MILIMA NI VIGINGI MAUMBO NA KAZI

MILIMA NI VIGINGI MAUMBO NA KAZI

 

 Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Na milima kuwa kama vigingi (vya ardhi).”?  Aya ya 7 ya Suratul Nabaa.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

         Milima hapo awali haikujulikana kwa lolote isipokuwa ni kama mkusanyiko wa jiwe lilikwenda juu kwa usawa wa ardhi.  Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema, “ Na milima kuwa kama vigingi (vya ardhi).”?  Aya ya 7 ya Suratul Nabaa.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

         Milima hapo awali haikujulikana kwa lolote isipokuwa ni kama mkusanyiko wa jiwe lilikwenda juu kwa usawa wa ardhi. Maana hiyo iliendelea hadi Pier Bouger alipoashiria mwaka 1835 kuwa nguvu ya mvuto iliyosajiliwa kwa aina ya milima ya Andes ni ndogo mno kuliko ilivyokuwa ikitegemewa kutokana na ukubwa wa mkusanyiko wa jiwe kama hilo. Akapendekeza udharura wa kuwepo kwa mkusanyiko mkubwa zaidi wenye kuzama chini wa mada hiyo hiyo ya milima ili iwezekane kutafsiri hali ya kipekee katika uwezo wa mvuto. Katikati ya karne ya 19, George Everest, aliashiria kuwepo kwa hali ya kipekee katika matokeo ya kupima mvuto wa milima  ya Himalayas baina ya maeneo mawili tofauti. Everest hakuweza kufasiri hali hiyo na akaipa jina la “Utata wa India”. George Ebry akatangaza mwaka 1865 kuwa aina zote za milima katika ardhi ni mkusanyiko wenye kuelea juu ya bahari kutokana na mada zilizoyeyuka chini ya ardhi, na mada hizo zilizoyeyuka zinachukua eneo kubwa zaidi ya mada ya milima. Kwa hiyo ni lazima kwa milima kuzama kwenye mada hizo zilizoyeyuka zenye eneo kubwa  ili ziweze kulinda kusimama kwake.

         Kama hivyo, elimu ya jiolojia imegundua kidogo kidogo kuwa ardhi ni mkusanyiko wa vipnde vilivyopakana vilivyoitwa mabamba ya  mabara. Pia imegundua kuwa milima mikubwa ni yenye kuelea juu ya bahari kuliko milima yenye kunyumburuka ambayo inachukua eneo kubwa zaidi huanguka. Pia imegundua kuwa milima ina mizizi inayoisaidia kuelea na kuyasimamisha mabamba hayo ili yasipinde na kutetereka. Mwanajiolojia Van Anglin anasema katika kitabu chake “Geomorphology” kilichochapishwa mwaka 1948 (uk.27) “ Inafahamika sasa kuwa ni lazima kuwepo kwa mizizi katika (AL SIYMAA)  kwa mkabala wa kila mlima uliopo juu ya  ardhi”. Ama kwa upande wa kazi au mchango wa milima katika kuituliza ardhi, kumethibitishwa na msingi wa “ Uwiano wa Hydrostaty wa ardhi”, kama ilivyoelezwa na mwanajiolojia wa Kimarekani Dutton mwaka 1889 ambapo anasema kuwa miinuko ya milima inazama ndani ya ardhi  kwa kiasi ambacho kinakwenda sambamba na muinuko na urefu wake. Uhakika wa “mbao za ardhi” ulioungwa mkono mwaka 1969, umebainisha kuwa milima inahifadhi uwiano wa kila bamba kati ya mabamba ya  ardhi.

    UPANDE WA MIUJIZA:        

       Katika wakati ambao binadamu alikuwa hajui uhakika wa milima ambao uliendelea hadi katikati ya karne ya kumi na tisa, Qurani Tukufu imeweka wazi katika aya hii tukufu kuwa milima inafanana na vigingi katika umbo na kazi. Hivi karibuni umebainika ukweli wa kufanana huko kukubwa.  Kutokana na kuwa milima ina sehemu iliyodhahiri juu ya ardhi na sehemu nyengine iliyozama ndani ya ardhi na kazi yake ni kuisimamisha sehemu inayoelea. Kadhalika, milima ina sehemu iliyodhahiri juu ya ardhi na sehemu nyengine iliyozama ndani yake inayokwenda sambamba na muinuko na urefu wake. Na kazi ya milima ni kuyasimamisha mabamba ya ardhi na kuyazuia yasipinde na kutetereka kutokana na tabaka lililoyeyuka chini yake. Kwa hiyo inadhihirika kuwa kitabu hicho ni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Muumba wa milima na dunia kuthibitisha kauli yake Mwenyezi Mungu “ Oh! Asijue Aliyeumba! Naye ndiye Avijuaye visivyojulikana na vinavyojulikana.” Aya ya 14 ya Suratul Mulki.