KUINGILIANA NA KUPAMBANUKA KWA MIKUSANYIKO YA BAHARI

KUINGILIANA NA KUPAMBANUKA KWA MIKUSANYIKO YA BAHARI

 

 Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Anazikutanisha bahari mbili (ya maji ya chumvi na ya maji matamu). Baina yao kuna kizuwizi, haziingiliani (zikaharibiana kabisa kabisa). Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? Katika hizo bahari mbili, hutoka lulu na marijani.”

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Haikuwa ikijulikana kuwa bahari ya chumvi ni tofauti katika mpangilio na wala sio bahari moja iliyochanganyika isipokuwa mwaka 1873 wakati msafara wa Challenger ulipozunguka katika bahari kwa miaka mitatu. Na katika mwaka 1942, 
          Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna            
Risala yetu: Kudhihirisha miujiza ya kisayansi Na kuihakiki na kuichapisha.

Lugha
    Ukurasa Kuu     Muhtasari Wa Utafiti     Kuhusu Bodi     Wasiliana Nasi      

    

KUINGILIANA  NA KUPAMBANUKA KWA MIKUSANYIKO YA BAHARI

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Anazikutanisha bahari mbili (ya maji ya chumvi na ya maji matamu). Baina yao kuna kizuwizi, haziingiliani (zikaharibiana kabisa kabisa). Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha (kuwa si neema yake)? Katika hizo bahari mbili, hutoka lulu na marijani.”

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Haikuwa ikijulikana kuwa bahari ya chumvi ni tofauti katika mpangilio na wala sio bahari moja iliyochanganyika isipokuwa mwaka 1873 wakati msafara wa Challenger ulipozunguka katika bahari kwa miaka mitatu. Na katika mwaka 1942, kwa mara ya kwanza palidhihiri matokeo ya tafiti ndefu yaliyopatikana kwa kuanzishwa mamia ya vituo vya baharini katika bahari. Wakakuta kuwa bahari ya Atlantic kwa mfano, haifanyiki na bahari moja, bali inafanyika kwa bahari tofauti. Ni bahari moja inayotafautiana mikusanyiko ya maji katika viwango vya joto, ukubwa wa eneo, chumvi, viumbe hai vya majini na kiasi cha kuyayuka kwa oksijeni. Hii ni katika bahari moja, mbali na bahari mbili zenye kutofautiana kama bahari ya Mediterranian na bahari ya Sham (Red Sea), bahari ya Mediterranian na bahari ya Atlantic, na bahari ya Sham (Red Sea) na ghuba ya Aden. Pia zinakutana katika mkondo maalumu. Katika mwaka 1942, kwa mara ya kwanza, imejulikana kuwa kuna bahari zenye kukutana maji yake, lakini baadhi yake zinatofautiana na nyengine katika sifa. Maji ya bahari si yenye kutulia, lakini daima yapo katika harakati zinazoendelea zinazoyafanya makundi ya maji kuingiliana baina yao lakini kila maji huendelea kuhodhi sifa zake katika kiasi cha chumvi, joto, wingi, kupwa na kujaa. Mawimbi, kasi za maji na pepo, vyote hivyo ni vitendakazi vyenye kuyafanya maji ya bahari daima kuwa katika harakati, lakini pamoja na hayo haichanaganyiki mikusanyiko ya bahari yenye kutofautiana sifa. Kumekuwa na kizuwizi chenye kutenganisha baina ya bahari mbili zenye kupakana katika maji au katika mkondo.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Aya tukufu zinazungumzia juu ya bahari mbili za chumvi zilizopakana zilizoingiliana na kila moja inahifadhi sifa zake, na baina yake kumekuwa na kizuwizi chenye kuzuwia zisichanganyike. Kutajwa kwa lulu na marijani katika aya tukufu, ni dalili ya kuwa ni bahari mbili za chumvi, kwani madini hizo hazipatikani isipokuwa kwenye bahari za chumvi, jambo ambalo linamaanisha kuwa mazungumzo yanahusu maji ya bahari za chumvi ambazo zinaonekana kuwa ni moja zenye sifa moja, lakini kwa hakika ni mikusanyiko inayopakana na yenye sifa tofauti.

         Bahari za chumvi zinazopakana kwa macho ya kawaida zinaonekana kama ni mkusanyiko mmoja wa maji yenye sifa moja, lakini kwa hakika  ni mikusanyiko yenye sifa tofauti katika chumvi, joto na katika wingi. Hayakufahamika hayo isipokuwa kwa kutumia teknolojia mpya. Pamoja na hayo, Qurani imezitaja sifa hizo ikajulisha kutofautiana kila bahari mbili za chumvi zenye kupakana. Kwani ni zenye kuingiliana baina yao daima na zinachanganyika, na baina yao kuna kizuwizi kinachozuwia maji yao yasichanganyike. Hivyo hii sio dalili ya wazi kuwa Qurani ni maneno ya Mwenyezi Mungu !.
                

Tafsili: Kiarabu   
              Kiingereza   Kifaransa     Kijerumani      Kispani      Kituruki       Kiurdu    Kifarsi     Kihausa

Bodi ya Kimataifa Ya Miujiza Ya Kisayansi Ya Qurani Na sunna   (1428-2007)