Je, IMANI YA UTATU Ni ya Ufunuo Mtakatifu?

Je, IMANI YA UTATU Ni ya Ufunuo Mtakatifu?.


Je, IMANI YA UTATU
Ni ya Ufunuo Mtakatifu?

 

By :  M. A. C. Cave

 

 

Kimetafsiriwa na Omari Juma Mangilile
Email: [email protected]
Na kupitiwa na Said Rashid Juma

 

 

 

 
 
Muhtasari kutoka kwa Mtunzi

(1) Dondoo za Biblia zimenukuliwa kutoka toleo la Revised Standard Version (RSV) zilizonukuliwa kutoka katika lugha asilia na kuunda toleo la kwanza la (King James Version) 1611 A.D. lililosahihishwa 1881-1885  A.D. na  1901, kisha likasahihishwa tena 1946-1952, pia toleo la pili la Agano Jipya 1971 A.D. lililochapishwa na Wm. Collins Sons & Co., Ltd. for Canadian Bible Society. 1835 Yonge St. Toronto 7, Ontario, Canada. Machapisho mengine yameonyeshwa kwa kiasi cha kutosha.

(2) Dondoo za Qurani  zimenukuliwa kutoka "http://sw.quran.u/", (Tafsiri ya Kiswahili ya maana na mafafanuzi ya Qur`an Tukufu).

(3) (SAW) ni kifupi cha "Rehema na amani ziwe juu yake" ambacho kimekuwa salamu ya kawaida inayotumika kwa Mitume yote ya Allah. Kwa hiyo, kinatumika kama salamu ya heshima kwa kila Mtume pale linapotajwa jina lake, sawa sawa na (As) yenye maana ya "Amani iwe juu yao" itumikayo pale majina mawili au zaidi ya mitume, yanapotajwa.
 
 
WAKFU
Nautoa wakfu utafiti huu wa kinyenyekevu, kwa Mungu, kwa kutupatia mawazo ya busara, mimi na mke wangu, Nenet ambaye ni msaidizi mwema kwangu, mwenye moyo wa kuridhia, mama mlezi wa watoto wetu. Yeye ni mwanamke mwema na mchamungu. Na kwa watoto wangu wote, kwa shauku yao ya kuniunga mkono, pia kwa jamaa, ndugu na marafiki zangu, kwa uaminifu wao, na kwa kuwakumbuka wazazi wangu waliotaabika sana nilipokuwa mnyonge wa wanyonge, wamenionyesha upendo na uvumilivu wao.

Hatimaye nautoa wakfu utafiti huu kwa marafiki zangu wote wa moyo ninaowafahamu, kwa maneno yao mazuri ya kunihamasisha pia na kwa msimamo wao wa kuunga mkono kuchapishwa kwa kitabu hiki.

M. A. C. Cave
15 August 1996
 
SHUKRANI

Kwa unyenyekevu wote namshukuru Mungu kwa baraka zake za kunipa nafasi ya kutoa kitabu hiki, kwa hiyo kulifanya lengo langu nililolitumainia kutimia.

Namshukuru anayepaswa kushukuriwa; Dr. Maneh Al-Johani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Kiislamu Duniani (WAMY) kwa kuuchapisha utafiti huu.

Shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioniunga mkono na kunisaidia katika kazi hii, kwa misaada ya kiufundi, kwa moyo wao wote. Shukrani zangu za dhati kwa wale wote waliofanyakazi nami kwa juhudi na uaminifu katika kukitoa kitabu hiki.

Namuomba Allah Mwenye nguvu, kwa Rehema zake zisizo na kikomo, awabariki wote hao. Aamiin.

M. A. C. cave
 
 
Katika Injili ya (Yohana 8:40), Yesu (As) anasema:

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu
ambaye nimewaambia iliyo kweli,
niliyoisikia kwa Mungu..."

Allah (Mwenyezi Mungu) anasema katika Quran (3:59):

Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama
mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo
kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.

Ukweli wa upweke wa Mwenyezi Mungu, maumbile na nafasi ya Yesu (As), kwa mujibu wa Maandiko:

Kuiacha dhana ya Mungu mwenye mwili na Utatu hakumwaibishi
Yesu, ispokuwa kunamuweka Mungu katika utukufu, upweke,
 ukuu na nafasi ya pekee isiyo na mfano ya kuwa yeye
ni Mungu wa pekee anayestahiki kuabudiwa.

Yesu Kristo si Mungu, ila ni Mtume na Mjumbe
`mkuu wa Mungu!
 
 
YALIYOMO
Somo                                           ukurasa
DIBAJI    1
UTANGULIZI    2
Habari Maalum Kutoka Uingereza.    5
WAKRISTO    7
IMANI YA UTATU    10
JINSI UTATU ULIVYOKUA KATIKA ITIKADI YA KIKRISTO    12
Imani ya Nicaea    13
Imani ya Nicene    14
SABABU ZILIZOSHAWISHI IMANI YA UTATU    17
KUHALALISHWA KWA UTATU NA WANAUTATU    19
IMANI YA UTATU HAIKUFUNDISHWA NA WAKRISTO WA MWANZO    20
JE, BIBLIA INAFUNDISHA IMANI YA UTATU?    22
Kuhusiana na Maandiko ya Kiyahudi    23
Kuhusiana na Maandiko ya Kigiriki    23
KUPINGWA IMANI YA UTATU NA WAKRISTO WA KISASA.    25
MAFUNDISHO YA MITUME YA MUNGU    27
BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU MUNGU NA YESU (AS)    32
1. Ushuhuda wa Biblia kuhusu Mungu    32
2. Ushuhuda wa Biblia kuhusu Yesu (AS)    34
3. Kile anachokisema Yesu (AS) juu yake na Mungu    37
KINACHOSEMWA NA QURAN TUKUFU KUHUSU MUNGU    40
UTHIBITISHO WA BIBLIA JUU YA IMANI YA UTATU    43
HOJA ZA NYONGEZA ZINAZOKANUSHA IMANI YA UTATU    51
JE, YESU (AS) ANATHIBITISHA UFAHAMU WA ROHO MTAKATIFU?    55
QURAN NI NINI? NA INASEMA NINI KUHUSU YESU (AS) NA MAMA YAKE?    60
KISA CHA AJABU    64
ONYO KWA WALE WANAOPOTOSHA UJUMBE WA MUNGU    66
 
 
DIBAJI

Chapisho hili, "Je, IMANI YA UTATU ni ya Ufunuo Mtakatifu?", litatumika kama chakula cha fikra kwa kila mwenye mawazo mazuri na kwa wafuasi wa Ukristo wa Kisasa. Maana ya Utatu imekanganya kila dhehebu la Kikristo. Ingawa  Bw. M. A. C. Cave alikuwa Mkristo anayeamini utatu hapo kabla, alipoanza kuutazama utafiti wake juu ya asili ya Imani hii, kwa mshangao mkubwa kabisa aligundua kuwa, Imani hiyo ilitungwa na kuendelezwa katika zama za mwishoni pia imepangwa na kuanzishwa na waandishi na watambuzi (Thinkers) mbali mbali wa Kikristo.

Bw. M. A. C. Cave anakusanya ushahidi wa kuonyesha kuwa Utatu si lolote ila ni imani iliyotungwa na wanadamu, ambayo inashindwa kufikia kuwa ni ya ufunuo kutoka kwa Mungu. Kisha, imani hii iliyoundwa na fundi cherehani, imepoteza nguzo yake muhimu, na hilo lipo katika kupingana kwake yenyewe kwa yenyewe na imethibitisha kuwa ni mwiba mchungu kwa upande wa tabaka za Wakristo kiujumla na hasa hasa kwa viongozi wakuu wanaojaribu kuipigia upatu imani hiyo.

Ni jambo lisilokubalika kwa mtu anayefikiria sawa sawa kuamini itikadi hii licha ya dosari zake zote. Mtu mwenye akili, anapaswa awe mmakinifu zaidi juu ya mambo ya mwelekeo wa kiroho na ambayo ni muhimu sana maishani mwake. Anatakiwa ajaribu kuchungulia katika maandiko ya dini nyingine ili kuondoa mashaka. Na hatakiwi ajiachie awe muhanga wa kuridhika na imani pofu kama ilivyokuwa zamani. Jaribu kutafakari juu ya aya za Maandiko Matakatifu:

Nakusihi msomaji, kipime kitabu hiki kwa akili isiyopendelea na moyo mkunjufu kiukweli, kwa kuwa hii ndio njia ya pekee inayoweza kuongoza katika uamuzi sahihi utakaojenga maisha ya mtu hapa duniani na maisha yajayo.
 
UTANGULIZI

Hakuna kinachowaudhi sana Wakristo kama kuitilia shaka imani ya Utatu, chemchemi ya imani yao. Kwa kukulia katika Ukristo, ninajua kwa hakika kuwa hilo litamuumiza mchamungu wa Kikristo, kwani ni kitu anachokijua kuwa ni cha ukweli. Lakini kuazima jicho pofu, (kujifanya sioni au sijui) wakati najua vizuri huko ni kuwa mbali kabisa na wema, kwani nimelazimishwa na amri za Mungu niwaongoze wale waliopotoshwa na imani ya uongo. Ni haki ya msingi kwa kila mtu kuujua ukweli utakaomwongoza katika njia ya haki.

Ni ukweli madhubuti kuwa, binadamu ndiye aliyebuni kuwepo kwa mantiki (kutumia akili), kwa kuwa, anamiliki uwezo wa kiakili. Akiwa na hilo, binadamu siku zote anaelekea katika kuutafuta ukweli. Kwa hiyo, kila mmoja, anatarajiwa afikiri kwa mantiki juu ya vitu bila ya upendeleo, katika maneno na matendo yake yote ili afikie lengo lake. Zaidi, amepewa sifa ya uhuru wa kuchagua ili kumwezesha kukaa sawa katika jamii iliyostaarabika. Ni ukweli madhubuti kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kumlazimisha mtu mwingine akubali hata kama ni haki. Hata hivyo, hiyo ni aina ya ufedhuli na ukaidi  kwa akili kukataa ukweli. Watu wenye maadili na msimamo sio tu wanatetea ukweli, hata kama mchungu, lakini pia wapo tayari kuutetea ukweli huo kwa hali yoyote ile hadi kufikia upeo wa kutoa muhanga maisha yao.

Utatu umeota mizizi sana miongoni mwa Wakristo kiasi ambacho ni mara chache mno mtu kuzingatia mahusiano tata ya 'Mungu mmoja katika utatu'. Ingawa asili ya imani hiyo inatokana na imani za kipagani, Wakristo wengi hawahoji ukweli wa imani kama hizo na hawako macho kuwa imani hiyo imetungwa na mwanadamu na si maneno ya Mungu. Imani ya Utatu inatangaza:

"Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu na kwa pamoja, si kwa kujitenga, wanaunda Mungu mmoja. Utatu ni umoja wa milele, hauna mwanzo wala mwisho, na wote ni sawa."

Yesu (As), anazingatiwa na waumini wa Utatu kuwa ana hali mbili ubinadamu na uungu. Anaaminiwa kuwa ni Mwana wa Mungu na ni Mungu Kamili kwa kuwa ni wa pili katika Uungu wa imani ya Utatu.

Hata hivyo, katika kitabu hiki, wasomaji watagundua kuwa ukweli fulani umepotoshwa kwa uangalifu mkubwa na wachambuzi, weledi, wanatiolojia, waandishi, wainjilisti na makanisa  ya Kikristo ili kuchangia hoja yao ya imani ya Utatu kuwa ni ya "ufunuo mtakatifu". Hapo kabla, Nabii Yeremia (As) aliwaonya watu juu ya ufisadi uliofanywa katika ufunuo na wale wanaofundisha dini ya Mungu. Anasema:

 "Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo." Yeremia 8:8

Kwa kile kinachofungamana na ibada za uongo, Nabii Yesu (As) amerudia kutumia onyo lilotolowe na Nabii Isaya (As), lakini watu kwa hakika hawasikii. Anasema:

"Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu." Mathayo 15:8-9  

Uwamuzi wangu wa kutumbukia katika jambo hili la hatari umetokana na utafiti wangu juu ya ukweli wa maana ya Utatu. Utafiti huo sio tu upo ndani ya mipaka ya Vitabu vitakatifu, lakini pia katika maandiko na makala za wanazuoni wa kidini. Baadhi ya kazi zao zimethibitisha mihemuko na kupokewa vizuri na madhehebu ya Kikristo.

Utafiti huu umefanywa kukiwa na mtazamo wa kukubali matokeo kwa moyo mkunjufu kwa imani yangu ya zamani ya kuamini Utatu. Kwa kweli, Wazo hili limechimbuka ili kutafuta ushahidi wa wazi wa kuthibitisha uhalisi wa imani hiyo, na si njia ya kubabaisha, huku nikiamini kuwa imani hiyo ina uhalisi kutoka kwa Mungu. Na zaidi, ili nisiwe napendelea nimetumia marejeo ninayoyategemea kwa mikono yangu.

Kwa hakika, ni utafiti wa juhudi za dhati kwa upande wangu ili nipime ushahidi  kama ulivyorundikana. Kwa bahati mbaya, wakati utafiti ulipokuwa unaendelea, imani ya Utatu iliyopitia vizazi vingi ikiwa ni ukweli wa mwisho, imepata ugonjwa. Kama matokeo ya utafiti yangekuwa kama ilivyotarajiwa, yangeangaza moyo wangu. Hata hivyo, kwa fadhaa, nimeigundua kuwa ni kosa. Imani hii iliyoundwa na mwanadamu ilibuniwa na watu ili inufaishe tamaa zao na kuwapatia maslahi. Kwa hiyo, hoja zote za zamani zimebadilika na kuwa uongo wa wazi. Imani ya Utatu sio tu ni kinyume na mafundisho ya mitume ya Mungu lakini pia ni matusi kwa akili za binadamu kwa kuwa inapingana na akili na haipatikani sehemu yoyote katika Biblia.
Hatimaye, ukweli mchungu ni kuwa, utafiti huu unabomoa Utatu na imani za kuwa na mwili wa kibinadamu, pamoja na imani zote zinazofungamana na hilo. Kumwabudu Mungu kwa mujibu wa mwongozo wake alioufunua ni kuzitupilia mbali imani hizo kinaganaga.

Kuwacha dhana ya Mungu mwenye mwili na Utatu hakumwaibishi Yesu bali kunamuweka Mungu katika utukufu, upweke, ukuu na nafasi ya pekee isiyo na mfano ya kuwa yeye ni Mungu wa pekee anayestahiki kuabudiwa. Yesu Kristo si Mungu lakini ni Mtume na Mjumbe mkuu wa Mungu!

Namkaribisha 'kila mtu' atafute ukweli katika kazi yangu ambayo itafungua mioyo ya wale wanaongoja uwokovu.

"Ee! Mungu wetu! Kwa kupitia kipande cha kazi hii tumepania kufikisha maana sahihi ya Ujumbe wako kwa wanadamu. Ee! Mola wetu onyesha baraka zako na uwaongoze kwenye ukweli. Popote tulipokosea, tafadhali tusamehe na wakinge wanadamu dhidi ya dosari zetu." Amiina – (tukubalie maombi yetu).
 
Habari Maalum Kutoka Uingereza.
   
UCHUNGUZI WA KUSHTUSHA WA MAASKOFU WA KIANGLIKANA

Mawimbi ya kushtusha yalibiringika Uingereza nzima na kwa ulimwengu wa Kikristo pale habari za DAILY NEWS la Uingereza zenye kichwa: “Uchunguzi wa kushtusha wa Maaskofu wa Kianglikana,” zilipoeleza kuwa zaidi ya nusu ya Maaskofu wa Kianglikana wanakubali kuwa: “Wakristo hawalazimishwi  kuamini kuwa Yesu Kristo ni Mungu”.  Kura ya maoni iliyopigwa na Maaskofu wa  Uingereza, Maaskofu 31 Miongoni mwa Maaskofu 39, Wamekana UUNGU wa Yesu pia KUFUFUKA KWAKE hilo linaonyesha kuwa imani mbili katika imani kuu za Kikristo zimebatilishwa kikamilifu.

Wao wanaona kuwa ufahamu huu wa zamani si sahihi katika Biblia.
 
SI MUNGU – ISPOKUWA NI “MJUMBE MKUU WA MUNGU”

Habari hizo zinaendelea kueleza kuwa, 19 miongoni mwa hao Maaskofu 31 wanakubali kuwa: “Ni jambo la kuridhisha kumchukulia Yesu kuwa ni mjumbe mkuu wa Mungu”.

KWA HIYO, ZAIDI YA NUSU YA MAASKOFU WA KIANGLIKANA WA UINGEREZA WANAJITAKASA NA DHAMBI YA KUMKASHIFU MUNGU NA WANAMZINGATIA  YESU KUWA NI MJUMBE TU.

ASKOFU JENKINS ANAKOSOA VIKALI  ITIKADI MUHIMU YA KIKRISTO

Katika mahojiano na kituo cha Runinga cha London`s Weekend katika kipindi cha dini “CREDO”, - Askofu mteule mpya wa Durban – Rev. Profesa David Jenkins, mwenye cheo cha nafasi ya nne katika Kanisa la Uingereza – ameelekeza mashambulizi yake kwa msingi usio wa hakika unaosimamia jengo zima la imani ya Kikristo. Imani muhimu sana ya Kikristo ya UUNGU wa Yesu na KUFUFUKA Kwake zimekosolewa vikali mno na Askofu huyo, akieleza kuwa, matukio ya wakati wa kazi za mwanzoni za Yesu: “Kwa hakika hayakuwa sahihi kabisa ispokuwa yameongezwa katika habari za Yesu na Wakristo wa mwanzo ili kuelezea Imani yao Kwake kama ni Masihi”.

Katika ufahamu huu juu ya Mungu na Yesu (AS) wanashirikiana wanafunzi wote, Wakristo wa mwanzo, wahenga, Wasomi wa Kikristo wa siku hizi, watambuzi, waandishi na hata Wakristo wa kawaida. Yesu (AS) anasema katika (Mathayo 4:10):

"...kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."

Katika (Yohana 17:3) anasema: "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."

Vilevile anasema katika Yohana 20:17: "...ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu."

Je, maelezo haya hayapo wazi? Wapi alipokubaliwa Yesu kuwa ni Mungu?

Sasa, hapa linakuja, swali la dola Bilioni moja: “Je, IMANI YA UTATU ni ya Ufunuo Mtakatifu?”
 
WAKRISTO

Karibu watu bilioni moja duniani wanaendelea kuamini na kutekeleza imani ya Utatu huku mara mbili ya hao, kama si zaidi, wanaikataa kinagabaga kuwa haipo katika wigo wa kibiblia pia wanaona ni upotoshaji, haina msingi, haingii akilini, inachukiza na ni kinyume na akili.

Kwa mujibu wa Bamber Gascoigne, katika kitabu chake “Wakristo”: Kwa  miaka hamsini ya mwanzo ya kile tunachokiita hivi sasa zama za Ukristo, hakuna hata neno moja lililosalimika katika nyaraka yoyote ile juu ya Kristo na wafuasi wake. Katika kipindi cha miaka hamsini iliyofuatia, Wakristo wenyewe waliandika vitabu vingi ambavyo kwa sasa vinaunda Agano Jipya. Lakini bado hakuna neno hata moja, pamoja na kuyatoa kidogo, lililotoka nje ya mwandishi. Na baadaye, katika karne ya pili, mamlaka ya Roma ilianza kueleza:

“Kuna kundi, lililochukiwa, kwa sababu ya chuki zao, lililoitwa Wakristo na watu wengine. Christus, amboa kutokana na wao ndio limepatikana jina Ukristo, waliteseka kwa adhabu kali mno katika kipindi cha utawala wa Tiberius mikononi mwa mmoja wa maofisa wetu, Pontius Pilate.” (Tacitus).

“Wakristo ni kundi la watu walioleta ushirikina na uovu mpya.”  (Seutonius).

“Maskini, mafukara waliojikinaisha kuwa hawafi na wataishi milele, kwa kuabudu ghiliba aliyesulubiwa na kwa kuishi chini ya sheria zake. Kwa hiyo, wao wanadharau vitu vya dunia hii, na kuvichukulia kuwa ni mali ya uma. Wao wamepokea imani hii toka katika tamaduni bila kuwa na ushahidi unaotambulika. Kwa hiyo, kama tapeli au laghai yoyote atatokea miongoni mwao, basi kwa haraka haraka atapata utajiri kwa kuwaamuru watu hawa duni.” (Lucian)

Bila kujali, Ukristo umeshastawi na kuwa moja ya dini kuu, lakini mafundisho ya Ukristo wa kisasa kama tunavyoujua leo hii, yapo tofauti na kile kilichofundishwa na Yesu (AS) kwa wanafunzi wake. Imani tofauti za Ukristo kama vile Utatu iliendelezwa baadae. Motisha wake ulianza katika kipindi cha utawala wa Mfalme Mkuu Constantine huko (Nicasea) na baadaye uliendelezwa katika imani kamili ya kuamini bila kuhoji (dogma) wakati wa utawala wa Mfalme Theodosius mwaka 381 C.E. Ajabu ilioje! Kuanzia hapo, Ukristo una madhehebu mengi tofauti tofauti na ni vigumu kwa sasa kutambua imani sahihi ya Kikristo. Vyovyote ulivyo, katika muktadha wa sasa, hakuna aliye karibu zaidi na mafundisho asilia ya mitume. Wao wanaegemeza mafundisho yao juu ya Biblia ambayo yenyewe ni mada inayoendelea kurekebishwa.

Mungu pekee ndiye ajuaye ni lini Wakristo wataweza kutoa nakala sahihi (asilia) ya kitabu chao (Biblia).

Mtu atashangaa, juu ya idadi ya matoleo ya Biblia yaliyopo leo hii. Kila moja linatofautiana na jingine, ndio, kila moja linadai kuwa yeye ndio toleo asilia. Matolea yote hayo yameshawahi kutangaza duniani kuwa, yenyewe ni ufunuo mtakatifu. Rejeo lao lililo tayari lipo katika (2 Timotheo 3:16), isemayo “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho...”  Lakini kile wasichokifahamu Wakristo ni kuwa, “Kwa hakika, yaliyomo katika Biblia zao si Maandiko matakatifu ispokuwa ni hekaya, fikra, matukio na tamaduni tu.” Tatizo hilo linachanganya zaidi pale tunapojua kuwa baadhi ya matoleo ya Biblia yana vitabu vingi zaidi kuliko mengine. Toleo la Orthodox (OVC), lina vitabu 86; Toleo la Charismatic (CV), lina vitabu 76; Toleo la Roman Catholic (RCV), lina vitabu 73; na matoleo yote ya Kiprotestanti yana vitabu 66 likiwemo The New World Translation of the Holy Scripture [1984] (NW), linalotumiwa na Mashahidi wa Yehova na matoleo mengine kama vile the King James [1611-1942] (KJ), American Standard [1901-1944] (AS), Rivised Standard [1971] Second Edition (RS) Jerusalem Bible [1966] (JB), Good News Bible (1954: iliyochapwa 1956), Ronald A, Knox (Kx), New International Version (NIV), na motoleo mengine yasiyo na idadi.

Zaidi ya hayo, vipi kuhusu hoja ya Warejeaji wanosifika wa Biblia ya the Rivised Standard Version (RS), Rivised Edition ya 1952, na kwa Agano Jipya, Second Edition ya 1971, by Wm. Collins Sons & Co. Ltd. Iliyochapwa na Canadian Bible Society, isemayo katika Utangulizi wake: (1) “Naam, Toleo la King James lina dosari kubwa mno.... dosari hizo ni nyingi sana na hatari sana kiasi cha kupelekea kuitishwa wito wa kurekebishwa kwa tafsiri yake ya Kingereza.” (2) “Toleo la King James la Agano Jipya liliegemea katika mandiko ya Kigiriki yaliyoharibiwa kimakosa” Vipi kuhusu hoja ya Mashahidi wa Yehova katika chapa ya Mwamko ya Septemba 1951 inayoeleza; “Biblia ina makosa 50,000!”

Na vipi kama nikisema, kinyume na imani yetu, kuwa “Katika Waandishi wanne wa Injili Hakuna hata mmoja aliyekuwa Mwanafunzi wa Yesu  (AS).” Katika (Luka 6:14-16 na Marko 3:17) tunaona yametajwa majina ya wanafunzi kumi na wawili na Yesu (AS). Huku majina Mathayo na Yohana yamo, na majina Marko, Luka na Paulo hayajatwaja.

Hata hivyo, kutokana na nkuu zifuatazo, utagundua kuwa hizo Injili mbili zinatajwa kuwa ni za Mathayo na Yohana kwa kuwaheshimu tu, kwani ziliandikwa na mtu wa tatu. Soma nakala halisi ya mstari wa (Mathayo 9:9):

 "Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani aitwaye Mathayo, akamwambia nifuate. Akaondoka akamfuata."

Na katika (Yohana 21:24):

"Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli?"

Katika aya ya kwanza, mwandishi anasimulia tu kile kilichotokea kati ya Yesu (AS) na Mathayo, huku katika aya ya pili, ni wazi kuwa kiwakilishi “nasi” kinawakilisha mwandishi.

Hebu kwa sasa tutafakari juu ya kile kilichosemwa na waandishi wawili wa Kikristo kuhusu kuundwa kwa Biblia:

“Wakati mwingine, Wanukuzi wanatia kile kisichokuwemo katika maandishi, pia kile wanachokifikiria kitakuwemo. Mnukuzi anaweza kuamini kumbukumbu zinazobadilika, au anaweza kuunda maandiko kwa mujibu wa mtazamo wa madhehebu anayoyafuata. Kwa kuongezea katika matoleo na manukuzi ya Mapadri wa Kikristo, takriban (Miswada) ya Mandiko Matakatifu elfu nne ya Wagiriki [MSS], ilijulikana kuwa ipo. Kwa hiyo, tofauti za usomaji ni jambo la kuzingatiwa.”

Kwa hiyo Injili ziliundwa, na ambazo kiwaziwazi, ziliakisi mitazamo ya ufahamu wa mahitajio na matumizi ya jamii za waandishi. Kwao wao, vitu vya kimila vilitumika, lakini kulikuwa hakuna kusita katika kukibadilisha kile kisichoendana na lengo la mwandishi.”
 
IMANI YA UTATU

Imani ya Utatu inazingatiwa kuwa ni ya Mungu mmoja katika nafsi tatu. Kila moja katika nafsi hizo inasemakana kuwa ipo milele bila ya kuwa na mwanzo. Kila moja inasemekana ni Yenye uwezo, si kuu wala si ndogo zaidi ya zingine; Kila moja inasemakana kuwa ni Mungu kamili kwa maana ya neno Mungu ambalo linajumuisha sifa za Mungu, zote ni sawa sawa kwa wakati mmoja, kwa eneo, nguvu na elimu. Imani hii inaunda kiini na nguzo ya imani ya Ukristo iliyotetewa na takriban na madhehebu yote ya Kikristo. Hata hivyo, imani ya Utatu si ya ufunuo mtakatifu, bali ni imani ya kuamini bila kuhoji kwa binadamu iliyoundwa na Wakristo wakati wa kipindi cha robo ya kwanza ya karne ya nne. Kwa hakika, hilo lilikuwa ndio zao la Baraza la Constantinople mwaka 381 C.E. ambalo lilikubali kumweka Roho Mtakatifu katika nafasi sawa na Mungu na vilevile Yesu Kristo.

Insaiklopidia Britannica inaeleza kuwa: ufahamu wa umoja wa kiasili (homoousia) ya msemo mtakatifu na Mungu Baba zinathibitisha uungu kamilifu wa Yesu Kristo. Fumbo la ubinadamu wa Yesu Kristo linaweza kueleweshwa katika njia hii: hali (natures) mbili kwa mtu mmoja....kimsingi halijaanzishwa na mafundisho ya kufikirika, kwa kiasi fulani linabadilika ndani ya liturujia (usharika mtakatifu) katika kila mfumo mpya na katika nyimbo za kidini zisizohesabika – kama ilivyo katika maneno ya liturujia ya Easter:

“Mfalme wa mbinguni amedhihiri duniani ili kumfanyia wema binadamu pia alishirikiana na wanadamu. Kwani alitwaa mwili wake kutoka kwa bikira na kutokana na bikira huyo amekuja, kwa kuwa amelikubali hilo. Huyo ni Mwana, mwenye asili mbili, lakini si kwa haiba. Kwa hiyo, katika kumtangaza Yeye, kwa hakika ni Mungu kamili na ni mtu kamili, tunakiri Kristo ni Mungu wetu.”  

Imani ya Athanasian inaeleza:

“Kuna nafsi moja ya Baba, nyingine ya Mwana, na nyingine ya Roho Mtakatifu. Lakini Uungu wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote ni mmoja; Utukufu ni sawa sawa, uwezo wa milele... Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu. Naam, hakuna Miungu mitatu bali ni Mungu Mmoja... Kama vile tunavyoshurutishwa na sheria za Kikristo kukiri kuwa kila nafsi katika hizo yeye yenyewe ni Mungu na ni Bwana, kwa hiyo, tumekatazwa na dini ya Ukatoliki kusema kuwa kuna Miungu mitatu. Au Mabwana watatu.”  

Ufafanuzi wa Kiothodox juu ya Utatu wa Kikrisro na Imani ya Athanasian: “Imani ya Utatu inaeleza kuwa Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, Roho Mtakatifu ni Mungu na kwa pamoja, na sio kwa upweke, wanaunda Mungu Mmoja. Utatu ni wa milele, bila mwanzo wala mwisho, na ni sawa.”   

Kanisa la Roman Katoliki linaeleza: Utatu ni istilahi inayotumiwa kuonyesha imani kuu ya dini ya Kikristo.... huku Kanisa la kiothodox la Kigiriki, linauita Utatu kuwa ni “Imani ya msingi ya Ukristo hata wanafikia kusema: Wakristo ni wale wanaomkubali Kristo kuwa ni Mungu.” Katika kitabu “Imani Yetu ya Ukristo ya Kiothodox”, kanisa hilo hilo linatangaza kuwa: “Mungu ni utatu. ... Baba ni Mungu kamili. Mwana ni Mungu kamili. Roho Mtakatifu ni Mungu kamili.”  
 
JINSI UTATU ULIVYOKUA KATIKA ITIKADI YA KIKRISTO

Mateso kwa Wakristo na ukandamizwaji wa kanisa la mwanzo chini ya watawala wa Kirumi yalioanza mwanzoni mwa karne ya kwanza, yameishia kwa kupata nguvu kwa Mfalme Constantine huko Milvian Bridge mwaka 312 C.E. matokeo yake, kwa kupitia kuingia kwake katika Ukristo, watu walipata nafuu fulani kisiasa, kijeshi na mapato ya kijamii. Matokeo yake, maelfu ya wale wasio Wakristo walijiunga na Kanisa na kumuwezesha Constantine kupata nguvu kubwa katika mambo ya Kanisa.

Na ilikuwa katika kipindi cha utawala wa Constantine pale wazo la kuwa Yesu Kristo ni sawa sawa na Mungu Baba, lilipopata nguvu. Naam, utatu haukuwa imani iliyofahamika kwa wakati huo. Wazo la mungu wa utatu lilichochea mabishano makali ndani ya kanisa kwani mapadri na walei (waumini wa kawaida) wengi hawakukubali nafasi ya Kristo kuwa ni Mungu.

Huku kutoafikiana kulifikia kiwango cha kupambana kati ya Askofu Alexander wa Alexandria, Misri na kuhani wake Arius. Askofu Alexander alifundisha kuwa Yesu ni sawa na Mungu kinyume na Arius. Kwa hiyo mkutano wa kanisa ulifanyika huko Alexandria mwaka 321 C.E., Arius aling`olewa na kufukuzwa.

Ingawa, Arius alichukiwa katika taasisi, bado alikuwa na wafuasi wengi nje ya Misri. Maaskofu wakuu wengi, kama vile msomi wa historia Kaisaria Eusebius wa Palestina na somo yake mwenye nguvu nyingi, Eusebius, Askofu wa Nicomedia, kimsingi wanaafikiana na arius: Yesu Kristo si Mungu.

Mabishano yenye kuendelea yalimsumbua Constantine na ili kuhalalisha nafasi yake, aliwaalika maaskofu wote wa Kanisa la Kikristo huko Nicaea (kunapojilikana kama ni Asia ndogo) mwaka 325 C.E. Kwa hiyo baraza la Nicaea lilianza kupatanisha ugomvi unaohusu mahusiano kati ya Mungu na Mwanawe. Constantine, aliyekuwa mkuu wa utendaji, alitumia nguvu yake ya kisiasa kuwabebesha maaskofu mzigo wa kukubali itikadi yake. Kanuni ya imani iliyosainiwa na maaskofu 218 kinaganaga ilikuwa ni ya kumpinga Arius. Kwa maneno mengine, kanuni ya imani ya Nicaea iliidhinisha kuwa Mwana ni sawa na Mungu. Maaskofu mia mbili kumi na wanane walisaini kanuni hiyo, ingawa kwa hakika ilikuwa ni kazi ya wachache.

Insaiklopidia Britannica inafupisha maendelezo ya Baraza la Nicaea kama ifuatavyo:

Baraza la Nicaea lilikutana mnamo Mei 20, 325. Constantine mwenyewe alitwaa uenyekiti, kwa uchangamfu aliongoza mjadala, na yeye mwenyewe alipendekeza (hakuna shaka kuwa kuna machagizo ya Ossius) njia muhimu sana inayoeleza mahusiano ya Kristo na Mungu katika kanuni ya imani iliyotolewa na baraza hilo, "ni asili moja na Baba. "Wakitishwa sana na mfalme, mapadri, kukiwa na wapingaji wawili tu, walitia saini kanuni hiyo, wengi wao wakiwa wapo kinyume na matakwa yao.

Constantine aliuchukulia uamuzi wa Nicaea kama ufunuo mtakatifu. Kwa muda alioishi hakuna aliyethubutu kiwaziwazi kuhoji kanuni ya Nicaea; lakini mapatano yaliyotarajiwa hayakufuata.

Imani ya Nicaea

Tunaamini Mungu mmoja ambaye ni Baba Mwenyezi, muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana; na Bwana mmoja Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, mzaliwa wa Mungu Baba, Mwana wa pekee, yaani, ni kiini cha Baba, Mungu wa Mungu, Nuru ya Nuru, Mungu wa kweli wa Mungu wa kweli. Amezaliwa sio ameumbwa, na ni asili moja na Baba, kupitia Yeye vitu vyote viliumbwa, vitu vya mbinguni na vitu vya ardhini; ambaye kwa ajili yetu sisi binadamu na kwa uwokovu wetu, amekuja ardhini na kufanywa kuwa na mwili, na akawa mtu, akateseka na akafufuka katika siku ya tatu, akapaa mbinguni, atarudi kuhukumu waliohai na wafu.
 
Na kwa Roho Mtakatifu.
Na wale wasemao "Kulikuwepo wakati yeye hakuwepo," na "Kabla ya Kuzaliwa kwake hakuwepo," na kuwa, "Amepata uhai kutoka katika kutokuwepo; au wale wanaodai, kuwa Mwana wa Mungu 'Ni wa asili au kiini kingine"
au "ameumbwa"
au, "kigeugeu"
au "wa kubadilishwa"
Hizo ni laana za Kanisa la Katoliki na la Mitume.

Imani ya Nicene

Bettenson anafafanua kanuni ya imani ya Nicene kama ifuatavyo: [Iliundwa huko Espiphanius, Ancoratus, 118, C.A.D. 374, na iliporwa na wanzuoni, takriban neno kwa neno, kutoka kwa Wahadhiri wa Catechetical wa S. Cyril Jerusalem; iliyosomwa na kuthibitishwa huko Chalcedon, 451, ikiwa ni imani ya (Mapadri 318 waliokutana huko Nicaea na kwa hiyo) wale 150 waliokutana baadaye, (yaani huko Constantinople, 381). Tangu hapo wameitwa Constantinopolitan au imani ya Nicaeano-Constantinopolitan, na lilifikiriwa na wengi kuwa ni kujikumbusha kwa kanuni ya imani ya Jerusalem alioendeshwa na Cyril.

Tunaamini Mungu mmoja ambaye ni Baba Mwenyezi, muumba wa mbingu na nchi, na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana;
 
Na kwa Bwana mmoja Yesu Kristo, mtoto pekee wa kuzaliwa na Mungu, Amezaliwa na Baba kabla ya zama zote, Nuru ya Nuru, Mungu wa kweli kwa Mungu wa kweli, aliyezaliwa si kuumbwa, kwa asili moja na Baba, na kupitia kwake vitu vyote vimeumbwa; ambaye kwa ajili yetu sisi binadamu na kwa uwokovu wetu amekuja ardhini kutoka mbinguni, na kufanywa mwili wa Roho Mtakatifu na Bikira Maria, na kuwa mtu, na alisulubiwa kwa ajili yetu chini ya Pontius Pilato, aliuawa na kuzikwa, na akafufuka katika siku ya tatu, kwa mujibu wa maandiko matakatifu, na akapaa mbinguni, na kuketi upande wa kuume wa Baba, na atarudi tena akiwa na fahari ya kuhukumu wanaoishi na waliokufa, ambaye mamlaka yake yatakuwa hayana mwisho:

Na kwa roho Mtakatifu, Bwana na Mtoa uhai, aliyeendelea kutokana na Baba, ambaye yupo pamoja na Baba na Mwana anaabudiwa pamoja nao na kutukuzwa pamoja, aliyesema kupitia mitume:
Katika Kanisa moja tukufu la Kikatoliki na la Mitume:
Tunathibitisha ubatizo mmoja wa msamaha wa dhambi. Tunatarajia ufufuo wa wafu, na kuja kwa maisha ya milele.  

Ingawa baraza la maaskofu lilikubali imani ya Nicaea lakini hakukutajwa Utatu.

Mabishano juu ya maumbile (nature) ya Yesu yameendelea kwa miongo mingi. Mwaka 381 C.E. baraza la busara la pili lilikutana huko Costantinople.  Baraza hili lilitoa azimio la imani la Nicene linaloeleza kuwa Yesu na Mungu walikuwa ni sawa sawa, wa milele na uungu wa Roho Mtakatifu. Imani ya Utatu ikadhihiri na kuanzishwa rasmi kama jiwe la msingi la imani ya Kikristo kwa karne kumi na tano zilizofuatia.

Zingatia: Mfano "Sala ya Bwana" (Mathayo 6:9-13), Waromani katoliki wote wanatakiwa waikariri "imani ya Nicene" ambayo inajumuishwa katika sala zao.

Mfalme Theodosius ameamani Ukristo kuwa ni jambo la amri za kibeberu/kifalme:

"Ni matakwa yetu kuwa watu wote tunaowatawala watatekeleza dini hii iliyoletwa na mtakatifu Petro Mwanafunzi wa Yesu kwa Warumi. Tutaamini Mungu mmoja katika Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, chini ya ufahamu wa usawa wa utukufu na Utatu mtakatifu.

Tunaamrisha kuwa wale wanaofuata sheria hii wataingia jina la Wakristo Wakatoliki. Waliobakia, hata hivyo, wale Tunaowahukumu ni vichaa na machizi, watapata hali mbaya ya kuzusha imani bila ya kuhoji, maeneo ya vikao vyao hayatapokea jina la makanisa na wataangamizwa kwanza na kisasi kitakatifu na pili kwa adhabu kali ya nguvu zetu. Tutahakikisha kwa mujibu wa hukumu takatifu."  

Kisha, imani ya kumtukuza Maria kuwa ni "mama wa Mungu" na "mzaa Mungu" pia iliundwa katika Baraza la Pili la Constantinople (553 C.E.) na jina la "Bikira wa Milele" liliongezwa. "Katika sala na nyimbo za kidini za Kanisa la Kiothodox hilo jina la Mama wa Mungu liliombwa mara nyingi kama jina la Kristo na Utatu Mtakatifu"... "Kwa imani ya Waroman Katoliki, Maria, mama wa Mungu, alifafanuliwa kwa umbo la Busara takatifu. Hapa matendo ya kumwabudu mama wa Mungu yalipiga hatua moja mbele, na ndani yake Maria anatendewa kama vile ni asili (hypostasis) takatifu. Umbo la Busara ya Mbinguni."  
 
SABABU ZILIZOSHAWISHI IMANI YA UTATU

Sababu zilizoshawishi kuundwa kwa Imani ya Utatu zimefupishwa na Wathtower pamoja na jumuia ya kijitabu cha dini na Biblia ya Pennsylvania, 1989, katika kile kinachoweza kuzingatiwa kuwa ni bishara (utangulizi) wa imani ya Utatu:

Kupitia ulimwengu wa kale, hadi kufikia umbali wa zama za mababyloni, kuabudu miungu ya kipagani iliyo katika makundi ya utatu ilikuwa kawaida. Tendo hilo vilevile lilienea kabla, ya wakati wa Yesu na baada yake huko Misri, Ugiriki na Roma. Baada ya kufa kwa wanafunzi wa Yesu, imani hizo za kipagani zilianza kuushambulia Ukristo.

Mwanahistoria Will Durant ameona: "Ukristo haujaangamiza upagani, ila Ukristo ulianzia katika upagani... Kutoka Misri yalikuja mawazo  ya utatu mtakatifu. "Na katika kitabu cha Dini za Kimisri, Siegfried Morenz ananukuu: Utatu ulikuwa unawashughulisha sana wanateolojia wa Kimisri... Miungu mitatu inajumuishwa na kutendewa kama kitu kimoja, kinaelekezwa kwa nafsi ya umoja. Kwa njia hii nguvu ya kiroho ya dini ya Kimisri inaonesha mafungamano ya moja kwa moja na teolojia ya Ukristo."

Kwa hiyo, huko Alexandria, wazee wa kanisa wa Misri wa mwishoni mwa karne ya tatu na mwanzoni mwa karne ya nne, kama vile Athanasius, aliakisi atahri hii kama zilivyounda wazo la lililopelekea Utatu. Athari zao wenyewe zilienea, kiasi kikubwa sana hadi bwana Morenz anazingatia kuwa "Teolojia ya Waalexandria ni kiunganishi kati ya dini za urithi wa Kimsri na Ukristo."
 
Katika insaiklopidia ya Dini na Maadili, James Hasting ameandika: "Katika dini za Kihindi, kwa mfano, tunakutana na makundi ya wanautatu ya Brahma, Siva, na Visnu; Katika dini za Kimisri, makundi ya wanautatu ya Osiris, Isis, na Horus... Wala si kuwa ipo katika dini za kihistoria tu ambazo tunakuta ndani yake Mungu akitazamwa kuwa ni wa Utatu. Mtu anaweza kukumbuka kwa sifa ya kipekee ya mtazamo wa new-Platonic Mkuu au Hakika ya Kikomo." Ambao ni "kuwakilisha seti ya utatu."

Insaiklopidia mpya ya Schaff-Herzog ya Elimu ya Dini inaonesha ushawishi wa falsafa za Kigiriki: "Imani za Logos na Utatu zimepokea maumbo yao kutoka kwa Mapadri wa Kigiriki waliokuwa wakivutiwa sana, moja kwa moja au si moja kwa moja, na falsafa ya Platonic... Makosa hayo na ufisadi huo uliotambaa Kanisani kutoka katika vyanzo hivi hayawezi kupingika."
 
Kanisa la Karne tatu za mwanzo linasema: "Imani ya Utatu ilikua polepole na kwa kuilinganisha ni ya kuundwa katika zama za mwishoni;... imani hiyo ina asili katika vyanzo vya kigeni kabisa si vya Maandiko ya Kiyahudi wala Kikristo;.. imekuzwa na kupandikizwa katika Ukristo, kupitia mikono ya Mapadri wa Platonizing."

Sanamu za miungu zikiwa na nyuso tatu zilipatikana katika maeneo kadhaa ulimwenguni (kwa mfano, Kampuchea, [Mungu wa Utatu wa Kibudha, c. Karne ya 12 C.E.]; Italia, [Utatu, c. Karne ya 15 C.E.];. Norway, [Utatu (Baba, Mwana  na Roho Mtakatifu), c. Karne ya 13 C.E.]; Ufaransa, [Utatu, c. Karne ya 14 C.E.] Ujerumani, [Utatu, c. Karne ya 19 C.E.]; India, [Mungu wa Kihindu wa Utatu, c. Karne ya 7 C.EI.] S.Falmyra, (Utatu wa mungu mwezi, Bwana wa mbinguni, mungu jua, c Karne ya 1 C.E.]; Babylon, [Utatu wa Ishtar, Sin, Shamash, Karne ya 2 B.C.E.] na Misri [Utatu wa Horus, Osiris, Isis, Karne ya 2 B.C.E.]).  
 
KUHALALISHWA KWA UTATU NA WANAUTATU

Wakuu wa Kikristo, katika kujaribu kuokoa Utatu, wamejaribu njia zote zilizopo ili kuhalalisha itikadi hiyo. Hata hivyo, baada ya kutumia njia zote za kimantiki zijulikanazo na akili za binadamu, na kushindwa kidhalili kabisa na hatimaye kuitangaza imani hiyo kuwa ni "FUMBO". Yafuatayo ni baadhi ya maelezo yaliyotolewa na viongozi wa Makanisa, Wanatiolojia wakuu wa Kikristo na waandishi mashuhuri waliojitokeza kinaganaga kutetea imani hiyo kwa ujasiri wa kisomi:

"Utatu Mtakatifu ni fumbo kwa ufahamu halisi wa neno hilo. Kwani akili peke yake haiwezi kuthibitisha kuwepo kwa Mungu wa Utatu, Ufunuo ndio unaofundisha hivyo. Na hata baada ya kufunuliwa kwetu kwa fumbo hilo, bado inabakia ni vigumu kwa akili ya binadamu kufahamu vipi kuwepo Nafsi tatu, lakini iwe ni Tabia (Nature) Takatifu moja."

Wanazuoni wa Kikatoliki, Karl Rahner na Herbert Vorgimler wameeleza katika Kamusi yao ya Kiteolojia: "Utatu ni fumbo... kwa ufahamu halisi..., ambalo haliwezi kujulikana bila ya ufunuo, na hata baada ya ufunuo bado haliwezi kuwa linaingia akilini kabisa."

"Imani bila ya kuhoji ni tata sana, inahitaji Ufunuo Mtakatifu." (Insaiklopidia ya Katoliki)

"Mungu ni mmoja, na Mungu ni Utatu. Kwa kuwa hakuna kitu kama hiki katika viumbe, hatuwezi kulifahamu hilo, ispokuwa ni kulikubali tu." (Monsignor Eugene Clark).

"Tunajua kuwa hilo ni fumbo gumu sana, ambalo hatuwezi hata kuanza kulifahamu." (Cardinal John 0`Connor)

"Fumbo la Mungu wa Utatu lisiloeleweka." (Pope John Paul II)   
 
IMANI YA UTATU HAIKUFUNDISHWA NA WAKRISTO WA MWANZO

Maneno "Mungu Baba", "Mungu Mwana", na "Mungu Roho Mtakatifu" si kisawe tu cha Ukristo lakini pia ni kiini cha imani ya Kikristo. Hata hivyo, imani hii inayozingatiwa kuwa ni chanzo cha dini ya Kikristo, ilikuwa haijulikani wala kutetewa na Yesu (AS) wala Wakristo wa mwanzo. Wanafunzi wa Yesu na vile vizazi vilivyofanikiwa katika robo ya mwisho ya karne ya nne C.E. kamwe hawajafikiria Mungu wa Utatu. Wao waliamini Mungu Mmoja Muweza, Mjuzi, Muumba na Mwenye miujiza anayestahiki kuabudiwa yeye peke yake.

Maelezo sahihi yaliyochukuliwa kutoka mamlaka mbalimbali za Kikristo yanajieleza yenyewe:

"Uundwaji wa 'Mungu mmoja katika Nafsi tatu' haukuwa wenye nguvu katika maisha ya Kikristo na kuungama kwa imani, kabla ya kufikia mwishoni mwa karne ya nne. Lakini kwa usahihi kabisa, uundwaji huu ambao kwanza ulidaiwa kwa jina la imani ya kuamini bila kuhoji ya Utatu. Miongoni mwa Wanafunzi wa Yesu kulikuwa hakuna kitu hata cha mbali kabisa cha mwelekeo kama huo kiakili na kimtazamo.  

Imani ya Utatu iliundwa na Wakristo kiasi cha miaka mia tatu baada ya Yesu. Injili nne za Maandiko Matakatifu (Cononical), ziliandikwa kati ya mwaka 70 na 115 C.E., hazina rejeo lolote la Utatu. Hata Mt. Paulo, aliyeingiza fikra nyingi za kigeni katika Ukristo, hakumjua Mungu wa Utatu. Insaiklopidia mpya ya Katoliki (yenye Nhil Obstat na Imprimatur, inayoonyesha ruhusa rasmi) inakiri kuwa imani ya Utatu ilikuwa haijulikani kwa Wakristo wa mwanzo na kuwa imani hiyo iliundwa katika robo ya mwisho ya karne ya nne:

"Kama ni vigumu, katika nusu ya pili ya karne ya ishirini kutoa maelezo ya wazi na manyofu bila upendeleo ya ufunuo, mageuzi ya kiimani, na mchanganuo wa kitiolojia wa fumbo la Utatu, Mjadala wa Wanautatu, Waroma Katoliki na wengineo, wanaleta aina fulani ya taswira ya kutetereka. Vitu viwili vimeshatokea. Kuna kutambuliwa kwa sehemu ya ufafanuzi na wanatiolojia wa Biblia, ikiwemo kuongezeka idadi imara ya Waroma Katoliki, na kuwa huwezi kuzungumzia Wanautatu katika Agano Jipya bila ya kuwa na kigezo madhubuti. Pia kuna mfano wa karibu sana wa utambulisho wa sehemu za wanahistoria wa imani bila kuhoji na wanatiolojia wenye utaratibu, kuwa wakati unapoongelea Wanautatu wasio na vigezo, hapo utakuwa umeshatoka katika kipindi asilia cha Ukristo na kuelekea, tuseme, robo ya mwisho ya karne ya nne. Ilikuwa ni hapo tu kwa kile ambacho kingeitwa ufafanuzi wa imani ya bila kuhoji ya Utatu 'Mungu mmoja katika nafsi tatu kiliingizwa  kikamilifu katika maisha na Fikra za Kikristo."  

"Mwanzoni imani ya Kikristo haikuwa ya Utatu... Haikuwa hivyo kwa wanafunzi wa Yesu na waliokuja baada yao, kama ilivyoakisiwa katika (Agano Jipya) na katika maandiko ya Kikristo ya mwanzoni.  (Insaiklopidia ya dini na maadili)

"Wakristo wa mwanzo, hata hivyo, mwanzoni hawakufikiria kulitekeleza wazo la (Utatu) katika imani yao. Walitoa bidii zao kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, nao walimtambua... Roho Mtakatifu; lakini hakukuwa na fikra za kuwepo watatu hao, walio Watatu sawa sawa kihakika na kuungana katika Mmoja." (Upagani Katika Ukristo wetu)  
 
JE, BIBLIA INAFUNDISHA IMANI YA UTATU?

Huku Biblia ikihubiriwa na kuaminika kuwa ni Neno la Mungu, haina imani ya Utatu inayotukuzwa sana. Kama imani hii ya Utatu ilikuwa ni ya kweli, ilitakiwa iletwe kiwaziwazi kwenye Biblia kwa kuwa tunahitaji kumjua Mungu na njia ya Kumwabudu Yeye.

Hakuna yoyote miongoni mwa mitume ya Mungu, kuanzia Adam hadi kufikia Yesu (AS), mwenye ufahamisho wa Utatu au Mungu wa Utatu. Na hakuna yoyote katika wajumbe wa Mungu aliyezungumza habari yoyote hata ya siri juu ya hilo au je, kuna rejeo lolote ima katika Agano la Kale au Agano Jipya la Biblia linalothibitisha imani hiyo. Kwa hiyo, hilo ni geni ambalo si Yesu (AS) wala wanafunzi wake anayezungumzia Utatu katika Biblia. Kinyume chake, Yesu (AS) anasema: "Marko 12:29. "Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;" Kwa mujibu wa Mt. Paulo: "Matendo 2:22 "Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;"

Aya za hapo juu zinajieleza zenyewe. Kwa nini mtu ajisumbue katika imani iliyojaa machafuko wakati Wanazuoni wa Kikristo wa vyeo vya juu hawawezi kufasiri au kufafanua imani hiyo kisomi na kiakili?  

Yesu (AS) kwa haki kabisa ameshatabiri aina ya tatizo hili katika (Mathayo 15:8-9) "Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami, nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu."

Kwa kuongezea, hilo lifuatwa na Mt. Paulo katika (2 Timotheo 4:3-4) "Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo."

Pia tunasoma zaidi katika (Tito 1:16) "Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala kwa kila tendo jema hawafai."

Katikati ya mkanganyiko huu, akili kuu miongoni mwa Wakristo zimemaliza mantiki zote zinazojulikana ili kuazima uthibitisho wa imani ya Utatu lakini wameshindwa kinyonge na kisha wametangaza kuwa hilo ni fumbo. Hata hivyo, kumwabudu Mungu Muweza hakuwezi kuwa kwa maafikiano. Yeye anataka watu wa kumwabudu Yeye peke yake kwa mujibu wa Mwongozo wake Mtakatifu. Kwa kuwa yeye ni mwadilifu, kinachofuata ni kuwa, Uadilifu wake unalazimu ujumbe wake uwe wa wazi na mwepesi katika mtindo wake. Mafundisho yake, kiujumla, lazima yasiwe na makosa/dosari yoyote, ushirikina wala kuchanganya. Lazima uwe wa ukweli kabisa, ambao siku zote utaweza kuhimili changamoto za elimu ya aina yoyote zikiwemo za magunduzi ya wanadamu katika nyanja za kisayansi. Kwa vile iamani ya Utatu yenyewe ni "Fumbo", kwa hiyo, haiwezi kuzingatiwa kuwa ni neno takatifu. Biblia inasema: (1 Wakorinto 14:33) "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani..."

Kuhusiana na Maandiko ya Kiyahudi
Isaiklopidia ya dini inakiri kuwa: "Wanatiolojia wa sasa wanakubaliana kuwa Biblia ya Kiyahudi haina imani ya Utatu". Na Isaiklopidia mpya ya Kikatoliki vilevile inasema: "Imani ya Utatu Mtakatifu haijafundishwa katika Agano la Kale."

Sawa sawa, katika kitabu chake "Mungu wa Utatu", Jesuit Edmund Fortman anakiri: "Agano la kale..... halituelezi chochote kwa uwazi au kwa kulazimisha kinachodokeza Mungu wa Utatu ambaye ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.... hakuna ushahidi wa kuwa mwandishi yoyote mnyofu aliyewahi kugusia kuwepo kwa (Utatu) ndani ya Uungu. Hata ukitazama katika ("Agano la Kale"), mapendekezo, maashirio na  alama za siri juu ya nafsi tatu, utaziona kuwa huko ni kwenda nje ya maneno na dhamira ya waandishi wanyofu."  

Kuhusiana na Maandiko ya Kigiriki  
Isaiklopidia ya dini inasema: "Wanatiolojia wanakubaliana kuwa agano Jipya pia halina imani ya wazi ya Utatu."

Jesuit Forman anaeleza: "Waandishi wa Agano Jipya... hawatupi muundo au kuundwa kwa imani ya Utatu, hakuna mafundisho ya wazi kuwa ndani ya Mungu mmoja kuna nafsi tatu takufu zilizo sawasawa... Hakuna sehemu yoyote tunapokuta imani yoyote ya utatu ya dhati tatu zilizombali mbali za maisha matakatifu na matendo kwa Mungu huyo huyo."

Kamusi Mpya ya Kimataifa ya Tiolojia ya Agano Jipya inaeleza sawa sawa na hayo: "(Agano Jipya) halina imani ya Utatu iliyoendelezwa. 'Biblia haina tangazo lilochambuliwa kuwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni asili sawasawa.' [amesema mwantiolojia wa Kiprotestanti Karl Barth']."

"Mwanahistoria Arthu Weigall ananukuu: "Yesu Kristo kamwe hajaonyesha jambo kama hilo, na hakuna popote katika agano Jipya kunapodhihiri neno Utatu. Hilo wazo liliundwa tu na Kanisa miaka mia tatu baada ya kufa kwa Bwana wetu." "Upagani katika Ukristo wetu"  
 
KUPINGWA IMANI YA UTATU NA WAKRISTO WA KISASA.

Wanatiolojia wa Kikristo wa kisasa walio wengi wanapinga kutii bila ya kuhoji imani za Makanisa zilizoimarishwa. Wa hivi karibuni kabisa na aliye mashuhuri sana miongoni mwao ni Askofu mpya wa Durban, Askofu David Jenkins, Profesa wa Tiolojia na Masomo ya Kidini Chuo Kikuu cha Leeds, anasema kuwa baadhi ya matukio katika kazi za mwanzo za Yesu: "HAYAKUWA YA KWELI KABISA ISPOKUWA YALIONGEZWA KATIKA HISTORIA YA YESU NA WAKRISTO WA MWANZO ILI KUELEZEA IMANI YAO KWAKE, KUWA YEYE NI MASIHI."  

Profesa John Hick anasema: "Kile kilichoendelezwa na Waorthodox kuwa ni tabia (natures) mbili za Yesu, uungu na ubinadamu vilivyojiunda pamoja ndani ya Yesu Kristo wa kihistoria kinaendelea kuwa ni maneno tu bila ya maana iliyotajwa." Anaongezea kusema: "Kwa kusema, bila ya ufafanuzi, kuwa Yesu wa Nazareti wa Kihistoria, pia alikuwa ni Mungu huko hakuna maana ni kama kusema duara hili lililochorwa na penseli katika karatasi pia nalo ni mraba. Msemo huo umelazimika upewe maana ya muktadha: na katika hali ya lugha ya kuonesha kuwa Yesu ana mwili, basi kila kilichomo na kilichopendekezwa lazima kikataliwe," Aliendelea kupendekeza kuwa uungu wa kuwa na mwili ni mitiolojia ya wazo la kubuni. Amesema tena: "Natumia istilahi ya 'ngano' katika ufahamu ufuatao: "ngano ni simulizi iliyoelezwa lakini si sahihi, au ni wazo au taswira ambayo inatumika kwa mtu au kitu lakini hakiendani na ukweli. "Kuwa Yesu alikuwa ni Mungu, Mwana mwenye mwili kihakika si ukweli, kwa vile halina maana halisi, ispokuwa anafanyiwa Yesu kwa ufahamu wa maruweruwe ambao kazi yake ni kulinganisha na lile wazo la uungu mwana lililopachikwa katika ulimwengu wa kale kwa kila aliyekuwa mfalme."
 
Maneno ya Victor Paul Wierwille katika iktabu chake: "Yesu Kristo si Mungu". "Ninasema kuwa Yesu Kristo si Mungu, lakini ni Mwana wa Mungu. Wao si "sawa, bila ya mwanzo wala mwisho, wala hawapo sawa." Yesu Kristo kwa maana halisi hakuwa na Mungu hapo mwanzo; wala hakuwa na sifa zote za Mungu."   
 
Maelezo makini ya Victor Paul Wierwille: "Kabla ya kufunga, acha niweke wazi hisia zangu. Kwa kusema kuwa Yesu Kristo si Mungu, katika akili zangu hakuvunji heshima, wala umuhimu wa Yesu Kristo kwa njia yoyote ile. Kiwepesi hilo linamtukuza Mungu, ambaye ni Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, kwa upekee Wake, Ametukuka na yupo kwenye nafasi isiyo na kifani. Yeye peke yake ndiye Mungu."  

Ninaamini kuwa Yesu (AS) aliumbwa na Mungu; na kuwa alikuwa ni "Masihi" (mpakwa mafuta) na ni Mtume wa Mungu; na alikuwa ni neno la Mungu lililopelekwa kwa Maria na ni roho toka kwake. Simkubali yeye kuwa ni Mungu au Mwili wa Mungu, Mwana wa Mungu wala Mungu mwana. Mungu na Yesu  (AS) ni tofauti kabisa na ni wenye kutengana. Mungu ni Muumba na Yesu (AS) alikuwa ni kiumbe aliyeumbwa. Wao ni wenye asili tofauti na za kipekee kwa wakati mmoja, kwa nguvu, elimu na nafasi.

Maelezo mbalimbali ya Yesu na ile mitume ya Mungu yote iliyotangulia (AS), inayopatikana katika Biblia wanazibatilisha imani zote mbili: ufahamu wa "MUNGU MWENYE MWILI" na "IMANI YA UTATU". Chochote kile ambacho ni kinyume na maelezo yangu si lolote ila uvumi ulioundwa na watu wanaohitaji kuthibitisha hoja yao. Ushahidi walio nao mkononi mwao ni wa kutomewa (kuingizwa) kulikotambaa ndani ya Injili asilia ya Yesu (AS) na ujumbe wa kwanza wa Mungu. "Yesu (AS) si Mungu ila ni Mtume mkuu tu! Na ni Mjumbe wa Mungu."
 
MAFUNDISHO YA MITUME YA MUNGU

Ajabu, hakuna mtume yoyote kabla au baada ya Yesu (AS) aliyefundisha imani ya Utatu. Ispokuwa, wametangaza upweke wa Mungu. Mungu pekee ndio Mwenye uwezo. Yeye ni Mwenye Nguvu na Muumba wa kila kitu kinachoonekana na kisichoonekana na hana mshirika, mwenza, jamii, famila, watoto wala msaidizi katika Uungu wake. Yeye pekee ndiye Mlezi na mpaji wa viumbe vyote. Yafuatayo yanatoa mafundisho ya mitume ya Mungu:

Mtume Musa (AS) anasema: "Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa unyeti." Kutoka 18:11

"Sikiliza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Nawe mpende BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo. Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako. Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako. Kumbukumbu la Torati 6:4-9

"Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu." Kumbukumbu la Torati 4:23

Ufahamu huo huo juu ya Mungu ulithibitishwa na Yesu (AS). (Marko 12:29) "Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, "Bwana Mungu wetu ni Bwana Mmoja;" Mitume yote miwili (AS) kwa nguvu zaidi wamethibitisha nukta ya kuwa Bwana wao na Bwana wetu ni Mungu Mmoja. Pia inafaa kutazamwa, kuwa hakuna kitu katika maelezo yao kinachoashiria kuwa kuna yoyote miongoni mwao aliyeshea Uungu.

"Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu." 1 Samweli 2:2  
 
Mtume Daudi (AS) anasema katika Zaburi ya Biblia: "Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote." aya 83:18) "Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na adhama." Zaburi 104:1 "Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Duniani mwote mna hukumu zake." Zaburi 105:7 "BWANA ndiye aliye Mungu, Naye ndiye aliyetupa nuru." Zaburi 118:27 "Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru, Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza." Zaburi 118:28

Mtume Suleimani (AS) anasema: "Kumcha BWANA ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu." Mithali 9:10

Maneno yafuatayo yalikuwa yakisemwa sana na Mtume Suleimani (AS): "Hii ndio jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu." Mhubiri 12:13

Mtume Isaya (AS) anasema: "Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki." Isaya 40:28

Kwa waziwazi, Muumba wa pekee ni Mungu, aliyeumba kila kitu (ulimwengu mzima na vilivyomo ndani yake) maelfu ya miaka iliyopita kabla ya kuja kwa Yesu (AS). Yesu mwenyewe aliumbwa na Mungu na hivyo hivyo Roho Mtakatifu. Kwa hakika, kulikuwa hakuna utatu hadi ulipoundwa na wanadamu katika karne ya tatu C.E.

"Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani, kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake." Yesu (AS) alitetea kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa ispokuwa Mungu peke yake. Mathayo 4:10 na Luka 4:8

Mtume Yesu (AS) anasema: (Yohana 17:3) "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."

Maelezo ya hapo juu ya Yesu (AS) yanathibitisha kuwa kuna Mtukufu mmoja tu "Mungu wa pekee wa kweli" na kuwa yeye hakujua chochote juu ya Utatu. Kandoni mwa hayo, Yesu (AS) hakutoa madai ya Uungu, kwa kuwa yeye alilinganishwa kuwa ni Kiumbe "Yeye" ni Mungu wa pekee wa kweli na ni yeye ni mjumbe tu wa Mungu, yaani "Yesu Kristo aliyemtuma".

Mt. Paulo hakung`amua juu ya kuwepo kwa Utatu. Anasema: "Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;" Matendo 2:22

"Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo." 1Wakorinto 8:5-6

"Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake." Quran 2:136

"Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu." Quran 7:59
"Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu." (Quran 2:132)

"Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina." (Quran 3:67)

"Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake." (Quran 2:133)

"Na kwa A'adi tulimpeleka ndugu yao, Hud. Akasema:Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?" (Quran 7:65)

"Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu." (Quran 7:73)

"Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwishakufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini." (Quran 7:85)

"Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani, Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na t'iini amri yangu!" (Quran 20:90)

"Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu." (Quran 21:83)

"Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi, Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini." (Quran 27:15)

"Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri." (Quran 27:16)

"Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi. Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya na tukamponyeshea mkewe. Hakika wao walikuwa wepesi wakutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea." (Quran 21:89-90)

Mtume Yesu (AS) anasema: 'Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabudni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka." (Quran 3:51)

Wakati Mtume Muhammad (SAW) alipoulizwa na mtu mmoja ni tendo gani akilifanya ataingia Peponi, akasema: "Mwabudu Allah, na usimshirikishe na chochote..." (Al-Bukhar – hadithi za Mtume Muhammad [SAW])

Mtume Muhammad (SAW), anasema: "Kama mtu atashuhudia kuwa hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah, Peke yake, asiye na mshirika na kuwa Muhammad ni mjumbe wake na Yesu ni Mjumbe wa Allah na ni neno lake alilolitoa kwa Mariamu na ni Roho itokayo kwake na kuwa Pepo ni kweli na Moto ni kweli, Allah atamuingiza Peponi kwa matendo yake aliyoyatenda hata kama yakiwa ni machache." (Al-Bukhar – hadithi za Mtume Muhammad [SAW]).

Katika hadithi sahihi nyingine ya Mtume Muhammad (SAW), anasema: "Yeyote atakayekufa huku akijua kuwa hakuna Mola ispokuwa Allah, ataingia peponi." (Al-Bukhar – hadithi za Mtume Muhammad [SAW]).

Ibn "Abbas anasimulia kuwa Mtume Muhammad (SAW), amesema: "Nataka kukufundisha kitu. Mtii Allah, Naye atakulinda. Zihifadhi amri zake, Naye atakuwa nawe (kama mlinzi wako). Utakapoomba, muombe Allah peke yake; utakapotaka msaada, taka msaada kwa Allah peke yake. Kumbuka, kama watu wote wataungana kukusaidia, hawataweza kukusaidia ispokuwa kwa kile alichokukadiria Allah; na kama watu wote wataungana kukudhuru, hawatokudhuru ila kwa kitu alichokukadiria Allah." (Tirmidhi – Hadithi za Mtume Muhammad [SAW]).

Katika hadithi nyingine ya Mtume Muhammad (SAW): "Allah hatowaadhibu watu kwa dhambi zao ispokuwa kama mtu atakuwa muasi, na mwovu dhidi ya Allah na anayekataa kuamini kuwa hakuna Mola ispokuwa Allah." (Hadithi za Mtume Muhammad [SAW]).

"Yesu hakuwa Mkristo; lakini kabila lake lilikuwa la Kiyahudi. Hakuhubiri imani mpya, lakini aliwafundisha wanadamu kufanya matakwa ya Mungu. Kwa maoni yake, vile vile, kwa Wayahudi, matakwa ya Mungu yalitakiwa yapatikane katika Sheria na katika vitabu vingine kwenye maandiko."  
 
BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU MUNGU NA YESU (AS)

Vifungu vifuatavyo kutoka katika Biblia vinaonyesha hakika ya tabia ya Mungu na Yesu (AS). Kwa sasa ni wazi kuwa Mungu pekee ndiye Mkuu, Mtawala, Asiyeshindika na Muweza. Yesu (AS), kiumbe mwenye kikomo, ameteseka kwa matakwa na mapenzi ya Mungu. Maneno na vitendo vya Yesu, vyote kwa uwazi kabisa vinaashiria udogo wake mbele ya Mungu.

1. Ushuhuda wa Biblia kuhusu Mungu

Mafundisho ya Agano la Kale na Jipya kimsingi ni ya imani ya Mungu mmoja na kuwa Agano Jipya halikengeuki na kumwacha Mungu mmoja na kwenda katika Utatu ndani ya Mungu mmoja.  Yesu amethibitisha mafundisho haya pale aliposema: "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie." Mathayo 5:17-18

Maelezo ya Mungu ni mepesi, ya wazi na hayana kupingana wala kuchanganya. Haya ni baadhi ya "maneno ya ufunuo" wa Mungu katika Biblia. Mungu anasema:

"...Mimi ni  Mungu Mwenyezi..." Mwanzo 17:1

"Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu,  Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu?" Kutoka 15:11

"Mimi ni BWANA, Mungu wako...". Kutoka 20:2
 
"Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao." Kutoka 20:3-5

Aya hizi kwa hakika zinaharamisha aina zote za sanamu za Mungu, tena ni kwa aina zote mbili za kumwabudu au za kumwakilisha Mungu tu. Hakuna sanamu inayoweza kumtosha Mungu kuliko Mungu Mwenyewe. Yeye ni Muweza hawezi kuwa na taswira-picha ya mwanadamu ila kwa kile alichokifunua Yeye mwenyewe kuwa ni Sifa Tukufu aliyoipeleka kwa mitume.

"...mimi ndimi BWANA, Mungu wenu. Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu; mimi ndimi BWANA Mungu wenu." Walawi 19:3-4

"Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?"  Hesabu 23:19
 
"Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye." Kumbu kumbu la Torati 4:35

"Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja." Kumbukumbu la Torati 6:4

"Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nauhisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu." Kumbu kumbu la Torati 32:39

"Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu." 1 samweli 2:2

Sulemani anasema: "...Ee BWANA Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini; ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote." 1 Wafalme 8:22
 
"Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe Mungu peke yako." Zaburi 86:10

"Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki." Isaya 40:28

"Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu." Isaya 42:8
 
"Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua; na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine. Mimi, naam, mimi, ni BWANA, zaidi yangu mimi hapana mwokozi." Isaya 43:10-11

"...Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu." Isaya 44:6

"Mimi ni BWANA wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua; ili wapate kujua toka maawio ya jua, na toka magharibi, ya kuwa hapana mwingine zaidi yangu mimi; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine." Isaya 45:5-6

"Maana BWANA, aliyeziumba mbingu, asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara; hakuiumba ukiwa, aliiumba ili ikaliwe na watu; Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine." Isaya 45:18

"Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;" Isaya 46:9

"Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia. Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu..." Isaya 48:12-13

"BWANA asema hivi, Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu; mtanijengea nyumba ya namna gani? Na mahali pangu pa kupumzika ni mahali gani?" Isaya 66:1

"Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake." Yeremia 10:10

"Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu nchi ya Misri; wala hutamjua mungu mwingine ila mimi; wala zaidi ya mimi hakuna Mwokozi;" Hosea 13:4

2. Ushuhuda wa Biblia kuhusu Yesu (AS)

Kuzaliwa kwa Yesu (AS) kulitabiriwa: "Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu." Luka 1:26-27 Hapa Mungu hajashuka chini ili awe na Mwili kama inavyodaiwa na baadhi ya makanisa, badala yake Yeye amempeleka malaika wake Gabriel (Jibrilu) kumwabarisha Mariamu juu ya mpango wa Mungu. Yesu (AS) alikuwa ni roho iliyoumbwa kwa nguvu za Mungu tumboni mwa Mariamu. Kwa kuwa, aya hizi zinakana imani ya Mungu kuwa amejivisha mwili, na kwa hiyo zinafafanua kuwa hoja hizo hazina msingi.

Malaika Gabriel alimwabarisha Mariamu: "Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu." Luka 1:31

Kwa hiyo, nani waliokuwa wahusika wa Utatu (yaani Mungu mmoja ndani ya watatu) kabla ya kuzaliwa kwa Yesu (AS)? Kulikuwa na Mungu Mmoja tu hapo mwanzo, anayeishi milele. Utatu uligeuzwa kutoka katika imani ya Mungu Mmoja kuelekea kwa Miungu Mitatu na upagani. Kabla ya Yesu (AS), watu waliamini Mungu Mmoja tu, lakini baada ya kuzaliwa kwake, Kanisa liliongeza nafsi mbili za ziada katika Uungu. Pili, wakati Yesu (AS) alipokuwa kijusi, je, Mungu muweza naye alikuwa ni mwenye kunywea? Kwa kuwa Wanautatu wanahoji kuwa nafsi mbili au tatu zimejiunga katika MWILI MMOJA. Je, wote walikuwa kama kijusi kimoja tumboni mwa Mariamu? Kama ni hivyo, kwa nini alimzaa Yesu peke yake? Utoto ulioje na kichefuchefu kilioje kufikiria kuwa Yesu (AS) aliungana na Mungu kimwili?

Mungu, ambaye hana mwanzo wala mwisho na aliyeumba mbingu na nchi, na kila kitu kati ya Mbingu na nchi kwa mamilioni ya miaka iliyopita, kabla ya kudhihiri kwa ustaarabu wa binadamu. Vizazi vingi vimeshapita kabla ya kuzaliwa kwa Yesu (AS).

"Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba." Luka 2:21 Kufuru ilioje dhidi ya Mungu! Kama Yesu (AS) ndiye Mungu wa kweli, je, unaamini kuwa anahitaji atahiriwe?

"Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu, ilikuwa juu yake." Luka 2:40 Mwanzoni, huyu "mungu" Yesu alikuwa hana elimu [hajui] alipokuwa mdogo lakini alipata elimu alipofikia balehe. Elimu ya Mungu wa kweli haiongezeki wala haipungui si kwa wakati au nafasi kwa sababu Yeye muda wote ni Mkamilifu na Mtimilifu.

Wakati Yesu (AS) aliposali "Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]" Luka 11:2-4 Je, mtu anaweza kujisalia nafsi yake? Kwa hakika haiwezekani! Kwa hiyo, hili linampambanua Mungu wa kweli badala ya Mtume Yesu (AS). Kwa kuongezea, Matakwa ya Yesu yametofautiana na yale ya Mungu, jambo linaloashiria kuwa wao si kitu kimoja wala si sawasawa.

Imetajwa kuwa Mtume Yesu (AS) amefunga: "Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa." Mathayo 4:2 Kufunga ni njia mojawapo ya mtu kutubia dhambi na kuonyesha utiifu na unyenyekevu kwa mkuu zaidi. Mungu si mnyenyekevu kwa yoyote yule wala hahitaji kufunga ili atubie dhambi zake, wala hata kutaka kuteseka, kinyume na Yesu (AS) Mungu yu huru na chochote kwa sababu Yeye Peke yake ndiye Mkuu na Mkamilifu.

Makutano makubwa ya watu yalikuja kumsikiliza Yesu (AS) na kuleta wagonjwa wengi walioponywa magonjwa yao. "Hata ule mkutano wakastaajabu, walipowaona mabubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona, wakamtukuza Mungu wa Israeli." Mathayo 15:31 Itakuwaje Mungu wa Kikristo ni WATATU huku Mungu wa Kiisraeli ni MMOJA?

"Na akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba ya kuwa ikiwezekana, saa hiyo imwepuke. Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; walakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe." Mathayo 26:29 na Marko 14:35-36) Yesu alielekeza maombi yake kwa nani? Je, amejielekezea kwake yeye mwenyewe kwa sifa kuwa yeye ni sehemu ya Uungu? Kwa hakika la! Kwa kweli, Yesu (AS) daima alimuomba Mungu amsaidie hata alipomfufua Lazaro. Tazama Yohana 11:41-43. Yesu daima amekuwa ni mwenye kumshukuru Mungu jambo linaloashiria kutojiweza kwake kikamilifu na kunyenyekea kwa Mungu.

"Hata asubuhi alipokuwa akienda mjini, aliona njaa. Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu..." Mathayo 21:18-19 Mungu kuhisi njaa na kutojua msimu wa matunda!

Mt. Paulo anasema: "Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;" "Matendo 2:22 Hapa, ni wazi kile anachokimaanisha Paulo kwa maneno "aliyedhihirishwa kwenu na Mungu" ni mpakwa mafuta na Mungu au "Mteule wa Mungu – akiwa ni mtume".
3. Kile anachokisema Yesu (AS) juu yake na Mungu

Yesu Kristo (AS) kamwe hajataja juu ya Utatu wala hakuwa macho kuwa kuna Mungu wa Utatu. Ufahamu wake ulikuwa ni ule ule kama wa wale mitume Waisraeli wa mwanzo, waliohubiri Upweke wa Mungu.

"Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote." Marko 12:29-30

"...Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake." Mathayo 4:10 na Luka 4:8. Yesu (AS) anasema kuwa ni Mungu peke yake ndio wa kuabudiwa.

"...Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.." Marko 12:29 Yesu (AS) anathibitisha upweke wa Mungu.

"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliyembinguni."  (Mathayo 7:21) Ni wazi kuwa Mungu alikuwa Mbinguni na Yesu (AS) alikuwepo ardhini. Kwa hiyo vipi watakuwa wameungana katika mwili mmoja?

Imani ya Kikristo inaeleza kuwa 'Nafsi Tatu' zimeungana katika mwili mmoja (watatu ndani ya mmoja). Itawezekana vipi kwa waunda Utatu wote wawe Miungu kamili wakati kila mmoja wao anaunda moja ya tatu ya Uungu?

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma." Yohana 17:3. Hapa, Yesu (AS) anachora mstari kati ya Mungu na yeye mwenyewe.  Ili ufikie uzima wa milele ni kujua Mungu wa kweli na Yesu (AS) kuwa ametumwa akiwa ni Mjumbe wa Mungu tu.

Yesu (AS) anasema: "Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu." Marko 10:18. Yesu (AS) anatetea kuwa hakuna mwema ispokuwa Mungu, na hilo linamtenga Mungu na Yesu.

"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake." Mathayo 24:36 na "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba." Marko 13:32 Yesu (AS) anakiri kuwa elimu yake ina mipaka finyu kinyume na Mungu, ambaye ni mjuzi wa kila kitu. Pia, hukumu ni ya Mungu peke yake anayetunza siri zote Yeye mwenyewe.

"Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile." Yohana 5:19 Hapa, Yesu (AS) anakiri kumtegemea Mungu.

"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama niskiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka." Yohana 5:30

"Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka." Yohana 6:38

"Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka." Yohana 7:16

"...na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo." Yohana 8:28
 
Yesu (AS) anaweka wazi sana kuwa Yeye ana upungufu wa nguvu takatifu. Yeye mwenyewe hawezi kufanya lolote kwa kuwa Mungu pekee ndiye chanzo cha nguvu na mamlaka.

"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu..." Yohana 8:40 Yesu (AS) ameungama kuwa Yeye alikuwa ni Mjumbe anayetimiza kazi aliyoamrishwa na Mkuu.

Ziada, Mtume Yesu (AS) anasema: "Yesu akamwambia, usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Yohana 20:17 Aya hii inatia nanga (inaumaliza) UTATU na IMANI YA MUNGU KUWA NA MWILI. Inaonesha mahusianao ya Yesu (AS) na Mungu kuwa ni kama ya binadamu yoyote yule yaani kusali na kuomba msaada toka Kwake.

Aya zote za hapo juu zinalenga kuonesha kuwa Yesu (AS) hajitoshelezi, mdhaifu na anategemea Rehema za Mungu.
 
KINACHOSEMWA NA QURAN TUKUFU KUHUSU MUNGU

Quran ni ufunuo wa mwisho wa Allah Muweza. Allah ameieleza nafsi yake katika njia ya wazi sana kiasi ambacho haiwezi kukubali fasiri nyingine ila ile ya maana ya maandiko yaliyoandikwa. Maneno ya Allah Muweza na ya Mitume Yake ni maneno ya Kweli. Hakuna shaka, maneno Yake ni wazi, mepesi na yanajifafanua yenyewe bila ya kuchanganya. Allah ni Mwanzilishi wa mbingu na ardhi, Uwezo na Elimu yake havina Kikomo. Yeye ni BWANA, Mnyanyuaji na Mtawanyaji wa viumbe vyote. Kwa hiyo, wanadamu wasidanganyike na maruweruwe ya uongo kuwa kuna miungu mingine kinyume na Mtawala Mkuu Allah.

Hebu tukiakisi kisemwacho na Quran juu ya Allah, mwenye sifa za ukamilifu na anayestahiki yeye peke yake, kuwa Mungu wa Kweli, na ambaye peke Yake tu ndio Muweza:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu;. Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. Quran 1:1-5
Enyi watu! Muabuduni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni nyinyi na wale wa kabla yenu, ili mpate kuokoka. (Mwenyezi Mungu) ambaye amekufanyieni hii ardhi kuwa kama tandiko, na mbingu kama paa, na akateremsha maji kutoka mbinguni, na kwayo akatoa matunda yawe riziki zenu. Basi msimfanyizie Mwenyezi Mungu washirika,   na hali nyinyi mnajua. Quran 2:21-22
Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu akakufufueni! Kisha atakufisheni, tena atakufufueni, kisha kwake mtarejeshwa?. Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. Quran 2:28-29
 Yeye ndiye Muumba wa mbingu na ardhi pasina ruwaza; na anapotaka jambo basi huliambia tu: Kuwa! Nalo huwa. Quran 2:117
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye Aliye hai, Msimamia mambo yote milele. Hashikwi na usingizi wala kulala. Ni vyake pekee vyote viliomo mbinguni na duniani. Ni nani huyo awezaye kuombea mbele yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao; wala wao hawajui chochote katika vilivyo katika ujuzi wake, ila kwa atakalo mwenyewe. Enzi yake imetanda mbinguni na duniani; na wala haemewi na kuvilinda hivyo. Na Yeye ndiye aliye juu, na ndiye Mkuu. Quran 2:255

Enyi mlioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakawasema ndugu zao waliposafiri katika nchi au walipokuwa vitani: Wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wasingeliuwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo. Quran 3:156

Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni. Quran 4:1

Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. Quran 5:76

Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni mwa washirikina. Quran 6:14

Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa? Wala hawana uwezo wa kuwanusuru wala wenyewe hawajinusuru. Quran 7:191-192
Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipokuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa. Quran 20:8
Au nani anayeuanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.  Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa.  Quran 27:64-65
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mkwasi, Mwenye kusifiwa. Quran 31:26
Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. Quran 55:29
Yeye ndiye Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye nguvu,  Anayefanya analolitaka, Mkubwa, Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo mshirikisha nayo. Quran 59:23

Yeye ndiye aliyekuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliyekafiri, na yupo aliyeMuumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda Quran 64:2

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Wala hana anaye fanana naye hata mmoja. Quran 112:4
 
UTHIBITISHO WA BIBLIA JUU YA IMANI YA UTATU

Wanautatu, katika kuunga mkono Utatau, wananukuu baadhi ya mistari tu kutoka katika Biblia, tafsiri zao ni za ajabu sana. Tafsiri hizo zipo mbali na muktadha wa maandiko asilia. Biblia, kiujumla inafundisha Upweke (Imani ya Mungu mmoja) kuanzia kitabu cha kwanza (Mwanzo) mpaka kitabu cha Mwisho (Ufunuo).

Zifuatazo ni nukuu za mistari hiyo ikiwa ndio kama ushahidi wa kuwepo kwa Imani ya Utatu:

Ushahidi wa kwanza kutolewa ni mstari unaopatikana katika (1 Yohana 5:7) ambao unapatikana katika Toleo la King James (KJ) la Biblia, lililoandikwa mwaka 1611: "Kuna watatu huko mbinguni, Baba, Neno na Roho Mtakatifu." Mstari huu umeshaondoshwa katika matoleo mengi ya Biblia yaliyorekebishwa kwani ilijulikana kuwa haukuwa katika mswada asilia ispokuwa ni maongezo ya baadaye.

Ushahidi wa pili ni (Mathayo 28:19) "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu."

Ushahidi wa tatu ni: (2 Wakorinto 13:13-14) "Watakatifu wote wawasalimu. Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa roho Mtakatifu ukae nanyi nyote."

Ushahidi wa nne ni (1 Wakorinto 12:4-6) "Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote."

Kwa ushahidi wa pili, wa tatu na wa nne, kule kutajwa tu kwa majina (jina-maelezo) hakuwezi kabisa kuunda Utatu, zaidi ya kuwahesabu mmoja mmoja tu. Wao kwa hakika, ni watatu waliotofauti tofauti wakiwa na tabia/vimo na hali mbalimbali. Hao watatu kamwe hawajakuwa sawasawa kiwakati, eneo, elimu, nguvu kama ilivyofafanuliwa imani ya Utatu. Kwa kuongezea, pale Yesu alipobatizwa kwa mujibu wa (Mathayo 3:16), Roho wa Mungu alimshukia akiwa kama njiwa. Kwa hivyo, vipi Yesu (AS) adaiwe kuwa ni sehemu ya Utatu wakati siku zote amekuwa na roho mtakatifu?

Baadhi ya mistari katika Biblia inayotolewa kama uthibitisho inamnyanyua Yesu Kristo (AS) kuwa Mungu kwa uundwaji wa baadaye wa imani ya Utatu:

Mfano wa kwanza: "Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu...." (Mwanzo 1:26) Baadhi ya wanatiolojia wa Kikristo walifikia hitimisho kuwa Mungu hakuwa mmoja peke yake wakati wa kuumba. Hata hivyo, Mungu anasema Yeye Mwenyewe kwa nafsi ya kwanza wingi na hili linaweza kufafanuliwa kuwa ni wingi wa kutia mkazo ambao unaonyesha Ukuu wa Mungu, utukufu na adhama. Wanazuoni (Wasomi wa Kidini) wa Kikristo wanafafanua hili kama ni kuashiria ukamilifu wa nguvu takatifu au nguvu bayana zisizo na kikomo kwa Mungu au Mungu katika ukamilifu wake. Baadhi wanauita wingi wa heshima na kwa kisarufi (kanuni za lugha) unachukuliwa kuwa ni wingi wa utukufu. Katika Mwanzo, kitabu cha kwanza cha Biblia, Mungu peke yake bila ya msaidizi ndiye aliyeathiri Uumbaji (mfano, sura 1, aya 3) "Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru." Katika aya 27 ya sura hiyo hiyo, inasema: "Mungu akaumba mtu kwa mfano wake..." Aya za hapo juu haziashirii msaidizi yoyote au mwenza wa Mungu yoyote yule. Na Kitenzi kinaeleza kile Kilichosemwa na kufanywa na Mungu kuwa ni umoja (mfano, Mungu aliona kuwa nuru ni nzuri, Mungu ameumba mbingu, Mungu ameumba mtu, Mungu amewabariki, Mungu amemaliza kazi zake, nk)

Mwanzoni mwa kitabu cha Mwanzo, tunasoma "Hapo mwaazo......" Zingatia kuwa, wakati neno mbingu ni wingi, neno Mungu na nchi ni umoja. Kwa nini mbingu ni wingi? Sababu ni nyepesi; Quran inatwambia kuwa mbingu ni saba. Na kwa nini Waandishi wa Biblia wanaendelea na maneno Mungu na nchi kwa umoja? Ilikuwa ni kwa sababu wanajua kwa hakika kuwa nchi ni MOJA TU na Mungu ni MMOJA TU kama ilivyofundishwa na Mitume yote ya Mungu.

Mfano wa pili: "Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu." (Yohana 1:1) Zingatia kuwa, hakuongea Yesu (AS) ispokuwa ni Yohana. Pia, kila mwanazuoni wa Biblia Mkristo anakubali kuwa aya hii ya pekee iliingizwa na Myahudi, aitwaye Philo wa Alexandria Misri kabla ya tukio la Yesu na Yohana Mbatizaji, Rehema na amani ziwe juu yao.

Zaidi, wakalimani wengi wa miswada ya Kigiriki kwenda Kingereza katika (Yohana 1:1) neno Mungu likitokea kwa mara ya kwanza wanaliandika kwa Kuanzia na herufi kubwa 'M' wakikusudia ni Mungu Muweza lakini likitokea kwa mara ya pili wanaliandika kwa herufi ndogo 'm". Kwa hiyo, hiyo 'g' ndogo kikawaida inatumika kwa viumbe si kwa Mungu Muweza kama katika Zaburi (82:6: Sema "Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa aliye juu, nyote pia." na katika 2 Wakorinto (4:4) "ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu." Kwa kuwa Neno Hili (lililotokea mara ya pili), lina maana ya "pamoja na Mungu", huyo hawezi kuwa Mungu Muweza lakini ni "mungu" tu kama katika mifano iliyo hapo juu.

Tangu, tafsiri za kisasa za Biblia kuonyesha maana ya Yohana 1:1 katika mifano ifuatayo:

"Hapo mwanzo kulikuwa na Neno, naye Neno alikuwa na Mungu; na Hilo Neno lilikuwa mungu."

"Hapo mwanzo Neno lilikuwapo, na Neno lilikuwa na Mungu, na Hilo Neno lilikuwa mungu."

Kwa upande mwingine, baadhi ya wanazuoni wa Kikristo wamelitafsiri "Neno" kuwa ni "Amri Takatifu", kwa hiyo, wao wanahoji kuwa uchaguzi mzuri wa maneno ya (Yohana 1:1-3) Lazima yawe: "Hapo mwanzo kulikuwa na Amri, na Hiyo Amri ilikuwa Takatifu. Hiyo (Amri) ilikuwapo mwanzoni pamoja na Mungu. Na hiyo Amri ilikuwa Takatifu. Vitu vyote vilifanywa na (Amri hiyo): na bila ya hiyo kusingeumbwa kitu, kilichoumbwa." Neno la Kigiriki lilotumiwa na Yohana ni Logos linalotokana na neno lego – maana yake 'kuongea'. Neno la Kingereza 'Decalogue' maana yake 'Amri Kumi' ni mchanganyiko wa maneno ya Kigiriki deka (Kumi) na logous (Amri). Hilo neno logos linamaanisha, "Amri iliyosemwa na Mungu.

Hilo neno 'pamoja' linaunda fumbo/swali la kukanganya kwa wale wanaopendelea kulionyesha hilo neno Logos kama ni 'Yesu' badala ya 'Amri'. Sababu ni wazi kabisa: Vipi Yesu ataweza kuwa pamoja na Mungu na ni Mungu vile vile?

Ufahamu wa Amri zilizosemwa na Mungu kuwa zipo 'pamoja na Mungu' tangu 'mwanzo', unafanana na ufahamu wa Biblia juu ya Uumbaji. "Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru...." (Mwanzo 1:3). Katika maandishi ya Kigiriki, Yohana ametumia [definitive article] 'the' (ho) kabla ya 'Mungu' (Theo), kwa sababu Hilo ni Kiima (subject). Hapa, Yohana hajaitumia [definitive article] 'the' kabla ya 'Mungu' kwa sababu ni kiarifa (predicate). Kwa maneno mengine, neno lililotumiwa hapa linamaanisha tabia/maumbile (nature), kiwango, sifa au miliki ya kiima. Kwa mfano huu, tabia ya amri za Mungu ni takatifu. Katika baadhi ya matoleo ya Biblia, neno 'hili' linabadilishwa na 'This (one)' au 'He (Yesu)'. Hata hivyo, hilo neno 'This' linaashiria 'Amri iliyosemwa'.

Zaidi, ni wazi kuwa katika (Yohana 1:1) Mungu peke yake amekuwepo milele. Maneno yake daima yapo pamoja Naye, katika hali ile ile ya kuwa maneno yako yapo pamoja nawe, na maneno yangu yapo nami. Neno analolitamka Mungu si Mungu mwingine wala Mungu mwenyewe lakini ni Neno Takatifu (Amri) kutoka Kwake. Vinginevyo, kila kiumbe kitakuwa ni Mungu kwa kuwa kila kiumbe kinawakilisha Neno Lake. Hoja hizo hizo zimetumika katika (Mwanzo 1:3). Nuru iliyoumbwa kwa Neno Lake si Mungu lakini kuumbwa kwa nuru ni kwa Neno Lake Takatifu. Kwa hiyo, ibara "Hilo neno Lilikuwa Mungu" katika Yohana 1:1 ndani ya Biblia lipo nje kabisa.

Kwa kuongezea, kama tutajaribu kusoma maandiko mengine yanayohusiana na Uumbaji, tutatambua kuwa, Mungu Muumba ametumia Maneno yake katika kila uumbaji kama ilivyo katika Quran (mfano "Kun fayakuunu" inayomaanisha kwa Kiswahili "Kuwa basi kinakuwa": Mwanzishaji wa Mbingu na ardhi: pale alipoamuru jambo, Analiambia, "Kuwa". Nalo linakuwa.   

Mfano wa tatu: "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30) Wakristo wameufahamu  mstari huu kuwa unamaanisha kwamba Baba (Mungu) na Yesu (AS) ni kitu kimoja; wameungana katika mwili mmoja; Mungu akawa na mwili ndani ya nafsi ya Yesu (AS) na aliishi miongoni mwa wanadamu. Maana hiyo hiyo imetolewa pale Yesu (AS) anaposema: "Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake." (Yohana 14:10-11) Pia katika (Yohana 14:20)  "Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu." Hata hivyo, wao wanatafsiri vibaya maana ya mstari wa 28 wa sura hiyo hiyo wakati Yesu (AS) anapotangaza: "Mlisikia ya kwamba mimi niliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi." Kama kile kilichosemwa na Yesu (AS) ni kweli kuwa Baba ni mkuu kuliko yeye, kwa hiyo, hili linafanya tatizo liishe, na kuwa wao si sawasawa.

Pia, wanautatu hawatambui kuwa kwa kuzifuata hoja zao, matokeo yake yataleta jumla ya miili 15 aliyojibiringisha katika mwili mmoja. Nayo ni "hesabu nyepesi" kama ya kuwekwa katika darasa la chekechea. Baba ni Mungu, Mwana (Yesu) ni Mungu na Roho Mtakatifu ni Mungu – (mfano wa Utatu) ulioundwa na vilivyopo vitatu (3) (Nafsi tatu) zimeungana ndani ya Mungu mmoja. Ongezea katika muungano huo wanafunzi (12) wa Yesu kwa namna ile ile kama ilivyofahamika na Wakristo (Yohana 14:20) watazalisha jumla ya vilivyopo kumi na vitano (15) vimejiviringisha na kuungana katika mwili mmoja.

Mstari wa (Yohana 17:21-23) "Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi." Aya za hapa juu zinaonesha  hakuna maana nyingine zaidi ya "umoja wao kimalengo" unatupa maana ya wazi juu ya tabia ya kuwa wao wana lengo moja.

Kandoni mwa hiyo, katika (yohana 10:31-36) hajadai kuwa yeye ni "Mungu" au "Mungu mwana" kwa kuwa wameungana na Baba (Mungu), ispokuwa yeye ni kiumbe aliyetofauti.

Ikiwa kwa upande mwingine, Wanautatu wanasisitiza kuwa (Yohana 10:30) inaunga mkono imani ya Utatu, sasa, wasiweke kikomo cha idadi ya Mungu wao kuwa ni utatu (3) ispokuwa wanatakiwa waongeze wanafunzi 12 katika (Yohana 14:10 na 20) kama walivyofahamu maana zao, kuwa wapo "kila mmoja ameyayukia ndani ya mwili mmoja." Kwa hiyo, mtanziko utakuwa mkubwa sana na mtandao wa maangamizi (Utatu) utakuwa unatatiza zaidi.

Mfano wa nne: "Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; Basi wewe wasemaje?, Utuonyeshe baba?" (Yohana 14:9) Lakini, hivi Yesu (AS) hakusema kinaganaga kuwa "Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona." (Yohana 5:37) Hapa, Yesu (AS) anasema kuwa yeye si Mungu kwa sababu alikuwa anaongea na kumwona yeye. Na katika (Mathayo 7:21) Yesu (AS) anasema: "Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni." Wakati kwa muda huo Yeye alikuwa mbele yao. Maelezo haya yote ya Yesu (AS) yana maana moja tu, nayo ni: Mungu na Yesu si kitu kimoja. Vipi itakuwa Baba (Mungu) na Yesu wawe kitu kimoja na wameungana katika mwili mmoja (kama inavyotafsiriwa na Wakristo) wakati Baba yupo mbinguni na Yesu (AS) yupo ardhini?  

Kumwani Mungu, unatakiwa uheshimu viumbe vyake ambavyo havina idadi: jua, mwezi, nyota, na kila kitu kilichotuzunguka. Katika (Yohana 4:24) Yesu (AS) anahoji: "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli." Kwa hiyo, vipi mtu ataweza kumuona Mungu? Na katika (Yohana 1:18) tunasoma: "Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote…"

Kwa kuongezea, Yesu (AS) ametoa tofauti za wazi kabisa kati yake na Mungu katika mistari ifuatayo ndani ya Injili ya (Yohana 14:1) "Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi" Neno "na" ni muhimu sana kiasi ambacho, linaonesha kuwa Mungu ametengana kabisa na Yesu (AS). Katika (Yohana 17:3): "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."

Mfano wa tano: (Yohana 20:28) "Tomaso akajibu, akamwambia,  Bwana wangu na Mungu wangu!" Hata hivyo, kifungu hiki hakimaanishi chochote kwa sababu kimeshakanwa na mistari iliyoonyeshwa hapo juu. Wanazuoni wanaunga mkono wazo la kuwa katika hali kama hiyo ya kimiujiza, maneno ya Mwanafunzi Tomaso yangejaaliwa kuwa ni mshangao wa kushutushwa kwa sababu ya jambo la kushangaza mbele za Yesu (AS), wakati kwa hakika, huo mshangao umeelekezwa kwa Mungu. Kando ya hayo, Tomaso hakumzingatia Yesu (AS) kuwa ni Mungu, kwa kuwa alijua vizuri sana kuwa Yesu (AS) kamwe hajadai kuwa yeye ni Mungu. (Yohana 17:3).

Kwa hakika, Mt. Paulo anatoa tofauti nyingine iliyo wazi kabisa kati ya Mungu na Yesu (AS). Yeye amehoji kuwa Mungu amempaisha Yesu kama ilivyoelezwa katika Biblia katika sehemu mbili (1 Wakorinto 15:15-20) na (Marko 16:19): "Basi Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu." Kama kwa hakika kabisa, Mungu na Yesu ni kitu kimoja na ni sawasawa, je, isingekuwa ni jambo la kufaa zaidi kusema: "Yesu amejipaisha mwenyewe?" na wakati Yesu (AS) aliporipotiwa kuwa amekaaa mkono wa kuume wa Mungu, je, haikuwa madhubuti kusema: "na Yesu (AS) ameketi kwenye "Kiti cha enzi"? Ukweli mgumu ni kuwa, hakuna Mwenye Kiti cha Enzi kinyume na Mungu, anayestahiki kuabudiwa kama ilivyosemwa na Yesu (AS) na si yeye Yesu (AS), aliyetukuzwa (Yohana 17:30)

Katika mstari mwingine Mt. Paulo anafafanua Mungu ni nani (Matendo 17:24): "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;"

Katika tofauti hizi kati ya Mungu na binadamu, Muumba na muumbwaji, Asiye na kikomo na mwenye kikomo, je, hilo lipo nje ya utambuzi wa binadamu? Ni uzembe tu, unafiki na matashi ya uasi kukataa kufahamu.

Hoja za nyongeza zinazomnyanyua Yesu na kuwa ni Mungu.

Wakristo wanahoji kuwa, Yesu (AS) ni Mungu Mwenye mwili, akiwa ni Mungu kamili na binadamu kamili. Ufahamu huu, unakanushwa kabisa na Yesu (AS) kwa maneno yake katika (Mathayo 1:18-20) "Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa roho Mtakatifu." Kwa hiyo, wapi swala la kuwa na mwili linapoibukia? Hiyo inatueleza kwa maneno mepesi kuwa Mungu ni mwenye kuwa tofauti na ameepukana na Yesu (AS). Kwa hiyo, hilo linaonyesha kukataliwa na kubatilishwa kwa imani ya kuwa ana mwili. Kandoni mwa hayo, ili awe Mungu kamili inamaanisha kuwa hana shida wala haitaji msaada, na kuwa mwanadamu maana yake ni, kuwa bila ya utakatifu.

Wakristo wengine wanahoji kuwa Yesu (AS) ni Mungu kwa sababu yeye naye aliitwa "Mwana wa Mungu", "Masihi", "Mwana wa Adam na ni "Mwokozi". Hata hivyo, Yesu (AS) amesema kuwa "mpatanishi" kama "Mwana wa Mungu". Katika tamaduni ya Kiyahudi, mtu yoyote anayefuata matakwa ya Mungu alikuwa akiitwa "Mwana wa Mungu". Tazama mifano iliyonukuliwa kutoka katika Biblia: (Mwanzo 6:2-4); (Kutoka 4:22): (Yeremia 31:9); (Zaburi 2:7); (Luka 3:38); (Warumi 8:14). Katika (Luka 6:35), Yesu (AS) anasema: "Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi, nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu,...."  Kuwa Mwana wa Mungu, hakumnyanyui kufikia daraja ya Uungu. Kama vile mtoto wa Rais hakumfanyi mtu awe Rais ispokuwa ni mtoto tu.

Ziada, imenukuliwa katika Biblia kuwa "Masihi" kwa Kiebrania maana yake ni "Mpakwa mafuta na Mungu" na sio "Kristo", na "Cyrus" Wapersian anaitwa "Masihi" au "Mpakwa mafuta" (Mwanzo 31:13); (Walawi 8:10); (Samweli 2:10); (Isaya 45:1); (Ezekieli 28:10). Ezekieli alielezwa katika Biblia kuwa ni ("Mwanaadamu". "Mwokozi", katika (2 Wafalme 13:5), watu wengine walipewa jina hilo vile vile bila ya kuwa waungu. Neno "mpakwa mafuta wa Mungu" linamaanisha kutoa mamlaka ya kiroho kwa mtu mwema kueneza maneno ya Mungu. Kwa hiyo, vipi neno hili liwe kigezo cha kumnyanyua Yesu (AS) afikie nafasi ya Uungu?

Swali lingine la Dollar Bilioni moja: "Ukristo ni nini bila ya Imani ya Utatu?"
 
HOJA ZA NYONGEZA ZINAZOKANUSHA IMANI YA UTATU

Si mara moja kwa Yesu (AS) kuchukuliwa kuwa ni "Mungu Mwana". Bali ni "Mwana wa Mungu" tu au "Mtoto wa Mungu". Zaidi ya mara 68 katika Agano Jipya jambo linalomaanisha kuwa yeye si Mungu kabisa. Kusema kuwa marejeo yote mawili ni kitu kimoja na ni sawasawa kimaana yanapingana na sheria za lugha, na kuacha matumizi yake halisi kama nyenzo ya kuwasiliana.

Yesu alikuwa ana mwanzo kwa sababu aliumbwa na Mungu. Hakuwa wa milele pamoja na Mungu wala Mungu Muweza sawasawa kwa ufahamu wowote; naye mara zote amekuwa ni mada ya kuzingatiwa na Matakwa ya Mungu na ataendelea kuwa hivyo.

Arius amemtambulisha Mungu kuwa ni 'agenetos', chanzo cha msingi sana cha kila kitu ambaye yeye mwenyewe amekuwepo bila chanzo.  Hiki ndicho kinachompambanua Mungu na vitu vingine, katika msingi wa Kuwepo kwake. Logos (au Neno) kutoka katika Injili ya Yohana, limekuwepo kutoka kwa Mungu na kwa hiyo hilo neno si Mungu kwa ufahamu ulio kamilifu.

Imani ya Utatu ni wazi kuwa imekengeuka (imepotoka) na kuacha mafundisho asilia ya mitume ya Mungu. Kumwabudu Mungu kwa mujibu wa matakwa Yake maana yake ni kukataa imani ya  Utatu kwa ujumla. "Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani;..." (1 Wakorionto 14:33).

Kwa hiyo, John Baker anaandika hivi: "Yesu hajajiona kuwa yeye ni kama vile kila mtu, wala kuwa ni mwokozi wa Dunia, pia hata kidogo hajajiona kuwa yeye ni kiumbe mwenye maisha ya utakatifu wa kiroho kabla ya kuzaliwa yatokayo mbinguni." John Baker anakiri kuwa Yesu 'alifahamika vibaya kuhusu mpango wake aliopangiwa na Mungu aufuate' na anaendelea kuhoji: 'kukosea juu ya maelezo ya mustakabali' ni 'tabia ya binadamu' na kuwa 'hilo linaweza kushindwa kwa kumpa Yesu nguvu za uungu mkuu ambazo kwa hakika, zimeshibisha ndoto ya zamani na iliyochoka ya wapagani lakini itaondoa kabisa hakika ya Mungu kuwa na mwili."

Kwa kuutambua ukweli huu, John Hick, mhariri wa "Maruweruwe ya Mungu kuwa na Mwili", katika dibaji yake, amesema: "Mahitaji yanayoibuka kutokana na kukua kwa elimu ya asili za Ukristo, na kujumuisha utambuzi wa kuwa "Yesu alikuwa kama alivyotajwa katika (Matendo 2:22) 'mtu aliyeletwa na Mungu kwa kushika nafasi maalumu katika lengo takatifu, na kwa hiyo, ufahamu wa baadaye juu yake (Yesu) kuwa yeye ni Mungu Mwenye mwili, mwenye nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu aliyeishi maisha ya kibinadamu, ni jambo la kubuniwa au njia ya kishairi ya kuelezea umuhimu wake kwetu."

Imani ya Kikristo inaeleza kuwa 'Nafsi Tatu' zimeungana katika mwili mmoja (utatu katika Mungu mmoja). Vipi kila mshiriki wa Utatu huo awe Mungu kamili wakati kwa hakika kila mmoja wao anafanyiza 1/3 ya Mungu? Kwa kweli ni upuuzi kudhani kuwa kila mmoja ni Mungu kamili wakati watatu hao wamejiviringisha ndani ya kitu kimoja na kwa hiyo wanaunda Mungu kamili mmoja.

Vilevile, wakati Yesu (AS) alipokuwa ardhini, hakuwa Mungu kamili, wala "Baba naye huko mbinguni" hakuwa Mungu kamili, jambo ambalo linapingana na maneno ya Yesu (AS). Yeye anasema katika (Yohana 20:17): "...ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Kama Mungu alikuwa ni utatu katika mmoja, nani aliyekuwa Mungu  huko mbinguni wakati wa siku tatu za madai ya kusulubiwa na kufufuka? Nani alikuwa Mungu pale Yesu alipokuwa tumboni mwa Maria?

Kama imani hii ingekuwa ndio mafundisho ya Yesu (AS), basi angeieleza kwa maneno ya wazi. Kwa kuwa, neno Utatu hata halijaandikwa katika Biblia, ispokuwa badala yake, Yesu amesema katika (Marko 12:29) "...Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja;"

Wakristo wengi kamwe hawajafikiria juu ya hatari ya vidokezo vya utatu katika Mungu mmoja (Utatu). Vipi Mungu atafurahishwa au kuabudiwa wakati haijulikani Mungu ni nani?

"Falsafa inatueleza kuwa hakuna kitu kilichopo ambacho kutokana na hicho kitu kingine kinaweza kutokea na kuishi vikiwa tofauti na viwe sawasawa na kushirikiana na kisha izingatiwe kuwa kitu hicho ni kamili. Kumsifu Mungu ni mwana huko ni kukana ukamilifu wa Mungu."   

"Kumnyanyua Yesu kuwa na hali ya Mungu huko ni kufikia katika kufuru ya kusikitisha dhidi ya Mungu mmoja wa kweli, wakati huo huo kumtofautisha Yesu na Mungu hakumvunjii heshima Yesu ispokuwa ni kumweka Yesu katika nafasi ya hali ya juu sana nayo ni mtume na mjumbe wa Mungu."

"Yeye ndiye aliyekuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliyekafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayoyatenda." Quran 64:2

Uthibitisho zaidi wa kubatilisha hoja ya imani ya Utatu:

"Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu, lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu" (Mathayo 20:23). Peke yake, Yesu (AS) alikosa nguvu au mamlaka ya kutoa chochote ispokuwa kile alichoamriwa na Mungu, anayeitwa "Baba".

"Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe." (Mathayo 26:39). Hapa Yesu (AS) anatafuta msaada wa Baba yake, akisisitiza kuwa hilo si kwa matakwa yake, lakini ni kwa Matakwa ya Mungu. Ushahidi wa hapa ni kuwa matakwa yake yanatofautiana na ya Mungu.

"…Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Mathayo 27:46). "Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu." (Luka 23:46). Maneno hayo, yaani "Mungu wangu" yanatoka kwa mtu aliye katika mateso tu. Na kama Yesu (AS) alikuwa ni Mungu, sasa nani aliyekuwa akimtelekeza? Je, alikuwa anajitelekeza mwenyewe? Hiyo ni kebehi. Mungu hahitaji kuwajibika kwa Mungu mwingine.

"…Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu." (Marko 10:18). Yesu (AS) amesisistiza kuwa hakuna aliyemkuu katika uungu au wema ila Mungu. Huko, ni kutojishirikisha yeye mwenyewe katika Uungu.

"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba." (Marko 13:32) Kama kweli Yesu (AS) angekuwa ni sawasawa na Mungu au sehemu ya Utatu, angejua kila alichokijua Baba.

"Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda;…" (Yohana 5:19).

"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo..." (Yohana 5:30).

"…Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka." (Yohana 7:16).

Katika maelezo matatu yaliyo hapo juu, Yesu (AS) ameweka wazi kuwa hakuna mamlaka wala nguvu aliyobaki nayo na kuwa kile alichokihubiri kimetoka kwa Mungu.

"…Baba ni mkuu kuliko mimi." (Yohana 14:28). Maelezo haya kwa hakika yanakanusha imani ya Utatu kwa maana wote wawili ni tofauti kabisa, mmoja ni mkuu kuliko mwingine.

"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma." (Yohana 17:3). Mungu hukutajwa na Yesu (AS) kwa mfumo wa Wingi, Mungu aliyemtaja kama ni Baba.

"...ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." (Yohana 20:17). Yesu (AS) hakuwa Mungu kwa sababu naye alikuwa na Mungu wake aliyemwita "Baba".

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee,..." (Yohana 3:16). Kama Yesu (AS) ni sehemu ya Utatu huku wote watatu wakiwa ni wa milele, bila mwanzo wala mwisho, na ni sawsawa, vipi awe mwana na wakati huo huo ana umri sawa na baba yake? Tazama (Mathayo 1:18, Luka 1:26 na 1Yohana 4:9).

"Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;" (1 Timotheo 2:5). Sentensi hii inajifafanua yenyewe kuwa Mungu na Yesu (AS) wanatofautiana tena wapo mbalimbali.

"Ufunuo wa Yesu Kristo, alipopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi;…" (Ufunuo 1:1). Mungu wa kweli ni Mjuzi wa yote, kwa hiyo, hili linatupilia mbali ile nadharia ya Utatu.
 
JE, YESU (AS) ANATHIBITISHA UFAHAMU WA ROHO MTAKATIFU?

Mungu kwa hekima na Rehema zake zisizo na kikomo, ameshatuma mitume mara kadhaa kusambaza UJUMBE Wake na kuwaita viumbe katika kufanya wema (yaani njia ya AMANI na UTIIFU kwa Mungu Mmoja wa Kweli). Huo Ujumbe unaitwa UISLAMU (kutii matakwa ya Mungu).

Ujumbe huu ulisambazwa kwa mataifa na makabila yote ulimwenguni kwa kufuatia mlolongo wa vizazi ukiwaita wanadamu kutii Matakwa ya Mungu. Hata hivyo, funuo zote za mwanzo zilibadilishwa na kupotoshwa na vizazi vilivyokuja baadaye, na mitume wakapuuzwa na kuteswa. Ufunuo safi wa Mungu umechafuliwa na maruweruwe, ushirikina, kuabudu masanamu na imani za kijinga. Kwa hiyo, dini ya Mungu ilipotezwa na kuingizwa katika mkondo wa ibada mbalimbali za uongo.

Historia ya nyendo za binadamu imekokotwa kati ya nuru na kiza. Mungu, kwa wingi wa Mapenzi na Rehema zake kwa wanadamu hajatuacha kizani tugundue njia ya haki kwa kujaribu na kukosea pekee. Amemtuma mjumbe wake wa mwisho, Mtume Muhammad (SAW) kuwaongoza binadamu katika kipindi kinachojulikana kuwa ni zama za kiza. Ufunuo, (yaani Quran Takatifu kwa kupitia malaika (Gabriel) Jibrilu) alioupokea Muhammad (SAW) unawakilisha chanzo cha msingi cha uongozi, chanzo chenye kukusanya mambo yote na cha maumbile ya dunia nzima. Mwongozo huu Mtakatifu unatoa muhtasari wa maarifa na hakika kuhusu Muumba Muweza, ulimwengu, lengo la kuumbwa kwetu na maisha yetu ya hapa duniani na Ahera. Ufunuo huo utawaongoza wanadamu kuelekea NJIA YA KWELI, WEMA na MAFANIKIO katika maisha haya na ya baadaye.

Kusema kuwa atakuja "mpatanishi /mshauri/ Mwombezi/ Roho wa kweli mwingine akiwa ni "mtume mwingine" kama vile Musa na Yesu (AS) ni sahihi kabisa. Ufahamu wa "Roho Mtakatifu" badala ya "mtume mwingine" umekanwa kikamilifu na Injili ya Yohana.

Ili kufahamu ujumbe wa Yesu (AS) juu ya maudhui hii, unatakiwa uanze na waraka wa kwanza wa (1 Yohana 2:1) Hapa, utamfahamu Yesu (AS) alikuwa ni "Mwombezi halisi", "Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,"

Yesu (AS) aliyekuwa "Mwombezi halisi" ameshatabiri kuja kwa "Mwombezi mwingine". Hata hivyo, ikirejewa Biblia kama ilivyotafsiri hilo neno "Mwombezi" kwa maneno mbalimbali ambayo msomaji anaweza kuyafikia kwa kutegemea nani aliyeandika Biblia, (yaani Msaidizi/ mpatanishi/ mshauri/ mwombezi/ Roho wa kweli/ Roho Mtakatifu).

Neno hilo hilo "Paraclete" linatumiwa katika Injili ya Yohana likiashiria utabiri wa Yesu (AS) kwa kuja kwa "Paraclete mwingine". Anasema: "Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;" (Yohana 14:16) Pia amewaambia wanafunzi wake kuwa huyo "msaidizi" atafundisha kila kitu na atawaletea kila kitu ili wakumbuke. Amesema katika (Yohana 15:26) "Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia."

Utaona katika mistari iliyopo hapo juu kuwa BIBLIA ya (RSV) imetumia neno "Counsellor" na neno hilo hilo limetajwa hapo juu (14:25) kuwa ni "Roho Mtakatifu". Lakini neno hilo hilo limebadilishwa katika (Yohana 15:26) hapo juu na kuwa ni "Roho wa kweli". Tena, katika aya zifuatazo hapa chini, imerejeshwa kwa "Counsellor" lakini utagundua baadaye kuwa neno hilo hilo kwa mara nyingine linarejeshwa kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 16:13).

(Yohana 16:7-8): "Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke; kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu, bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu." Hili limeshathibitishwa katika Quran pale Mungu alipomnyanyua Yesu (AS) na sio kusulubiwa kama ilivyodaiwa.

Katika aya ya hapo juu, (Yohana 16:7-8), kuja kwa "Counsellor" au "Paraclete" kunategemea kuondoka kwa Yesu (AS). Kando ya hayo, Yesu (AS) hajaashiria kuwa huyu "Mpatanishi" atakuja katika kipindi hiki. Katika (Yohana 16:12-15), Yesu (AS) ameendeleza utabiri wake wa kuja kwa huyu Mpatanishi mwingine aliyemwita kuwa ni "Roho wa kweli". Anasema: "Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi  kuyastahamili hivi sasa. Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari."

Aya ya hapo juu inavunja utata ulioundwa na neno Roho Mtakatifu [Holy Ghost] au Roho Mtakatifu [Holy Spirit] uliodaiwa na Wakristo kwa sababu, kwa mujibu wa Biblia katika (Mwanzo 1:2), huyu Roho Mtakatifu ameshakuwepo duniani tangu siku ya kuumbwa dunia. "Huyo-Roho Mtakatifu" vilevile alikuwepo kule mto Jordan wakati Yohana alipombatiza Yesu (AS). Kwa hiyo, vipi Yesu (AS) aseme: "bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu." (Yohana 16:7). Kile alichomaanisha Yesu (AS) ni kuwa "Msaidizi mwingine" au "Mtume mwingine" akiwa kama yeye atakuja kwa sababu kuletwa kwa Roho Mtakatifu kumeshafutiliwa mbali kabisa kwa kuwa huyo Roho Mtakatifu ameshakuwa hapa duniani tangu siku ya kuumbwa.

Zaidi, Roho Mtakatifu na Roho wa kweli hayo ni maneno mawili tofauti na kila moja linajitegemea kikamilifu. Hilo la mwisho limechukuwa kiwakilishi "he" nacho kinamaanisha yeye mwanamume, wakati ambapo ya kwanza (Roho Mtakatifu) inachukuwa kiwakilishi "it" nacho kinamaanisha hicho kitu. Yesu (AS) ametuambia kwa maneno ya sawasawa kuwa Counsellor au Roho wa kweli (paraclete) aliyemtabiri ni Mtu atakayetufundisha vitu vyote.

Viwakilishi vyote vya he vimerejea kwa "Roho wa kweli" jambo linalodhihirisha jinsi ya kiume ili liafikiane na neno "Counsellor" katika (Yohana 16:7). Hilo neno "Counsellor" ni neno kivumishi (descriptive - la kueleza sifa) linalotumika sehemu ya "Roho wa kweli", na kwa kisarufi (kigrama), kiwakilishi lazima kiafikiane kijinsia na jina linalofungamana nalo. Kwa hiyo, aya ya 13 na 15 ya Yohana 16 zinathibitisha kuwa Roho wa kweli si sehemu ya Utatu.

Kando ya hayo, katika (Yohana 16:13) Yesu (AS) ametilia mkazo nukta inayomhusu huyu Roho wa kweli, kuwa ndiye mtume wa pekee atakayefundishwa cha kufanya kutoka kwa Aliye Juu: "Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hata nena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena," Kuwa ni mtume wa pekee (si Mungu wala Roho Mtakatifu), hatokuwa na mamlaka yake mwenyewe, bali atapewa ufunuo kutoka kwa Mungu huko Mbinguni.

Zaidi, utagundua kuwa katika (Yohana 16:14), Yesu (AS) anasema juu ya Roho wa kweli: "Yeye atanitukuza mimi; kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari." Quran, ambayo ni ujumbe wa Muhammad (SAW) umewatukuza wote wawili Yesu (AS) na mama yake Mariamu. Jina Isa [Yesu (AS)] limetajwa katika Quran Takatifu mara tano zaidi ya jina Muhammad. Na ukweli ni kuwa, sura kamili ya 19 ya Quran Takatifu bayana kabisa, imeitwa jina la mama yake Yesu ambaye ni Mariamu (yaani Surat Maryam), imethibitisha kiumbuji (utaalamu wa kueleza) hoja yetu kuwa, kwa hakika, Yesu (AS) ametukuzwa sana.

Kwa kuongezea, Yesu (AS), anasema: "Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia." Hiyo ndio sababu kuwa ujumbe wa Muhammad (SAW) ambao ni Quran Takatifu ni ujumbe uliokamilika, unaojumuisha ujumbe wa Yesu (AS) na ujumbe wote uliotangulia. Kwa hakika, Quran ni kithibitisho cha ujumbe wa Yesu (AS) na wale wote waliokuja kabla yake. Huo ni ujumbe mpana unaokusanya mitazamo yote ya juhudi za wanadamu, sawa ni za kibinafsi, kijamii, kisiasa, kiuchumi au mahusiano ya kimataifa. Unaitwa UISLAMU (dini ya kutii Matakwa ya Mungu Mmoja wa Kweli – Allah) hiyo ni sheria kamili ya maisha, na vilevile ni ujumbe wa dunia nzima ulioelekezwa kwa wanadamu wote unaomwongoza mwanadamu kusuluhisha nafsi yake na Mungu Ujumbe ambao unaweza kuuita, Matakwa ya Mungu, matunda ya Uokovu.

Pia, katika (1 Waraka wa Yohana 4:6) maneno mawili "Roho wa kweli" na "Roho mwovu" yametumika kwa ajili ya mwanadamu. Na, katika MSS, Codex Syriacus ya zamani imegunduliwa mwaka 1812 katika Mlima Sinai na Bibi Agnes S. Lewis na Bibi Bensley, andiko la (Yohana 14:26), linalosomeka: "Paraclete, the Spirit" na sio "Paraclete, the Holy Spirit". Hilo neno "Roho" imerejeshwa na MSS, ya zamani, kwa "Roho wa kweli" katika (Yohana 15:26) ya Biblia za kisasa.

Mwisho, akisi kile alichokisema Mtume Isa - Yesu (AS), katika (Mathayo 21:43): "Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake."

Zingatia kuwa, onyo la Yesu (AS) kwa wayahudi pale walipokuwa waasi kwa kuamini na kuabudu miungu mingine kinyume na Mungu Muweza wa asili katika (Mwanzo 49:10) na Mtume Yakobo (AS) ameonya kuhusu Yuda. Kwa kweli ilikuwa ni kukamilisha utabiri wa awali katika (Kumbukumbu la Torati. 32:21): Mungu anasema: "Wamenitia wivu kwa kisicho cha Mungu; Wamenikasirisha kwa ubatili wao; Nami nitawatia wivu kwa wasio watu, Nami nitawakasirisha kwa taifa lipumbaalo."

Warabu wa kabla ya Uislamu walikuwa wakielezwa na watu wa Magharibi kuwa ni taifa jinga. Mwandishi mmoja amewatolea taswira ya kuwa ni "wanyama wakiwa na ngozi ya mwanadamu", ndipo, pale walipoletewa Uislamu, wakawa ni kiigizo cha wanadamu. Mtume Muhammad (SAW) ameondosha aina zote za kuabudu masanamu na kuhubiri upweke wa Mungu – Muumba. Yeye peke yake ndiye Mungu, Mlezi na Mpaji wa ulimwengu wote Asiye na Mke, Mwenza, Mshirika, Familia, mtoto wala msaidizi. Taifa la Kiarabu kwa ujumla na mtume Muhammad (SAW) kwa kipekee walikuwa ni ukamilisho wa tabiri zote za hapo juu.
 
QURAN NI NINI? NA INASEMA NINI KUHUSU YESU (AS) NA MAMA YAKE?

Quran Takatifu, ni ujumbe mpana na ni wa ulimwengu mzima uliofunuliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) kwa kupitia malaika Jibrilu (Gabriel) ukiwa ni ufunuo wa mwisho wa Mungu kwa wanadamu. Nao ni Rehema na Mwongozo kutoka kwa Mungu kwenda kwa wanadamu na ni Mfumo wa Maisha uliokamilika, kiasi ambacho unajumuisha mitazamo yote ya juhudi za mwanadamu (mfano, mfumo wa mtu wa kuendesha mahusiano ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na ni mfumo wa mahusiano ya kimataifa). Umeshahimili majaribu ya nyakati kwa kuwa inalindwa na Mungu Mwenyewe. Kwa kuwa hiki ni kitabu cha pekee cha Mungu kilichopo leo hii kikiwa safi baada ya zaidi ya miaka elfu moja na mia nne. Kinathibitisha ufunuo wote wa mitume iliyopita. Kinasahihisha makosa yaliyotambaa katika funuo zilizopita na inatangua kila kitu [chenye kasoro] katika funuo hizo. Allah anasema:

"Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliyeumba. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu. Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!. Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu, aliyokuwa hayajui. Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri. Akijiona katajirika. Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo." (Quran 96:1-8)
"Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinachotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote." (Quran 32:2)
"Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kuhakikisha yaliyotangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao." (Quran 6:92)
"Na hatukukuteremshia Kitabu isipokuwa uwabainishie yale ambayo wanakhitalifiana, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanaoamini." (Quran 16:64)
"Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao." (Quran 39:41)

Kwa hakika, kwa mujibu wa wafasiri (wafafanuaji) wa Quran, kuna malengo matatu ya ufunuo kwa Mtume Muhammad (SAW):

(1)    Kuleta umoja miongoni mwa makundi yaliyofarakana, kwa Habari njema ya Umoja, wakati wa kuhuburi Upweke wa Mungu wa kweli.
(2)    Uwe mwongozo katika njia sahihi; na
(3)    Kufungua njia ya kutubia (kuomba msamaha au kuungama dhambi) na uwokovu, na kwa hayo yatakuwa kwa rehema za hali ya juu kwa madhambi ya kupotoka. Hilo limetolewa ili wanaume na wanawake wawe wema. Na kama watakataa basi kupotea kwao itakuwa ni juu yao.

Nafasi ya Yesu (AS).

"Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa." (Quran 3:59)
"Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu – nao hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa kwao. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alimnyanyua kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao." (Quran 4:157-159)
"Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lililo kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilompelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha." (Quran 4:171)

"Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru. Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Munguni ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayoyasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanaokufuru. Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyowabainishia Aya zetu, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa. Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua." (Quran 5:72-76)
"Na pale Mwenyezi Mungu atakaposema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwishayajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyofichikana. Sikuwaambia lolote ila uliyoniamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa nao. Na uliponifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu." (Quran 5:116-117)
"Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka." (Quran 19:34-36)
"Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana! Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno! Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande. Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana. Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana. Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake." (Quran 19:88-93)
"Mariamu kamwe hajadai kuwa yeye ni mama wa Mungu, au kuwa mwanawe ni Mungu. Alikuwa ni mwanamke mwema mwadilifu. Na hapa Yesu anakanusha kuwa hajui lolote katika vitu alivyopachikwa na wale waliolichukua jina lake. Kumwabudu Mariamu, ingawa kumekataliwa na Waprotestant, kulienea kwa kiasi kikubwa katika makanisa ya mwanzo, katika sehemu zote mbili, Mashariki na Magharibi."  

Kwa kuongezea, marejeo yafuatayo katika Biblia pia yatakupa ufahamu wa mafundisho ya Yesu (AS): katika Injili ya (Mathayo 4:10), "Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani, kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake." Katika (Yohana 20:17), pale anapomwambia Mariamu Magdalena, "Yesu akamwambia, Usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, Kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Katika (Luka 18:19), pale anapokaripia mtawala maalum kwa kumwita yeye ni Mwalimu Mwema, "Yesu akamwambia, Mbona unaniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, naye ndiye Mungu." na Katika (Marko 12:29) pale anaposema: "Yesu akamjibu, Ya kwanza ndio hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja."
 
KISA CHA AJABU

Kuna simulizi ya Wachawi watatu walioingia Ukristo na wakawa wanafunzi wachamungu wa mchungaji. Huyo mchungaji aliwafundisha kanuni za Ukristo, hasa hasa Utatu. Ili kujifunza zaidi imani, walikaa sana na mchungaji huyo. Baada ya muda, rafiki wa mchungaji alikuja kumtembelea na kumuuliza juu ya kubadili dini kwa wale waliokuwa Wachawi watatu. Mchungaji alikuwa na fahari sana kuwaonyesha wale jamaa watatu waliobadili dini juu ya mafunzo yao ya imani bila ya kuhoji ya Kikristo. Mchungaji alimwita mmoja wa wale wachawi ili aonyeshe umahiri wake juu ya Utatu kwa mgeni wake.

Yule mchawi kwa furaha akasema: "Umenifundisha kuwa kuna watatu ndani ya Mungu mmoja. Mmoja mbinguni, wapili amezaliwa na Mariamu na wa tatu, ni Roho Mtakatifu, aliyeshuka kwa Masihi akiwa na umbo la njiwa, pale Mungu wa pili alipokuwa na miaka thelethini." Aliposikia haya, mchungaji aliudhika na kumgeukia na kusema huyu jamaa ni mpumbavu. Baada ya hayo, alimwita wa pili na kumpa swali lile lile. Wa pili akajibu: "Umenifundisha kuwa kuna waungu watatu wa asili, mmoja wao alisulubiwa na kufa, wakabakia wawili." Mchungaji kwa mara nyingine aliudhika na kumsukuma. Kisha alimwita wa tatu aliyekuwa ni mwerevu zaidi ukimlinganisha na wenzake waliotangulia na ameshajifunza kwa bidii kanuni za imani. Mchungaji alimtaka aeleze imani bila ya kuhoji ya Utatu. Yule mtu akajibu:

"Kile ulichonifundisha, kwa baraka za Masihi, nimeshajifunza kwa uangalifu na bidii, nacho ni kuwa moja ni tatu na tatu ni moja. Mmoja wao alisulubiwa na kufa. Hivyo basi, kwa sababu ya kifo cha mmoja, wote miungu watatu walikufa: kwa sababu wote watatu ni mmoja na wameungana; kwa hiyo, kifo cha mmoja ni kifo cha wote watatu. Vinginevyo, kusingekuwa na umoja wao."  

Hili linamaanisha kuwa kwa mujibu wa kusulubiwa kama ilivyodaiwa na Wakristo, wote wawili Mungu na Yesu Kristo (AS), wameshatoweka na kuwa ni wenye kutoweka. Kwa sababu kwa mujibu wa imani yao, Yesu ni Mungu na ni mtume, baada ya kifo chake Wakristo hawana Mungu wala Mtume au Roho Mtakatifu. Hivyo, ni kwa kupitia muungano, miungu yote mitatu walikufa kwa kifo cha Kristo. Kwa ufupi, umoja na utatu pia umetoweka baada ya kutoweka kwa Mungu, kwa sababu umoja na Utatu unabakia kwa kuwepo kwa Mungu. Pamoja na kutoweka kwa Mungu kuacha mandhari, kikawaida sifa zake nazo zitatoweka.
 
ONYO KWA WALE WANAOPOTOSHA UJUMBE WA MUNGU

Kitabu bora zaidi ni Kitabu cha Allah na mwongozo bora ni Mwongozo wa Mtume Muhammad (SAW).

Allah ameshatoa onyo kali mno kwa wale wote wanaopotosha ujumbe wake asilia kwa wanadamu:

"Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyoyaandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma." (Quran 2:79)
"Kwa hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu mali zao, wala watoto wao; nao hao ndio kuni za Motoni" (Quran 3:10)
"Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na anayezikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu." (Quran 3:19)
"Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri." (Quran 3:85)
"Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu kama ipasavyo kumcha; wala msife ila nanyi ni Waislamu." (Quran 3:102)
"Tutazitia khofu nyoyo za waliokufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi yao ni Motoni; na ubaya uliyoje kwa maskani ya wenye kudhulumu!" (Quran 3:151)
"Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliyekuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni." (Quran 4:1)

"Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali." (Quran 4:116)
"Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina." (Quran 6:14)
"Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au anayezikanusha Ishara zake? Hao itawafikia sehemu yao waliyoandikiwa, mpaka watakapowafikia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi mliokuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri." (Quran 7:37)
"Ati wanawafanya viumbe kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, nao hawaumbi, bali wao ndio wanaumbwa? Wala hawana uwezo wa kuwanusuru wala wenyewe hawajinusuru." (Quran 7:191-192)
"Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa ni mtumwa wake." (Quran 19:93)
"Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa, haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai, wala kufufuka." (Quran 25:3)
"Na nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uwongo Mwenyezi Mungu au anayekanusha Haki inapomjia? Je! Si katika Jahannamu ndio yatakuwa makaazi ya makafiri?" (Quran 29:68)
"Mkikufuru basi Mwenyezi Mungu si mwenye haja nanyi, lakini hafurahii kufuru kwa waja wake. Na mkishukuru Yeye hufurahika nanyi. Wala mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi. Hapo atakwambieni mliyokuwa mkiyafanya. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyomo vifuani." (Quran 39:7)
"Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika." (Quran 7:179)