HISIA ZA MAUMIVU

HISIA ZA MAUMIVU

 

 Mwenyezi Mungu Amesema, “ Hakika wale waliozikataa Aya zetu, Tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao zitakapowiva, Tutawabadilishia ngozi nyengine badala ya zile; ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima.” Aya ya 56 ya Suratul Nisaa.

 Pia Mwenyezi Mungu amesema, “  Na wakanyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao.” Aya ya 15 ya Suratut Muhammad.

UKWELI WA KISAYANSI:

          Kabla ya gunduzi za kisayansi, kulikuwa na imani kuwa mwili wote ni wenye kuhisi maumivu. Haikuwa wazi kwa yeyote kuwa kuna mwisho wa nava katika ngozi ambazo zinahusika na uchukuzi wa hisia  na maumivu, hadi ulipogunduliwa mchango wa mwisho wa nava katika ngozi,  Mwenyezi Mungu Amesema, “ Hakika wale waliozikataa Aya zetu, Tutawaingiza katika moto. Kila ngozi zao zitakapowiva, Tutawabadilishia ngozi nyengine badala ya zile; ili wawe wanaonja (uchungu wa) adhabu (maisha). Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hekima.” Aya ya 56 ya Suratul Nisaa.

 Pia Mwenyezi Mungu amesema, “  Na wakanyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango zao.” Aya ya 15 ya Suratut Muhammad.

UKWELI WA KISAYANSI:

          Kabla ya gunduzi za kisayansi, kulikuwa na imani kuwa mwili wote ni wenye kuhisi maumivu. Haikuwa wazi kwa yeyote kuwa kuna mwisho wa nava katika ngozi ambazo zinahusika na uchukuzi wa hisia  na maumivu, hadi ulipogunduliwa mchango wa mwisho wa nava katika ngozi,  nacho ni kiungo muhimu mno kwani kina idadi kubwa ya nava. Dk. Head ameigawa hisia ya ngozi katika makundi mawili : Hisia nyeti (EPICRITIC)

inayohusika na kupambanua hisia ya mguso mdogo na tofauti ndogo ya joto, na hisia kuu (PROTOPATHIC) inayohusika na maumivu na kiwango kikubwa cha joto. Na kila hisia kati ya hizo mbili, inafanya kazi kwa aina tofauti ya sehemu za nava . Pia kuna seli maalumu inayohusika na ugunduzi wa mabadiliko maalumu ya mazingira (RECEPTORS). Nazo zimegawika katika sehemu nne : Seli zinazoathirika na mazingira ya nje (EXTEROCEPTORS). Hizi zinahusika na hisia ya kugusa na zinakusanya vijisehemu (MEISSNERS CORPUSCLES) na vijisehemu (MERKELS CORPUSCLES). Seli za nywele na mwisho wa (BULBES ERAUSE END) inayohusika na baridi. Silinda ya Ruffini, (RUFFINI’S CYLINDERS) inayohusika na joto. Mwisho wa nava zenye kuchukua maumivu. Ngozi ni sehemu tajiri mno kwa mwisho wa nava zenye kuchukua maumivu na joto.

          Pia wataalamu wa uchunguzi wa mwili wamethibitisha kuwa mwenye kuungua ngozi kikamilifu, basi hahisi maumivu makubwa  kutokana na kuharibika kwa mwisho wa nava wenye kuchukua maumivu, kinyume na kuungua kidogo (kiwango cha pili), kwani maumivu huwa makali zaidi kutokana na kuwa wazi kwa mwisho wa nava. Pia wataalamu wa uchunguzi wa mwili wamethibitisha kuwa michango midogo kwa ndani, haina chenye kupokea hisia wakati ambapo zipo kwa wingi kwenye eneo la kuta na eneo la nje la matumbo makubwa. Na katika eneo hilo, kuna kiasi kikubwa cha vijisehemu (vinavyofikia cubic cm 20400) ambavyo ni sawa na kiwango cha ngozi ya nje ya mwili. Pia makutanio ya maumivu (RECEPTORS) na sehemu nyengine za hisia zilizopo katika michango ya tumbo, yanafanana na zile zilizopo katika ngozi.

UPANDE WA MIUJIZA:

 (a)  Mwenyezi Mungu Amebainisha kuwa ngozi ndipo mahali pa adhabu. Akaunganisha baina ya ngozi na hisia  katika aya ya kwanza na kwamba ngozi inapowiva na kuungua na kupoteza mpangilio wake na kazi yake, basi huondoka hisia  ya maumivu ya adhabu. Basi kubadilika kwa ngozi mpya iliyokamilika mpangilio wake na iliyotimia kazi yake, mwisho wa nava – unaohusika na hisia ya joto na maumivu ya moto – hutekeleza mchango wake na kazi yake, ili kumfanya mtu huyu kafiri anayezikataa aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu aonje adhabu ya kuungua kwa moto.

Sayansi mapya imegundua kuwa mwisho wa nava unaohusika na hisia ya joto na maumivu ya kuungua, hazipo kwa wingi isipokuwa kwenye ngozi. Na hakuna hata mtu mmoja  kabla ya kugunduliwa kwa darubini na kuendelea kwa sayansi ya uchunguzi wa mwili, ambaye angejua ukweli huu ulioashiriwa na Qurani Tukufu tokea karne kumi na nne. Kama hivi unajitokeza wazi muujiza na kudhihiri dalili za  Mwenyezi Mungu .

(b)      Qurani Tukufu imewakamia makafiri kwa adhabu ya maji yachemkayo yakatayo chango zao katika aya ya pili. Imedhihirika siri ya makamio hayo mwishoni kwa kugundua kuwa chango haziathiriki na joto, lakini zikikatika, hutoka maji yanayochemka na kuingia kwenye eneo lenye kiasi kikubwa cha mapokezi ya joto na maumivu na kwenye mwisho wa nava na kufikisha kwenye ubongo. Na wakati huo mtu huhisi kiwango cha juu cha joto.

Kama hivi inadhirika wazi miujiza ya kisayansi katika hisia ya maumivu kwa kukubaliana baina ya ukweli wa tiba na miujiza ya Qurani Tukufu.