe wake, havihitajii hana mzazi wa kike wala wa kiume wala mke wala mtoto, hahitaji kula wala kunywa wala msaada wa yeyote. Lakini viumbe vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu ni vyenye kumuhitaji.
6: Mwenyezi Mungu ni mwenye kutakasika kwa sifa za ukamilifu asizo shirikiana wala kushabihiana na yeyote katika viumbe wake, hakuna anaye fanana nae.
Na yawezekana kutumia sifa hizi na sifa nyinginezo zinazo muhusu Mwenyezi Mungu peke yake katika kfichua na kupinga miungu yote inayodaiwa ya uongo.
Na sasa niacheni narudi kwenye ujumbe mmoja uliotajwa hapo juu ili nichukue baadhi ya dalili kutoka katika kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu zinazo tilia mkazo ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja. Na kabla ya yote napenda nikushirikisheni katika fikra hii: "Kuna baadhi ya wakristo wanadai kwamba Mungu ni mmoja na wao wanamwamini Mungu mmoja"
Na ukweli uliopo katika kusoma kwangu sana kuhusu ukristo na mjadala pamoja na wakristo nimekuta kwamba "Mwenyezi Mungu" kwa upande wao anafungamana na mambo yafuatayo:
1: Mungu Baba.
2: Mungu Mwana.
3: Mungu Roho Mtakatifu.
Kwa hakika kwa maumbile ya kawaida na akili iliyokuwa safi inampelekea mpekuzi wa mada hii kuwauliza maswali mengi wakristo:
 Nini maana yenu kusema ya kwamba "Mungu ni mmoja" wakati nyinyi mnaashiria miungu watatu?
Je! Mwenyzi Mungu ni mmoja kagawanyika katika utatu au utatu umekuwa kitu kimoja (1 katika 3 au 3 katika 1)?
Ukijumlisha hayo na ukizingatia itikadi ya baadhi ya wakristo kwamba miungu hawa watatu wana kazi maalum wana sifa maalum na namna maalum kama ifuatavyo:
1: Mungu Baba = ndiye muumbaji.
2: Mungu Mwana = ndiye mwokozi.
3: Mungu Roho mtakatifu = ndiye mshauri.
Kwa hakika madai ya wakristo ya kwamba Yesu ni mwana wa Mungu, au ni Mungu, au ni sehem ya Mungu, yanapingana na yale yaliyoelezwa katika Taurati na Injili, kwasababu imeelezwa ya kwamba Mwenyezi Mungu hatoonekana na yeyote hapa duniani: "Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona. " (Yohana 5:37).
" Ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina " (waraka wa kwanza kwa Timotheo 6:16).
" Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi (Kutoka 33:20).
Tukiziangalia hizi dalili na nyinginezo kwa hakika mimi naona ajabu sana na kujiuliza maswali kwa ukweli na uaminifu vipi tunaweza kuoanisha maneno ya wale wanaosema ya kwamba Issa (Yesu) ni Mungu na dalili za kitabu kitakatifu zinazo elezea na kuthibitisha ya kwamba hakuna yeyote aliyemuona Mwenyezi Mungu wala kusikia sauti yake?!.
Je! Mayahudi hawakumuona Issa (Yesu) (Mungu mwana kama wanavyo itakidi baadhi yao) kipindi kile na familia yake au wafuasi wake na kusikia sauti yake?
Kwanini Taurati na Injili vinaeleza ya kwamba Mwenyezi Mungu hajaonekana na yeyote wala kumsikia, kisha tunaona ya kwamba Issa (Yesu) waliomuona na kumsikia sauti yake wanaitakidi kuwa ni Mungu au mtoto wa Mungu? Je! Kuna siri iliyojificha kuhusu ukweli wa Mwenyezi Mungu?
Taurati inaelezea kinyume cha hayo inanukuu kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: " Sikusema kwa siri, katika mahali pa nchi ya giza; sikuwaambia wazao wa Yakobo; Nitafuteni bure; Mimi, Bwana, nasema haki; nanena mambo ya adili (Isaya 45:19).
Ikiwa ndivyo uhakika uko wapi? Samahani soma dalili zilizo tangulia vizuri zaidi ya mara moja na ufikirie vizuri kwa umakini.
Na tuondoke pamoja katika msafara wa kutafuta ukweli kuhusu Mwenyezi Mungu katika kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu nikitaraji mtakubaliana nami kutokana na rai zenu na muono wenu baada ya kuzingatia kwenu Aya na dalili na kusoma kwenu kitabu hiki kwa mazingatio na kutafuta haki.
Kwa kuchunga mada tuliyonayo nitataja dalili bila ya kuweka nyongeza yoyote nataraji mazingatio kwa umuhimu wa mada hii.

 


MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA (Agano la kale):
" Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. (Kumbukumbu la torati 6:4).
"Je! Mwenyezi Mungu mmoja hajatuumbia roho ya maisha na kuturuzuku"?. (Malaki 2:15).
" Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi ". (Isaya 43:10-11).
" Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. "?. (Isaya 44:6).
" Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, Bwana? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi. (Isaya 45:21).
Je! Unakumbuka dalili nyingine kama hizo.
MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA (Agano jipya):
" Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma (Yohana 17:3).
" Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake " (Matayo 4:10).
" Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye ".
 (Marko 12:28-33).
" Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu " (waraka wa kwanza kwa Timotheo 2:5).
"16 Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri Akamwambia, Zipi? Yesu akasema, Ni hizi, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo." (Matayo 19:16-17).
Je! Unaweza kutaja dalili zingine zinazo thibitisha ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja na sio watatu?.
MWENYEZI MUNGU NI MMOJA WA KWELI KATIKA QUR-AN TUKUFU.
Amesema Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja). (Surat Ikhlas 1-4).
(Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu). (Surat Ambiyaa 25).
(Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru). (Surat Maida 73).
(Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja).
(Surat Sswafaat 4).
(Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli). (Surat Nnamli 64).
Kwa hakika ujumbe huu (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ndiyo mada ya msingi ndani ya Qur-an Tukufu.


HITIMISHO
Kwa hakika dalili hizi na nyinginezo nyingi katika kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu zinaonyesha yasiyokuwa na shaka ndani yake ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja hakuna mwingine zaidi yake, kitabu kitakatifu kinasema: " Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye ". (Marko 12:28-33).
Na Qur-an Tukufu inataja jambo hili katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee). (Surat Ikhlas: 1).
Na kitabu kitakatifu hakitilii mkazo ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja tu bali kinatilia mkazo pia ya kwamba Mwenyezi Mungu ndiye muumbaji na muokoaji pekee, "Ninyi ni mashahidi wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni Bwana, zaidi yangu mimi hapana mwokozi ". (Isaya 43:10-11).
Kwa sababu hiyo inabainika ya kwamba Uungu wa Issa (Yesu) au Roho mtakatifu au wengine tofauti na hao wawili hauna mashiko, wala dalili juu yake hawakuwa isipokuwa ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu, hawana chochote katika maamrisho, wao si waungu wala hawafananishwi na Mungu. Hakuna kinacho fanan nae kwa mujibu wa kitabu kitakatifu na Qur-an Tukufu.
Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewakasirikia Mayahudi kwa sababu ya upotevu wao na kuabudu miungu tofauti pamoja na Yeye, "Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israili" (Hesabu 25:3), na akaharibu Mussa (s.a.w) ndama yao ya dhahabu.
Kwa upande mwingine  wamepata adhabu na mateso baadhi ya wakristo waliokuwa wakimpwekesha Mwenyezi Mungu, yote hayo ni kwasababu wameamini tauhidi ya Mwenyezi Mungu na wakakataa kubadilisha mafundisho sahihi ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu ya Nabii Issa (s.a.w) na wakakanusha uzushi wa utatu mtakatifu ulioanzishwa na Paulo na wafuasi wake.
Muhtasari wa maneno Mwenyezi Mungu amemtuma Adam na Nuuh na Ibrahim na Mussa na Issa na Muhammad (s.a.w) kuwalingania watu katika imani ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtakasia ibada yeye peke yake hana mshirika wala mwenza utakasifu ni wake. Huu ndio ujumbe wao wote.

Mungu wa kweli ni mmoja tu muabuduni peke yake.
Kwa hali namna ilivyo ni kwamba ujumbe wa Manabii na Mitume ni mmoja kwa sababu hiyo na dini yao ni moja. Ikiwa ndivyo ni ipi dini ya hao Manabii na Mitume?.
Kwa hakika kiini cha ujumbe wao kinasimama juu ya "kujisalimisha" kwa Mwenyezi Mungu, hili ndilo neno linalobeba maana ya "Uislam" na ndivyo lilivyoeleweka katika lugha ya kiarabu.
Na kwa hakika Qur-an imaetilia mkazo ya kwamba Uislam ndiyo dini ya haki kwa Manabii wote wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na tunaweza kufuatilia uhakika huo uliopo ndani ya Qur-an kwenye kitabu kitakatifu pia. (Tutafatilia uhakika huo katika kitabu kitakatifu kijacho akipenda Mwenyezi Mungu).
Na mwisho kabisa, ni wajibu juu yetu kwa ajili ya kupata ufupisho wa maneno kuupokea ujumbe huu na kuuamini kwa ukweli na ikhlas. Lakini jambo hili halitoshi peke yake! Bali ni wajibu juu yetu pia kuamini Manabii wote wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake (na inakusanya imani hiyo kumuamini Mtume Muhammad s.a.w), na kufuata mwongozo wao na kuufanyia kazi hii ndio njia ya kupata maisha mazuri ya milele.
Ewe unayetafuta uhakika kwa ukweli kabisa na kutaka kuokoka yakupasa kutafakari katika jambo hili na kuzingatia sasa hivi kabla muda haujapita. Kabla hujafikiwa na umauti ghafla! Nani anajua lini ataondoka?.
Baada ya kutafakari na kuzingatia katika jambo hili muhimu sana na kwa akili yenye kudiriki na kwa moyo safi unaweza kuchukua uamuzi ya kwamba Mwenyezi Mungu ni mmoja hana mshirika katika Uungu wake wala mtoto, yapasa kumuamini yeye na kumuabudu peke yake na kuamini ya kwamba Muhammad ni Nabii na Mtume kama vile Nuuh na Ibrahim na Mussa Issa (s.a.w).
Na kwa sasa yawezekana ukatamka –ukitaka-maneno haya:
Ash-hadu an laa ilaha illa Llah wa ash-hadu anna Muhammada rasulu Llah. (Nakiri kwa moyo na kutamka kwa ulimi ya kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu, na nakiri kwa moyo  na kutamka kwa ulimi ya kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake).
Shahada hii ndiyo hatua ya kwanza ya kufanya kuelekea katika maisha ya milele na ndio ufunguo wa kweli wa milango ya pepo.
Na utakapokiri kufuata njia, ni juu yako kutafuta msaada kwa rafiki yako au jirani yako Muislam aliye karibu na Msikiti au kituo cha kiislam ili upate elimu zaidi.
Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
(Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu* Na rejeeni kwa Mola wenu Mlezi, na silimuni kwake, kabla ya kukujieni adhabu. Kisha hapo hamtanusuriwa* Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui).
 (Azzumar: 53-55).
Na rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimwendee Mtume wetu Muhammad bin Abdallah pamoja na familia yake na Maswahaba zake na watakao mfuata kwa wema hadi siku ya mwisho.