MAWINGU YANAYOLETA MVUA

MAWINGU YANAYOLETA MVUA

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “ Naapa kwa mawingu yanayoleta mvua.” Aya ya 11 ya Suratul Tariq.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

 1.     Wingu wa juu unayarejesha maji yaliyogeuka kuwa mvuke  katika hali ya mvua.

 2.     Wingu wa juu unarejesha ardhini vimondo vingi na kuvirejesha kwenye anga la nje.

 3.     Wingu wa juu unairejesha mionzi yenye kuua viumbe hai na kuisukuma mbali na ardhi.

 4.     Wingu wa juu unaakisi mawimbi mafupi na ya kati ya redio kuyarejesha ardhini. Kwa hiyo tunaweza kuihesabu anga kama kioo chenye kuakisi miale na sumaku umeme. Ni wenye kuakisi au kurejesha mawimbi yasiyotumia waya na televisheni yanayorushwa angani na ambayo hurejeshwa baada ya kurushwa angani baada ya kuelekezwa kwenye tabaka za juu. Huu ndio msingi wa kazi ya vyombo vya kurusha matangazo ya idhaa na televisheni kupitia pande mbali mbali za ardhi.

 5.     Wingu wa juu unafanana na kioo chenye kuakisi joto  Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “ Naapa kwa mawingu yanayoleta mvua.” Aya ya 11 ya Suratul Tariq.

UHAKIKA WA KISAYANSI:

 1.     Wingu wa juu unayarejesha maji yaliyogeuka kuwa mvuke  katika hali ya mvua.

 2.     Wingu wa juu unarejesha ardhini vimondo vingi na kuvirejesha kwenye anga la nje.

 3.     Wingu wa juu unairejesha mionzi yenye kuua viumbe hai na kuisukuma mbali na ardhi.

 4.     Wingu wa juu unaakisi mawimbi mafupi na ya kati ya redio kuyarejesha ardhini. Kwa hiyo tunaweza kuihesabu anga kama kioo chenye kuakisi miale na sumaku umeme. Ni wenye kuakisi au kurejesha mawimbi yasiyotumia waya na televisheni yanayorushwa angani na ambayo hurejeshwa baada ya kurushwa angani baada ya kuelekezwa kwenye tabaka za juu. Huu ndio msingi wa kazi ya vyombo vya kurusha matangazo ya idhaa na televisheni kupitia pande mbali mbali za ardhi.

 5.     Wingu wa juu unafanana na kioo chenye kuakisi joto. Unafanya kazi kama ni ngao ya kujikinga na joto la jua wakati wa mchana. Pia unafanya kazi kama ni pazia wakati wa usiku, huzuia joto la ardhi lisisambaratike. Lau uwiano huu ukiteteruka, basi itakuwa ni vigumu kuishi katika ardhi, ama kwa joto kali mchana au baridi kali wakati wa usiku.

UPANDE WA MIUJIZA:

          Aya Tukufu ya Qurani, “Naapa kwa mawingu yanayoleta mvua.” Inaashiria kuwa sifa muhimu ya wingu wenye kuizunguka ardhi ndio wenye kuleta mvua . Watu wa kale wamefahamu kuwa ni wenye kuashiria mvua tu. Sayansi mpya imekuja kuimarisha maana ya kuleta mvua katika kusifia anga na kukusanya hali nyingi ambazo binadamu hakuzijua hapo awali. Neno kurejesha maana yake ni kukirejesha kitu sehemu kilipokuwa mwanzo. Maana yake ni kurejesha kitu katika muelekeo wa chimbuko lake mfano wa kurudisha mwangwi. Wingu hapa maana yake ni anga la ardhi na maelezo yana maana ya kuwepo pazia lenye kuuzunguka ambalo huirejeshea ardhi kila lenye manufaa na kufukuza kila lenye madhara. Imebainika kuwa neno kurejesha (kuleta mvua) lina maana zaidi ya kushuka mvua.  Na bila ya sifa hiyo ya anga, basi maisha yasingekaa sawa katika ardhi. Na kwa hii Qurani Tukufu imekusanya pamoja kwa neno moja sifa zote za anga zilizogunduliwa na sayansi mpya.