KUUMBWA MTOTO KATIKA MAUMBO TOFAUTI

KUUMBWA MTOTO KATIKA MAUMBO TOFAUTI

  

  

 Mwenyezi Mungu Amesema : “Mmekuwaje hamuweki Heshima ya Mwenyezi Mungu. Na hali ya kuwa Amekuumbeni namna baada ya namna?”. (Aya 13-14 Suratul Nuh).

UHAKIKA WA KISAYANSI :

          Mtu wa kwanza kumsoma mtoto wa kuku kwa kutumia lensi ndogo ni Harvey katika mwaka 1651. Pia alidurusu vijusi vya mbawala. Kutokana na ugumu wa kuainisha siku za kwanza za uja uzito  Mwenyezi Mungu Amesema : “Mmekuwaje hamuweki Heshima ya Mwenyezi Mungu. Na hali ya kuwa Amekuumbeni namna baada ya namna?”. (Aya 13-14 Suratul Nuh).

UHAKIKA WA KISAYANSI :

          Mtu wa kwanza kumsoma mtoto wa kuku kwa kutumia lensi ndogo ni Harvey katika mwaka 1651. Pia alidurusu vijusi vya mbawala. Kutokana na ugumu wa kuainisha siku za kwanza za uja uzito, akajua kuwa mtoto si chengine isipokuwa ni takataka za mfuko wa uzazi. Katika mwaka 1672, Graaf akagundua kokwa ndogo ndogo katika mayai ya uzazi ambazo hadi leo zinaitwa kwa jina lake “Graafian Follicles” na akakuta vijiwe vidogo katika tumbo la uzazi la sungura vyenye kufanana na kokwa ndogo ndogo. Akajua kuwa mtoto sio takataka za tumbo la uzazi lakini anatokana na mayai ya uzazi. Muundo huo wa ndani kabisa alioujua Graaf si chengine isipokuwa ni vitundu vidogo katika koja la seli za awali za mtoto (Blastocysts). Katika mwaka 1675,  Malpighi alikuta kijusi katika yai la kuku akadhani kuwa halihitaji vitu vya kurutubisha toka kwa jogoo. Akadhania kuwa ni lenye kiumbe kidogo chenye kukua na wala hakiumbiki katika maumbo tofauti. Kwa kutumia darubini iliyoendelea zaidi, Hamm na Leeuwenhoek, waligundua wadudu wa manii ya binaadamu  kwa mara ya kwanza katika historia mwaka 1677, lakini hawakuelewa ni ipi kazi yake hasa katika uzazi. Pia walidhani kuwa yana binaadamu mdogo anayekua katika tumbo la uzazi  bila ya maumbo maalum ya uumbaji. Katika mwaka 1759, Wolff alikisia kuwa ukuaji wa mtoto unatokana na koja la awali la uumbaji lisilo na umbo la kiumbe kilichokamilika. Katika mwaka 1775, ulimalizika mjadala kuhusu dhana ya uumbaji uliokamilika na ukafikiwa ukweli wa uumbaji katika maumbo. Majaribio ya Spallanzani kwa mbwa, yakathibitisha umuhimu wa wadudu wa manii katika zoezi la uumbaji. Kabla ya hapo, ilitanda fikra ya kuwa wadudu wa manii ni viumbe vya ajabu vinavyoishi kwa kutegemea viumbe vyengine, kwa hiyo wamepewa jina la wanyama wa manii (Semen Animals). Katika mwaka 1827, baada ya kupita miaka 150 ya ugunduzi wa wadudu wa manii,  Von Baer alikuta viyai vidogo katika vijiwe vya ovari ya mbwa mmoja. Katika mwaka  1839, Schleiden na Schwann walithibitisha kuwa uumbikaji wa mwili wa binadamu unatokana na sehemu hai muhimu za uumbaji na matokeo yake, na sehemu hizo zikaitwa Seli . Baadae ikawa ni wepesi kufahamu ukweli wa uumbikaji wa binadamu katika maumbo, kuanzia seli iliyorutubishwa inayotokana na muungano wa manii na ovari.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Aya tukufu inajuilisha kuwa binadamu haumbwi ghafla kwa mujibu wa dhana iliyokuwepo hadi karne kabla ya iliyopita, enzi za Aresto kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, bali anaumbwa katika maumbo yenye makadirio thabiti yanayomkusanya kila mtu licha ya kutofautina kwa makabila na kuambatana kwa vizazi.

         Historia ya sayansi ya kijusi, inashuhudia kugongana kwa wataalamu  katika namna ya uumbaji wa binaadamu wakati ambapo Qurani tukufu tokea karne ya kumi na saba, inatangaza kuwa binadamu hawi ghafla, bali anakuwa kupitia maumbo yaliyokisiwa kama ulivyo ujenzi wa jengo kwa mujibu wa muundo uliowekwa. Sudfa haitafsiri maumbo yaliyokisiwa, lakini inashuhudia hekima, kusudio na Uwezo wa Mwenyezi Mungu na elimu yake ya vinavyomzunguka na uzuri wa uumbaji Wake. Ama umoja wa maandalizi, mipango na uthabiti wa maumbo, licha ya wingi wa makabila na kuambatana kwa vizazi, basi tunahakikisha upweke wa Muumba Mtukufu.

     Fikra ya Aresto ya kuumbwa kijusi kutokana na damu ya hedhi, iliendelea kuwepo hadi karne ya kumi na saba ambapo aligundua darubini. Pamoja na hayo, wataalamu walidhani kuumbwa kwake ni kamili bila ya maumbo tofauti.