MATINI YA AKIDA YA TWAHAWIYA

MATINI YA AKIDA YA TWAHAWIYA

MATINI YA AKIDA YA TWAHAWIYA


Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; Mwanazuoni mkubwa Huja Al-Islaam Abuu Jafar Al-Waraaq Al-Twahawiyu wa Misri Allah amrehemu amesema: Nyaraka hizi ni ukumbusho unaobainisha itikadi ya Ahlu Sunna wal-jamaatu, na yale wanayoyaamini na kuyatekeleza kwa Mola wa viumbe vyote, miongoni mwa misingi ya dini kwa mujibu wa madhehebu ya wanazuoni wa Kiislamu wafuatao: Abuu Hanifa Al-Nuumani bin Thaabit Al-Kuufiyu, Abuu Yusufu Yakubu bin Ibrahim Al-Answaariyu na Abuu Abdallah Muhammad bin Al-Hassan Al-Shaybaaniyu Allah awawie radhi wote. Juu ya tauhidi Katika kumpwekesha Munguu tunasema ( ) kwa kujiamini ya kuwa Allah atatuwezesha. Hakika Allah ni mmoja hana Mshirika, hakuna kinachofanana naye, hakuna kinachomshinda na hakuna Mungu kinyume na yeye.
Wa tangu na tangu bila ya kuwa na mwanzo ( ). Ni wa daima bila kikomo, hamaliziki wala hatoweki, na hakitokei chochote ila akitakacho, hafikwi na fikra potofu wala hatambuliki undani wake kwa milango ya fahamu, na Hashabihiani na viumbe / wanadamu, Yu hai hafi, Yu macho halali,  Ni Muumba bila ya kuwa na haja, na Mwenye kutoa riziki bila Kusaidiwa, Anafisha bila kuhofia, Anafufua bila tabu, Ni mwenye kuwa na sifa zake hizo hizo tangu na tangu kabla ya viumbe vyake, hakuna sifa iliyozidi kwa Allah kwa kuwepo viumbe – sifa ambayo haikuwapo kabla ya kuwepo viumbe, kama alivyo na sifa zake ni za tangu na tangu, vivyo hivyo zitaendelea kuwa za milele, baada ya kuumba viumbe hajafaidika kulipata jina la (Muumba), na kwa kuanzisha viumbe hajafaidika kulipata jina la (Mwanzilishi / Muumba), Ana maana ya kuwa ni Mola Mlezi bila ya kuwepo kwa viumbe wa kuwalea, na Ana maana ya kuwa Muumba bila ya kuwepo kwa viumbe alivyoviumba. Yeye ni mfufuaji wa maiti baada ya kuwahuisha. Amestahiki jina hili kabla ya kuwahuisha, pia amestahiki jina la Muumba kabla ya kuwaumba, na haya ni kwa kuwa yeye ni Muweza wa kila kitu huku kila kitu ni fakiri mbele ya Allah.  
Kila jambo ni lepesi kwake, haitaji kitu (Hafanani na …) Ameumba viumbe kwa elimu yake, na kuwakadiria makadirio yao, na kuwawekea miisho yao, hakuogopa chochote kabla ya kuwaumba, ameyajua watakayoyafanya kabla hajawaumba, akawaamrisha wamtii, akawakataza wasimuasi, kila kitu kinaenda kwa makadirio na matakwa yake, matakwa yake yanatekelezwa, hakuna matakwa kwa waja zake, ispokuwa yale aliyoyataka yawe kwa viumbe miongoni mwa alivyovitaka na vikawa, na vile asivyovitaka viwe havikuwa.
Humwongoza amtakaye, na kumkinga na kumponya kwa ukarimu wake, humpoteza amtakaye, anadhalilisha na kutoa mitihani kwa uadilifu, na wote wamo katika mabadiliko mabadiliko kwa matakwa yake, baina ya fadhila na uadilifu wake, ametakasika na vinyume pamoja na washirika, hakuna wa kuzirejesha hukumu zake, hakuna wa kuzitolea maelezo hukumu zake, wala mwenye kuzishinda amri zake. Tumeamini haya yote na tumeyakinisha kuwa haya yote yanatoka kwake na Hakika Muhammadi ni Mja wake Mteule, ni nabii wake alimujtaba na ni nabii wake mwenye kuridhiwa. Naye ni nabii wa mwisho miongoni mwa manabii, imamu (kiongozi) wa wachamungu, bwana wa mitume, kipenzi cha Mola wa viumbe wote, na madai yote ya kupewa utume baada yake ni upuuzi na kuangamia, yeye ni mwenye kutumwa kwa majini na wanadamu wote kwa haki na uongofu, kwa nuru na mwangaza, na kwa hakika Qurani ni maneno ya Allah, yameanza kwake bila ya kuwa na namna nayo ni kauli, ameiteremsha kwa mjumbe wake ikiwa ni ufunuo, na waumini wakaisadiki hivi ilivyo kwa haki kabisa, wameyakinisha kuwa Qurani ni maneno ya Allah ya hakika, haijaumbwa kama yanavyoumbwa maneno ya wanadamu, na atakayeyasikia na akadai kuwa hayo ni maneno ya mwanadamu ameshakufuru, Allah ameshamkemea, mkosoa na kumwahidi adhabu ya moto wa Saqari, pale aliposema: ‘Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.” Quran 74:26 kwa kuwa Allah amwahidi moto wa Saqari yule anayesema: “Haya si chochote ila kauli ya binaadamu”. Quran 74:25 kwa kuwa Allah amesema hivi tumejua na kuyakinisha kuwa Qurani ni kauli ya muumba wanadamu na haifanani na kauli za viumbe.
Atakayemsifu Allah kwa maana miongoni mwa maana za wanadamu kwa hakika amekufuru. Aliyeyaona/aliyeyatambua haya amezingatia, na ameshaacha kauli zilizo kama za makafiri, na ameshajua kuwa Allah na hata sifa zake hazifanana na za wanadamu. Na watu wa Peponi ni kweli watamwona  Mungu, bila ya kumhitwu wala namna na hivyo ni kama vile kilivyotamka kitabu cha Mola wetu: “Nyuso siku hiyo……) Quran 75:22-23 na tafsiri yake ni kwa mujibu wa alivyotaka Allah Mtukufu na ujuzi wake, yote yaliyokuja katika hadithi sahihiza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, kuhusu tafsiri yake ni haki na ndivyo hivyo hivyo na maana zake ndivyo kama alivyozikusudia, hutuingilii katika jambo hilo, kwa kutaawili (kutoa fasili) kwa rai zetu, wala hatujisemei kwa matamanio yetu, kwani hakika mambo yalivyo, hakuna kilichosalimika katika dini yake ila kwa yule aliyekisalimisha kwa Allah Mtukufu aliyetukuka pamoja na mtume wake Rehema na amani ziwe juu yake, pia ujuzi wa yale yanayomtatiza anaurudisaha kwa mjuzi wake.     
Mguu wa Uislamu hausimami ila kwa mgongo wa kujisalimisha (kwa Allah), hivyo atakayeikusudia elimu ya vilivyoharamisha kuvijua, na hajakinaika na kuisalimisha fahamu yake, basi makusudio yake yatamzuia asifikie tauhidi halisi, maarifa safi na imani sahihi kwa hiyo atayumbishwa baina ya ukafiri na imani, kusadikisha na kupinga, kukiri na kukana, ana wasiwasi akihangaishwa na shaka si muumini mwenye kusadikisha wala si si mpingaji mwenye kukadhibisha.
Imani ya kumwona Allah haisihi kwa watu wa Peponi kwa yule aliyelichukulia swala hilo kuwa ni imani potofu, au aliyelifasili kwa ufahamu wake, kwani fasili ya kumwona Mungu – na fasili ya kila maana iliyoegemezwa kwa Uunguzi Ulezi wake – fasili yake inaachwa na kupaswa kuisalimisha kwake na hii ndio dini ya Waislamu. Na asiyejihadhari na kumkana na kumfananisha Allah atatereza na hatapatia kumtakasa Allah.
Kwa hakika Mola wetu Mtukufu aliyetukuka amesifika kwa sifa za upweke, umoja, na maana zake hana mtu yeyote miongoni mwa wanadamu. Ametakasika ( ) na mipaka na vikomo, nguzo na viungo, nyenzo, hazungukwi na pande sita kama wanavyozungukwa viumbe vingine vilivozuka
Na Miraji (Ngazi aliyopandia mbinguni) ni haki, kwa hakika Nabii Rehema na amani ziwe juu yake, amepelekwa usiku kwa usiku, (hadi msikiti wa Aqsaa huko Palestina) kisha akapandishwa akiwa yu macho hadi mbinguni, kisha akafika hadi pale alipopataka Allah. Allah akamkirimu kwa alivyovitaka, na akamfunulia alivyomfunulia, “Moyo haukusema uwongo uliyoyaona.” ‘8’ Quran 53: 11 Nabii Rehema na amani ziwe juu yake Akhera na duniani. Na Hodhi alilokirimiwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, ni haki nayo ni kinywaji cha uma wake, na Shafaa (ponyo la kuwaombea watu watolewe motoni) Allah alilowawekea nalo ni kweli, kama lilivyopokelewa katika hadithi.
Na ile ahadi aliyoiweka Allah Mtukufu kwa Adam na kizazi chake ni ya kweli, kwa hakika Allah alijua idadi ya watakaoingia peponi na idadi ya watakaoingia motoni kwa jumla moja, na idadi hiyo haitozidi wala kupungua. Pia alijua matendo yao watakayoyafanya, na yote hayo yamewezeshwa kwa yalichoumbiwa, na matendo yanazingatiwa mwisho wake, na mwenye furaha ni yule aliyepewa furaha na hukumu ya Allah na mwenye tabu ni yule aliyepewa tabu na hukumu ya Allah.
Asili ya kadari (makadirio ya Allah) ni siri ya Allah kwa viumbe wake, hajamuonesha siri hiyo malaika aliyekaribu na Allah wala mtume aliyemtuma, na kujikita na kulitafiti sana jambo hili ni sababu ya kudhalilika, ngazi ya kunyimwa mazuri na ni daraja la kuchupa mipaka. Jihadhari sana na kulichunguza, kulifikiria na kuwa na shaka nalo. Kwa hakika Allah ameiziba elimu ya kadari kwa viumbe wake, na amewakataza kuilenga/kuikusudia kama alivyosema Allah Mtukufu katika kitabu chake: “Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaohojiwa kwa wayatendayo.” Quran  Al-Anbiyaai 23 Na atakayeuliza kwa nini amefanya hivi? Mtu huyo ameikataa hukumu ya kitabu, na anayeikataa hukumu ya kitabu ashakuwa miongoni mwa makafiri.
Haya ndio jumla ya mambo anayoyahitajia mtu mwenye nuru ya moyo miongoni mwa mawalii (wapenzi) wa Allah mtukufu.  Hii ni daraja ya wale walibobea katika elimu kwa kuwa elimu zipo aina mbili: elimu waliyonayo viumbe na elimu wasiokuwa nayo viumbe( )  kwa hiyo kupinga elimu uliyopo ni kukufuru. Na kujidai kuwa una elimu isiyokuwepo pia ni kukufuru. Imani haithibiti ispokuwa kwa kukubali elimu iliyopo na kuacha kuitafuta elimu isiyokuwepo.
Tunaamini ubao na kalamu na yote yaliyokuwemo na kuandikwa humo, lau kama viumbe wote wataungana juu ya jambo lililoandikwa na Allah kuwa liwepo na hao viumbe wakataka walifanye lisiwepo hawataweza. Pia lau kama viumbe wote wataungana juu ya jambo lisiloandikwa na Allah kuwa liwepo na hao viumbe wakataka walifanye liwepo hawataweza. Kalamu imeshakauka kwa vilivyopo hadi siku ya Kiama. Kisichomkosa mja hakikuwa cha kumpata pia kile kilichompata nacho hakikuwa cha kumkosa.
Mja lazima aelewe kuwa kwa hakika Allah kwa elimu yake ametangulia kukijua kila kiumbe miongoni mwa viumbe vyake na akavikadiria makadirio mazuri kabisa hayana upungufu, hayana wa kuyatilia maelezo, wa kuyaondosha, wa kuyageuza, wa kupunguza, wala kuzidisha miongoni mwa viumbe walioko katika mbingu na ardhi zake. Haya ni kifungo cha imani na misingi ya maarifa na kuikiri tauhidi ya Allah mtukufu pamoja na umola ulezi wake. Kama Allah mtukufu alivyosema katika kitabu chake: “Na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo”. Surat Al-Furqaan 2 Pia Allah amesema: “Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa.” Surat Ahzaabu 38.  
Ole wake yule atakayekuwa adui wa Kudura za Allah, na kuhudhurisha katika hili mtazamo wake wa moyo mgonjwa, kwa hakika mtu huyo kwa imani yake potofu amejitafutia siri ya kiza ya kutafiti undani wa yaliyofichikana mtokeo yake kwa hayo aliyoyasema atakuwa amerejea katika ufasiki na madhambi.   
Arshi na Kiti cha enzi ni haki, na Allah ni mwenye kujitosheleza hana shida na Arshi wala vilivyo chini yake au juu yake, amekizunguka kila kitu, huku amevifanya viumbe vyake kuwa vimeshindwa kuizunguka.  
Tunasema: Kwa hakika Allah amemjaalia Ibrahimu kuwa kipenzi chake, na akasema na Musa haki ya kusema naye, haya tunayamini, kuyasadikisha na kujisalimisha kwayo. Tunaamini Malaika, Mitume, Vitabu vilivyoteremshwa kwa mitume, tunashuhudia kuwa Mitume ilikuwa katika haki ya wazi. Watu wa kibla chetu tunawaita Waislamu waumini, muda wa kuwa wanayakubali yale aliyokuja nayo Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, pia wanayasadikisha yale yote aliyoyasema na kuyaeleza, wala hatujitumbukizi katika dhati ya Allah wala hatuipuzi dini ya Allah, wala hatuijadili Quran. Tunashuhudia kuwa Quran ni maneno ya Mola wa viumbe wote iliyoteremshwa na Malaika mwaminifu akamfundisha bwana wa mitume Muhammad Rehema na amaini ziwe juu yake, Quran ni maneno ya Allah mtukufu hayapo sawa na maneno yoyote miongoni mwa maneno ya viumbe, hatusemi kuwa Quran ameiumbwa wala hatuendi kinyume na jamaa ya waislamu wala hatumkufurishi yeyote miongoni mwa watu wa kibla kwa dhambi asiyoihalalisha. ( )
Wala hatusemi kuwa “Mwenye imani akitenda dhambi haidhuru”.
Tunataraji kwa Allah awasamehe wale wema miongoni mwa waumini na kuwaingiza peponi kwa rehema zake. Hatuna dhamana nao wala atushuhudii kuwa wataingia peponi ( ). Pia tunawaombea msamaha wale waovu miongoni mwa waumini, tunaogopa wasidhurike na hatuwakatishi tama.
Dhamana na kukata tamaa vinatoa mtu kutoka katika Uislamu. Kwa hiyo, njia ya haki kwa watu wa kibla yetu ipo baina ya mawali haya. Mja hatoki katika imani ispokuwa kwa kukanusha yale yaliyomuingiza katika Uislamu  )). Imani ni kukiri kwa ulimi na kusadikisha kwa matendo ( ).
Yote yaliyoswihi kutoka kwa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, miongoni mwa Sheria na Ubainifu wa yote ni haki. Imani ni moja ( ) na wenye imani kwa asili wapo sawasawa. Na tofauti za ubora miongoni mwao ni kwa kumcha na kumwogopa Mungu, kupingana na matamanio ya nafsi na kushikamana na yaliyomema. Waumini wote ni mawalii wa Mungu wa Rehema, na mbora wa Waislamu ni mtiifu sana miongoni mwao na mfuasi mzuri wa Quran.
Imani ni kumwani Allah, malaika zake, vitsbu vyske, mitume yake, siku ya Kiama na Kadari ya heri yake na shari yake, tamu yake na chungu yake zote zinatoka kwa Allah Mtukufu. Sisi tunaamini yote hayo, hatumtofautishi yeyote miongoni mwa mitume yake. Tunawasadikisha wote kwa yale waliokuja nayo.
Wenye madhambi makubwa (katika uma wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake) watakapokufa huku wakiwa wanampwekesha Allah wataingia motoni bila kuishi humo milele na watu hao wapo katika matakwa na hukumu ya Allah. Allah akipenda atawaghufiria na kuwasamehe kwa fadhila zake, kama ilivyotajwa na Allah Mtuku aliyetukuka katika kitabu chake: “…na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye… ”. Surat Al-Nisaa 48 na 116.
Ewe Mola, ewe Mlinzi wa Uislamu na watu wake tuthibitishe katika Uislamu hadi tukutane nawe kwa Uislamu. Pia tunaona kuwa inafaa kuswali nyuma ya mwema au mwovu miongoni mwa watu wa kibla pia kumsalia yeyote miongoni mwao. Wala hatumuingizi peponi au motoni yeyote miongoni mwao. Wala hatuwashuhudii wao kwa ukafiri, ushirikina wala unafiki kama hakijadhihiri kwao chochote katika hayo, na siri zao tunaziacha kwa Allah Mtuku.
Hutoenelei kuwa kuna mtu yeyote katika uma wa Muhammad, Rehema na amani ziwe juu yake kuwa anayestahiki kukatwa panga ispokuwa yule aliyewajibikiwa kupigwa panga. Wala hatuonelei kutoka katika kuwatii maimamu na watawala wetu hata kama watachupa mipaka, wala hatuwaombei laana, wala hutoi mkono wa kuwatii. Tunaonelea kuwa kuwatii wao ni lazima na ni miongoni mwa twaa kwa Allah Mukufu, ikiwa hawajaamrisha maasi. Tunawaombea uongofu na kusamehewa. Tunafuata Sunna na jamaa na kujiepusha michepuko, kwenda kinyume na kufarikiana. Tunaapenda waadilifu na waamini. Tunawabughudhi waovu na wahaini.  
Tunasema: Allah anajua yale yenye kututatiza kuyajua, tuaonelea kuwa kupaka juu ya Khofu mbili safarini na sio safarini kama ilivyokuja katika hadithi. Hija na Jihadi vinaendana na wenye mamlaka miongoni mwa Waislamu wema wao na waovu wao hadi kusimama kwa Kiama vitu hivyo havibatilishwi wala kutanguliwa na chochote.  
Tunaamini ukarimu wa Malaika waandishi kwa hakika Allah amewajaalia wao kwetu sisi wawe ni watunzaji (kumbukumbu), tunamwamini malaika wa mauti aliyepewa jukumu la kutoa roho za viumbe wote, tunaamini adhabu ya kaburi kwa mwenye kuistahiki, pia tunaamini maswali ya malaika waitwao Munkari na Nakiiri huko kaburini kuwa yapo, watauliza juu ya mungu wake, dini yake, nabii wake, nahabari zilizomfikia kuhusiana na mtume wa Allah, rehema na amani ziwe juu yake, pia kuhusu maswahaba, Allah awawie radhi.
Kaburi ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya peponi au ni shimo miongoni mwa mashimo ya moto. Tunaamini kufufuliwa na kulipwa matendo siku ya Kiyama, kufufuliwa na kuhesabiwa na kusoma kitabu, thawabu na adhabu. Njia nyembamba na mizani. Pepo na moto vimeumbwa havitoweki milele wala haviangamii. Na kwa hakika Allah Mtukufu ameumba pepo na moto kabla ya kuumba na akaviumbia watu wake, atakayemtaka miongoni mwao ataingia peponi kwa fadhila toka kwa Allah, na atakayemtaka miongoni mwao ataingia motoni kwa uadilifu wa Allah, na kila kimoja anatenda kwa mujibu wa alichowekea, pia atakuwa katika yale aliyoumbiwa.
Heri na shari zimekadiriwa kwa mja, na kule kuweza ambapo kwa ajili yake kitendo kinalazimika mfano kuafikishwa ambapo hakuwezi kujuzu kusifiwa kiumbe jambo hilo lipo pamoja na kitendo. Ama kuweza kwa upande wa kusihi na ukunjufu na kuweza na kusalimika kwa vifaa hivyo vinakuwa kabla ya tendo. Na kwa kuweza huku ndiko kunakofungamana mahubiri kama alivyosema Allah Mtukufu:  “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwakadiri ya iwezavyho…: Surat Baqara 286.
Matendo ya waja yameumbwa na Allah, kuchuma ni kwa waja. Allah Mtu hajawakalifisha ispokuwa yale wanayoyaweza. Na hakuna wanachokiweza ( ) zaidi ya kile walichokalifishwa kwacho na hii ndio fasili ya (hapana hila wala nguvu ila ni za Allah) tunasema: hakuna hila kwa yeyote wala harakati wala kubadilika kwa yeyote kuacha kumuasi Allah ila kwa msaada wa Allah. Na yeyote hana nguvu ya kuanza kumtii Allah na kuthibiti katika jambo hili ila kwa taufiki (kuwezeshwa) ya Allah.
Kila kitu kinaende kwa matakwa ya Allah Mtukufu, elimu yake, hukumu zake na kadari yake. Matakwa yake yameshinda matakwa yote. Hukumu zake zimeshinda hila zote. Anafanya atakavyo naye ni dhalimu milele,  ametakasika na kila baya na HIIN na ametakasika na kila dosari na upungufu. “Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaohojiwa kwa wayatendayo". Surt Al-Anbiyaau 23.
Dua za walio hai na sadaka ni manufaa kwa waliokufa, Allah Mtukufu anapokea dua, anakidhi haja haja na anamiliki kila kitu. Hamilikiwi na chochote. Haiwezekani kujitosheleza pasi na Allah Mtukufu hata kwa kupepesa jicho. Na atakayejifanya ametosheka hana haja ya Allah hata kwa kupepesa jicho ameshakufuru na kuwa kafiri na kuwa miongoni mwa watu wa HIINI. Allah anaghadhibika na kuridhia lakini si kama yeyote miongoni mwa wanadamu.
Tunawapenda Maswahaba wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wala hatchupi mipaka katika kumpenda yeyote miongoni mwao. Hatumbagui yeyote miongoni mwao. Tunawachukia wanaowachukia Maswahaba na kuwataja kwa yasiyo ya heri. Hatuwataji Maswahaba ila kwa heri. Kuwapenda wao ni dini, imani na ihsani. Kuwabughuzi wao ni kufuru, unafiki na kuchupa mipaka.
Tunathibitisha Ukhalifa baada ya Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake kuwa wa kwanza ni Abu Bakri Al-Swidiiqi, Allah amuwie radhi, na huku ni kufadhilisha na kumuweka mbele ya umma wote. Kisha Omar bin Al-Khatwaabi, Allah amuwie radhi, kisha Othmani, Allah amuwie radhi, kisha Ali, Allah amuwie radhi. Hawa ndio makhalifa waongofu na maimamu waongofu.
Kwa hakika Maswahaba kumi waliotajwa na kubashiriwa Pepo na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, tunawashuhudia kuwa wao ni watu wa Peponi kwa kuwa wameshuhudiwa hivyo na Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, na kauli yake ni kweli. Nao ni Abu Bakari, Omari, Othumani, Ali, Twalha, Zuberi, Saadi, Said, Abdulrahman bin Aufi na Abu Ubaida bin Al-Jaraah na huyu ndiye mtunza siri wa umma huu. Allah awawie radhi wote.
Atakayetoa kauli nzuri juu ya Maswahaba, wa Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, wake zake walioepukana na kila chafu, kizazi chake kilichotakaswa na kila chafu, Mtu huyo ameepukana na unafiki.
Wanazuoni wa Kisalafi waliotangulia, na waliokuja baada yao miongoni mwa Mataabiina ni watu wa heri, athari nzuri, fiqihi (ufahamu wa dini) na mtazamo mzuri. Hawataji ila yaliyomazuri, na atakayewataja kwa uovu mtu huyo yupo nje ya njia ya haki.
Hatumfadhilishi walii yeyote kuliko mtume yeyote miongoni mwa mitume, Rehema na amani ziwe juu yao na tunasema: Mtume mmoja ni mbora kuliko mawalii wote.
Tunaamini karama walizokuja nazo kuwa ni sahihi zikiwa zimetoka kwa wapokezi wa kuaminika.
Tunaamini alama za Kiama: miongoni mwazo ni kutokea kwa Dajali, kuteremka kwa Issa ibni Maryam, amani iwe juu yake, tunaamini kuwa jua litachomoza upande wa magharibi, kutokea kwa mnyama wa ardhini katika sehemu yake.
Hatumsadikishi kuhani wala muagua nyota (mpiga ramli) wala anayelingania kitu kilichokinyume na Kitabu na Sunnah na Ijimai ya umma.
Tunaamini kuwa Jamaa lipo katika haki, na kufarikiana nayo ni kupotea na kuadhibika.
Dini ya Allah ardhini na mbinguni ni moja, nayo ni Uislamu. Allah Mtukufu amesema: “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu…” Surat Al-Imrani 19. Na amesema tena:  “…Mimi, leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini…” Surat Al-Maaida 3.
Na Uislamu ni dini ya kati na kati baina ya ziada potofu na upungufu mbaya, baina ya kumfananisha Allah na kumuondolea sifa zake, baina ya imani ya (Ajabri na Alqadari) kulazimishwa na kukadiriwa, baina ya kujiamini mno na kukata tamaa. Hii ndio dini yetu na itakadi yetu kwa wazi na kwa siri. Sisi tunajitakasa kwa Allah na kila anayeenda kinyume na haya tuliyoyataja na kuyabainisha.   
Tunamuomba Allah Mtukufu atuthibitishe katika imani, na atufikishe mwisho wetu na imani hiyo, atukinge na matamanio ya nafsi yaliyo mbalimbali, pia atuepushe na rai za kufarikisha na madhehebu mabaya kama vile madhehebu ya Al-Mushabiha (ya kumfananisha Allah), Muutazila, Al-Jahamiya, Al-Jabriya, Al-Qadariya na wengineo miongoni mwa wale ambao wameenda kinyume na Sunnah Waljamaa. Wakaungana na upotevu. Sisi tunajitenga nao, na madhehebu hayo kwetu sisi yanazingatiwa kuwa ni upotovu na ubaya. Na kwa Allah ndipo tunapotarajia kulindwa na kuwafikishwa.
Mwisho wa akida ya Twahawiya, Allah amsamehe mtunzi wake na awanufaishe waja zake kwa utunzi huu.
[Akida ya Attwahawiya imeisha, Allah amsamehe mtunzi wake na awanufaishe kwayo waja zake]