UTOSI

UTOSI

 

 

 Mwenyezi Mungu Amesema : “Sivyo hivyo! Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi.  Utosi muongo, wenye madhambi.”  ( Aya za 15-16 Suratul Alaq ).

UKWELI WA KISAYANSI :

       Ubongo wa binadamu una vigawanyo vinne vikuu ambavyo ni :  “Frontal Lobe”, “Occipital Lobe”,  “Temporal Lobe”  Mwenyezi Mungu Amesema : “Sivyo hivyo! Kama haachi, Tutamkokota kwa nywele za utosi.  Utosi muongo, wenye madhambi.”  ( Aya za 15-16 Suratul Alaq ).

UKWELI WA KISAYANSI :

       Ubongo wa binadamu una vigawanyo vinne vikuu ambavyo ni :  “Frontal Lobe”, “Occipital Lobe”,  “Temporal Lobe”, na “Parietal Lobe”. Kila sehemu ina kazi yake peke yake inayotofautiana na nyengine. Wakati huo huo, sehemu zote hizo ni zenye kukamilishana. Sehemu ya mbele ndio yenye kusifika na nyenzake katika wanyama, kwani ndio sehemu zinazohusika na tabia, maneno yaliyoendelea na ndio iliyowazi kwa upande wa uchunguzi na kikazi. Ni sehemu yenye vituo kadhaa vya akili ambavyo vinatofautiana  kwa upande wa eneo na kazi. Na utandu wa mbele wa utosi (Pre-Frontal Cortex), uko moja kwa moja nyuma ya paji la uso, nao ndio sehemu kubwa ya sehemu ya mbele ya ubongo na kazi yake inashikamana na kujenga haiba ya mtu . Pia ina athari kubwa katika kuainisha hatua (Initiative) na hukumu (Judgment). Kisha sehemu ya kuendeshea maneno ya broka ( Motor Speech Area of Broca) yenye kuratibu harakati baina ya viungo vinavyoshiriki katika zoeza la usemaji mfano wa koo, ulimi na uso. Kisha maeneo ya harakati yanayokusanya sehemu ya mbele ya jicho (Frontal Eye Field) ambayo hutoa msukumo unaoambatana na macho kuelekea kwenye upande unaokabiliana nao na sehemu ya kuendeshea viungo vikuu na visaidizi (Primary & Secondary Motor Areas). Sehemu zote hizo mbili ni zenye kuhusika na uendeshaji wa matakwa ya viungo. Kama hivi imethibika kuwa mwanzo wa sehemu ya mbele ya utosi  iliyoko katika kina cha utosi, ndio yenye kuelekeza tabia na yenye kuainisha haiba. Kujeruhiwa kwake, kunaweza kusababisha mporomoko wa vigezo vya tabia, kiwango cha kumbukumbu na uwezo wa kutatua matatizo ya akili.

UPANDE WA MIUJIZA:

         Tatizo halikupata ufumbuzi au kudhihirika namna yake isipokuwa hivi karibuni katika zama za sayansi . Quran Tukufu imeikusudia sehemu ya utosi  au sehemu ya mbele ya kichwa bila ya sehemu nyengine yoyote ya viungo kuhusika na uongo, na kosa na uhalifu wake wa maneno machafu, nako ni kukikamata kitu na kukivuta kwa nguvu ikiwa ni taswira ya kukihukumu kiungo kinachohusika na tabia katika binadamu. Ukweli huu wa kuhusishwa sehemu ya mbele pekee  kabla ya ugunduzi wa kazi yake ya kuelekeza tabia na kupambanua haiba ya mtu hakufasiriwi na sudfa wakati wa kuachishwa ziwa la mama.

         Kwa hekima ya sheria ya Mwenyezi Mungu, umekuwepo utosi huu  na pengine kuna uhusiano baina ya utosi wenye kusujudu kwa woga na tabia iliyonyooka (Bila shaka sala ni yenye kuzuia mambo machafu na maovu.  Na kwa yakini, kumbusho la Mwenyezi Mungu  ni jambo kubwa kabisa, na Mwenyezi Mungu Anayajua mnayoyatenda.)

 Undani wa utosi na kazi ya sehemu ya mbele ya ubongo,  ni durusu ya miujiza ya Suratul alaq.