NYOTA ZINAZOREJEA NYUMA ZINAZOKWENDA NA KUJIFICHA

NYOTA ZINAZOREJEA NYUMA ZINAZOKWENDA NA KUJIFICHA

 

Mwenyezi Mungu Anasema, “ Basi Naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda, kisha zikajificha.” Aya za 15 na 16 za Suratul At Takwyr.

UKWELI WA KISAYANSI:

          Umri wa uzee katika maisha ya nyota kubwa ni kama tundu nyeusi (Black holes), kundi kubwa zaidi kuliko jua kwa mara tano zaidi. Tundu hizo nyeusi zinasifika kwa ukubwa wa eneo na mvuto mkubwa mno, kwani hakuna kitu kinachokwepa kabisa hata mwangaza wenyewe ambao kasi yake ni ( kiasi cha kilometa 300,000 kwa sekunde). Toka hapa basi limekuja jina lake lenye kuonyesha kuwepo kwa maeneo kama tundu katika ukurasa wa mbingu uliopotea kila kitu na kuwa tundu nyingi.  Mwenyezi Mungu Anasema, “ Basi Naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda, kisha zikajificha.” Aya za 15 na 16 za Suratul At Takwyr.

UKWELI WA KISAYANSI:

          Umri wa uzee katika maisha ya nyota kubwa ni kama tundu nyeusi (Black holes), kundi kubwa zaidi kuliko jua kwa mara tano zaidi. Tundu hizo nyeusi zinasifika kwa ukubwa wa eneo na mvuto mkubwa mno, kwani hakuna kitu kinachokwepa kabisa hata mwangaza wenyewe ambao kasi yake ni ( kiasi cha kilometa 300,000 kwa sekunde). Toka hapa basi limekuja jina lake lenye kuonyesha kuwepo kwa maeneo kama tundu katika ukurasa wa mbingu uliopotea kila kitu na kuwa tundu nyingi. Nyota hizi kubwa zenye kupotea au kuonekana, hufagia kila kitu kinachozikaribia. Kwa hiyo, yametambulishwa hayo na hesabu zilizoitwa fagio kubwa (Giant vacuum – Cleaners), nadharia iliyowekwa na Karl Schwars Child mwaka 1916. Tokea mwaka 1971, Robert Oppenheimer amezidisha uwezekano wa kuwepo kwake kwa kuthibisha. Wataalamu wana imani kwamba kundi letu la nyota kwa mfano ni kama tundu nyeusi.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Kiapo kimekanusha katika mtindo wa Qurani Tukufu kwa ajili ya  kuthibitisha kama kwamba Mwenyezi Mungu Anasema kuwa hauna haja ya kiapo kwa hoja hizo zilizo bayana. Kiapo kimetajwa katika kuonyesha dalili ya kuwa Qurani Tukufu ni Wahyi wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Basi naapa kwa nyota zinazorejea nyuma. Zinazokwenda kisha zikajificha. Na kwa usiku uingiapo. Na kwa asubuhi inapopambazuka. Kwa hakika hii (Qurani) ni kauli (aliyokuja nayo) Mjumbe mtukufu (Jibrili).” Aya za 15 – 19 za Suratul At Takwyr. Ni zenye kuonyesha utukufu wa kiapo na umuhimu wake katika kujulisha chenye kuapiwa. Na hapa kimetajwa kwa sifa ambazo zinakutana sawasawa na sifa za kinachoitwa tundu nyeusi. Katika asili yake, ni nyota zinazokwenda katika mizunguko yake. Kwa hakika ni nyota kubwa ambazo mwisho wa umri wake zimeporomoka, ikanywea mada yake, zikajificha na hazidhihirishi mwangaza wowote. Sababu ya hayo, ni ukubwa wa mvuto wake ambao unazifanya zifagie kila kitu kilicho pembeni yake katika njia yake na kukimeza kwa hiyo huzidi ukubwa wake na nguvu yake. Hapa unadhihiri wasfu wake wa (zinazokwenda kisha zikajificha) au mafagio makubwa. Ujuzi wa sifa hizo ni mpya kwa hiyo kutajwa kwake katika Qurani kwa maneno yenye kuzijulisha kwa kina, ni katika kuthibitisha wahyi wake wa dalili tosha kuwa ni maneno ya Mwenyezi Mungu Muumba.