MAMWAIKIO YA MITO

MAMWAIKIO YA MITO

 

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye Anayeziunganisha bahari mbili; hii ni tamu, inayoondosha kiu,  na hii ni yenye chumvi kali; na Akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho (zisiharibiane ila pale kiasi cha kukutana tu). Aya ya 53 ya Suratul Furqan.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Kitabu cha kwanza kudhihiri kuhusu sayansi ya bahari katika karne ya kumi na nane, maelezo yake yalikuwa duni. Kisha sayansi ya bahari ikaanza kuchukua sehemu yake baina ya sayansi mpya wakati meli ya Challenger ya Uingereza ilipoanza safari yake ya kuizunguka dunia kuanzia mwaka 1872 hadi mwaka 1876. Kisha zikafuatia safari za kisayansi za ugunduzi wa bahari   Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Naye (Mwenyezi Mungu) ndiye Anayeziunganisha bahari mbili; hii ni tamu, inayoondosha kiu,  na hii ni yenye chumvi kali; na Akaweka kinga kati yao na kizuizi kizuiacho (zisiharibiane ila pale kiasi cha kukutana tu). Aya ya 53 ya Suratul Furqan.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

          Kitabu cha kwanza kudhihiri kuhusu sayansi ya bahari katika karne ya kumi na nane, maelezo yake yalikuwa duni. Kisha sayansi ya bahari ikaanza kuchukua sehemu yake baina ya sayansi mpya wakati meli ya Challenger ya Uingereza ilipoanza safari yake ya kuizunguka dunia kuanzia mwaka 1872 hadi mwaka 1876. Kisha zikafuatia safari za kisayansi za ugunduzi wa bahari. Mwishoni mwa karne ya ishirini, yakaanza kuzidi matumaini ya binadamu ya kuifahamu bahari kwa njia ya setalaiti na upigaji picha wa mbali. Baada ya uchunguzi wa maeneo mengi ya makutanio ya mito na bahari, watafiti wamegundua kuwa eneo la mamwaikio ni mazingira pekee katika sifa zake za kimaumbile na kibayolojia kulinganisha na mto na bahari licha ya kuingiliana kwa maji na mwendo wake baina yao kwa mujibu wa kupwa na kujaa kwa bahari na kufurika kwa mto na ukame wake. Na yalikuwa ni kizuizi chenye kutenganisha mazingira ya mamwaikio na mazingira ya  mto na mazingira ya bahari. Eneo hilo hubakia na sifa zake za pekee licha ya sababu za mchanganyiko kama vile kupwa na kujaa kwa bahari, na hali za mafuriko na kupungua, ambazo zinahesabiwa kuwa ni kati ya sababu zenye nguvu za mchanganyiko. Kwa kutenganisha mazingira matatu, na kwa kuvihesabu viumbe hai vinavyoishi katika mazingira hayo, eneo la mamwaikio linahesabiwa kuwa ni chumba cha viumbe hai vingi vinavyoishi ndani yake. Kwani viumbe hai hivi haviwezi kuishi isipokuwa katika eneo la mamwaikio lenye sifa za pekee. Wakati huo huo ni eneo lililohamwa na viumbe hai vingi vinavyoishi baharini na mitoni, kwani viumbe hai hivyo hufa iwapo vitaingia katika mazingira hayo kwa sababu ya tofauti ya sifa zake.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Mikusanyiko yote ya maji inaweza kuitwa bahari. Bahari tamu inayoondosha kiu au tamu mno, ni mto na bahari yenye chumvi kali au chumvi nyingi ni bahari au bahari ya chumvi. Na kwa hali hiyo, yamevuliwa maji ya mamwaikio kwani ni mchanganyiko baina ya chumvi na utamu, hayana sifa ya maji matamu yenye kuondosha kiu wala chumvi kali. Kwa wasfu huu, maji yako katika mafungu matatu: Maji ya mto, maji ya bahari, na baina yao maji ya eneo la mamwaikio lililoelezewa katika aya tukufu kuwa ni kinga au kizuizi chenye kuzuia kutamba kwa sifa ya chumvi ya bahari juu ya mto au utamu wa mto juu ya bahari. Mazingira ya mamwaikio ni chumba kwa wenye kuishi ndani yake kati ya viumbe hai, na kizuizi chenye kuzuia wenye kuishi nje yake katika mto au bahari. Hii maana yake ni kutofautika kwa mazingira matatu katika sifa za kimaumbile na katika viumbe hai.

         Maendeleo ya kihistoria katika mwendo wa sayansi ya bahari yanashuhudia kutokuwepo kwa maelezo ya uhakika kuhusu bahari kabla ya mwaka 1400. Pamoja na hayo, Qurani Tukufu imeeleza kwa hakika kabisa eneo la mamwaikio ya mito. Imebainisha kuwa ni mazingira ya pekee katika sifa zake za kimaumbile na za kibayolojia kulinganisha na mazingira ya  mto na mazingira ya bahari. Imeelezea kuwa licha ya kuingiliana kwa maji na mwendo wake wa kudumu kuelekea kwenye bahari, basi sifa hizo hubakia thabiti. Unatokea wapi ujuzi huo katika Qurani bila ya teknolojia na vyombo vya kisayansi, ikiwa si kutoka kwa ambaye elimu yake imekizunguka kila kitu?!